Ambwene Mwasongwe kwa sasa ndiyo icon ya nyimbo za injili

Boaz wimbo wake wa uongezeke nauelewa sana, jamaa anakuja kasi sana.
Noma sana
Mimi nipungue wewe uongezeke
Uongezeke Yesu uongezeke sana....

Na ana wimbo mpya wa "Unaweza"(Yeremia18)
Baadhi ya mashairi
..Bwana akamwambia Yeremia
Nenda nyumbani Kwa Mfinyanzi
Utamuona Mfinyanzi anavyofinyanga chombo
Kilichoharibika ,anakifinyanga Tena
Jinsi apendavyo yeye....
Yeremia 18

Muimbaji anaesoma neno la Mungu!
Ndo maana akiwa anaimba ,anahubiri pia,anaombea at the same time ,etc

Bila kusahau Dr Ipyana,Gwamaka(Essence of Worship)
 
Mimi nawakubali waimbaji wote wa nyimbo za injili kutoka Tz,maana wa kwetu Kenya miyeyusho Sana hawanaga Cha kuimba zaidi ya mashushu tu.
 
Kuna utofauti mkubwa sana kati ya Ambwene na Mwaitege,vip ukitazama kiuhalisia hapo unamuona nan ni mburudishaji?? Alaf usikariri mafunzo kutoka ndan ya biblia tu..wengne wanafunzwa na dunia ndipo hurejea kwenye iman na hapo ndo nyimbo zake zimeegemea...inaonekana humfatilii,au una chuki nae au ni mweupe tu huna unalolijua!!
 
Vijana wa kutoka mbeya hawajawahi kuniangusha
 
Mimi napenda Sana ile inayoitwa "ombi langu" hasa verse ya pili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…