A
NimeshangaaHuyo mwnafumzi ni dhaifu kweli kitaaluma. Hakupaswa kuacha chuo kisa msimamizi wake wa Tasnifu alimWambia hajafanya kitu.
Alipaswa kuomba kubadilishiwa mhadhiri ili aendelee na Tasnifu yake. Anakubali vipi pesa yake yote hiyo Tsh 15+M na muda wake vipotee Bure?
This is so sad.Miaka kadhaa nyuma wakati nipo Undergraduate pale Open University - Dar, ilibaki kidogo nisi-graduate sababu ya Mhadhiri aliyenisimamia Research, nilipambana kwa nguvu zote lakini aliniwekea pozi balaa, ilibidi nimfuate Mwalimu mwenzake kumuuliza mbona nimefanya kila kitu lakini nazungushwa tu, akaniambia “nyoosha mkono mdogo wangu”.
Iliniuma sana, nikafanya hivyo kishingo upande, akapitisha Research yangu. Sasa nikiwa Chuo cha Maji hapa Ubungo Dar nikichukua Master’s Degree (Shahada ya Uzamili) kuna mwenzetu amekutana na kisanga kinachofanana na kilichonikuta, ameshindwa kuvumilia, kabwaga manyanga.
Wakati wa Coursework, mwenzetu alipowasilisha wazo lake la utafiti (dissertation), wakati wa marekebisho kila kitu kilienda fresh, ilipofika zamu ya kutete hoja yake, Mhadhiri huyohuyo anayesimamia dissertation za Wanafunzi wa Shahada ya Uzamili aliyekuwa anasimamia, akamwambia mwishoni kabisa kuwa “hakuna chochote cha maana alichofanya katika research na hawezi ku-graduate”, akaishiwa nguvu kabisa.
Mshkaji ni Mtumishi wa Umma, akafikiria nguvu aliyotumia, ada, utafiti alioufanya, GPA, fedha kibao alizopoteza, akili yote kisha dakika ya 90 anaambiwa “Hamna kitu alichofanya”, amechoka ameona kuna maisha nje ya chuo.
Nadhani Serikali inatakiwa kuangalia hizi Sera za Elimu nchini, baadhi ya Wahadhiri wanatumia nguvu waliyonayo kuumiza Wanafunzi kwa kigezo kwamba “Huwezi kunifanya chochote”, Walimu wengi wa chuo wanaamini kufelisha Wanafunzi, kuwanyanyasa, waonesha wao wakubwa ndiyo elimu bora, si sawa.
Sehemu ya malalamiko ya mshkaji ambayo aliamua hadi kwenda kuandika kwenye group anasema:
“Mhadhiri anakutengenezea mazingira uonekane haufai, hujitambui wala hujui kwanini upo shule…”
“Sasa mtu akiweka kazi kwenye ma ChatGPT yake inamwambia huyu haja-analyze kitu fulani hivyo kazi nzima haifai!
“Nimetumia zaidi ya Sh 10m kufanya utafiti, Dr Magori anakuambia hujafanya kitu…
“Nikipiga hesabu Ada yangu na michango ni Sh 5M+, Research 10M+, Nauli, Hela za Lodge ili ukae na wenzako m-discuss, Miaka miwili, GPA yangu ya coursework daah nilivyoipambania ili ku-decorate cheti ila waapii. Daaa Dr. Magori!! Mungu atakulipa tu. Mliofanikiwa kuvuka, kila la kheri.”
Wapare kesi kwao ni jambo la kawaidaElim ya bongo ina maumivu yake,nakumbuka Michael Kadege PhD yake ilipatikana kwa njia ya mahakama baada ya Supervisor kushindwa kuthbitisha kasoro ya Thesis ya jamaa,na hapo alisha mzungusha mara kdhaa.
Kumbe ndio ilivyokuwa!Elim ya bongo ina maumivu yake,nakumbuka Michael Kadege PhD yake ilipatikana kwa njia ya mahakama baada ya Supervisor kushindwa kuthbitisha kasoro ya Thesis ya jamaa,na hapo alisha mzungusha mara kdhaa.