KERO Ameamua kuachana na Chuo cha Maji kisa ‘mateso’ ya Mhadhiri anayemsimamia ‘Dissertation’

KERO Ameamua kuachana na Chuo cha Maji kisa ‘mateso’ ya Mhadhiri anayemsimamia ‘Dissertation’

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Miaka kadhaa nyuma wakati nipo Undergraduate pale Open University - Dar, ilibaki kidogo nisi-graduate sababu ya Mhadhiri aliyenisimamia Research, nilipambana kwa nguvu zote lakini aliniwekea pozi balaa

Ilibidi nimfuate Mwalimu mwenzake kumuuliza mbona nimefanya kila kitu lakini nazungushwa tu, akaniambia “nyoosha mkono mdogo wangu”
Iliniuma sana, nikafanya hivyo kishingo upande, akapitisha Research yangu.

Sasa nikiwa Chuo cha Maji hapa Ubungo Dar nikichukua Master’s Degree (Shahada ya Uzamili) kuna mwenzetu amekutana na kisanga kinachofanana na kilichonikuta, ameshindwa kuvumilia, kabwaga manyanga.

Wakati wa Coursework, mwenzetu alipowasilisha wazo lake la utafiti (dissertation), wakati wa marekebisho kila kitu kilienda fresh.

Ilipofika zamu ya kutetea hoja yake, Mhadhiri huyohuyo anayesimamia dissertation za Wanafunzi wa Shahada ya Uzamili aliyekuwa anasimamia, akamwambia mwishoni kabisa kuwa “hakuna chochote cha maana alichofanya katika research na hawezi ku-graduate”, akaishiwa nguvu kabisa.

Mshkaji ni Mtumishi wa Umma, akafikiria nguvu aliyotumia, ada, utafiti alioufanya, GPA, fedha kibao alizopoteza, akili yote kisha dakika ya 90 anaambiwa “Hamna kitu alichofanya”, amechoka ameona kuna maisha nje ya chuo.

Nadhani Serikali inatakiwa kuangalia hizi Sera za Elimu nchini, baadhi ya Wahadhiri wanatumia nguvu waliyonayo kuumiza Wanafunzi kwa kigezo kwamba “Huwezi kunifanya chochote”

Walimu wengi wa chuo wanaamini kufelisha Wanafunzi, kuwanyanyasa, waonesha wao wakubwa ndiyo elimu bora, si sawa.

Sehemu ya malalamiko ya mshkaji ambayo aliamua hadi kwenda kuandika kwenye group anasema:

“Mhadhiri anakutengenezea mazingira uonekane haufai, hujitambui wala hujui kwanini upo shule…”

“Sasa mtu akiweka kazi kwenye ma ChatGPT yake inamwambia huyu haja-analyze kitu fulani hivyo kazi nzima haifai!

“Nimetumia zaidi ya Sh 10m kufanya utafiti, alafu mtu anakuambia hujafanya kitu…


“Nikipiga hesabu Ada yangu na michango ni Sh 5M+, Research 10M+, Nauli, Hela za Lodge ili ukae na wenzako m-discuss

Miaka miwili, GPA yangu ya coursework daah nilivyoipambania ili ku-decorate cheti ila wapi!


Pia soma ~ Serikali iangalie walimu wanaosimamia somo la Utafiti (Research) OPEN University, kuna mmoja ipo siku kitamkuta kitu
 
Huyo mwnafumzi ni dhaifu kweli kitaaluma. Hakupaswa kuacha chuo kisa msimamizi wake wa Tasnifu alimWambia hajafanya kitu.

Alipaswa kuomba kubadilishiwa mhadhiri ili aendelee na Tasnifu yake. Anakubali vipi pesa yake yote hiyo Tsh 15+M na muda wake vipotee Bure?
 
Huyo mwnafumzi ni dhaifu kweli kitaaluma. Hakupaswa kuacha chuo kisa msimamizi wake wa Tasnifu alimWambia hajafanya kitu.

Alipaswa kuomba kubadilishiwa mhadhiri ili aendelee na Tasnifu yake. Anakubali vipi pesa yake yote hiyo Tsh 15+M na muda wake vipotee Bure?
Nimeshangaa
 
Miaka kadhaa nyuma wakati nipo Undergraduate pale Open University - Dar, ilibaki kidogo nisi-graduate sababu ya Mhadhiri aliyenisimamia Research, nilipambana kwa nguvu zote lakini aliniwekea pozi balaa, ilibidi nimfuate Mwalimu mwenzake kumuuliza mbona nimefanya kila kitu lakini nazungushwa tu, akaniambia “nyoosha mkono mdogo wangu”.

Iliniuma sana, nikafanya hivyo kishingo upande, akapitisha Research yangu. Sasa nikiwa Chuo cha Maji hapa Ubungo Dar nikichukua Master’s Degree (Shahada ya Uzamili) kuna mwenzetu amekutana na kisanga kinachofanana na kilichonikuta, ameshindwa kuvumilia, kabwaga manyanga.

Wakati wa Coursework, mwenzetu alipowasilisha wazo lake la utafiti (dissertation), wakati wa marekebisho kila kitu kilienda fresh, ilipofika zamu ya kutete hoja yake, Mhadhiri huyohuyo anayesimamia dissertation za Wanafunzi wa Shahada ya Uzamili aliyekuwa anasimamia, akamwambia mwishoni kabisa kuwa “hakuna chochote cha maana alichofanya katika research na hawezi ku-graduate”, akaishiwa nguvu kabisa.

Mshkaji ni Mtumishi wa Umma, akafikiria nguvu aliyotumia, ada, utafiti alioufanya, GPA, fedha kibao alizopoteza, akili yote kisha dakika ya 90 anaambiwa “Hamna kitu alichofanya”, amechoka ameona kuna maisha nje ya chuo.

Nadhani Serikali inatakiwa kuangalia hizi Sera za Elimu nchini, baadhi ya Wahadhiri wanatumia nguvu waliyonayo kuumiza Wanafunzi kwa kigezo kwamba “Huwezi kunifanya chochote”, Walimu wengi wa chuo wanaamini kufelisha Wanafunzi, kuwanyanyasa, waonesha wao wakubwa ndiyo elimu bora, si sawa.

Sehemu ya malalamiko ya mshkaji ambayo aliamua hadi kwenda kuandika kwenye group anasema:

“Mhadhiri anakutengenezea mazingira uonekane haufai, hujitambui wala hujui kwanini upo shule…”

“Sasa mtu akiweka kazi kwenye ma ChatGPT yake inamwambia huyu haja-analyze kitu fulani hivyo kazi nzima haifai!

“Nimetumia zaidi ya Sh 10m kufanya utafiti, Dr Magori anakuambia hujafanya kitu…


“Nikipiga hesabu Ada yangu na michango ni Sh 5M+, Research 10M+, Nauli, Hela za Lodge ili ukae na wenzako m-discuss, Miaka miwili, GPA yangu ya coursework daah nilivyoipambania ili ku-decorate cheti ila waapii. Daaa Dr. Magori!! Mungu atakulipa tu. Mliofanikiwa kuvuka, kila la kheri.”
This is so sad.
 
Pole kwa jamaa na watanganyika wengine. Sasa mabinti inakuwaje??? Hizi mambo zinatia hhasirq, je PhD itakuwa vipi?
 
Usiwe siriaz sana kuliko wanaostahili kuwa serious!

Elimu yetu inatuandas kuwa watumwa wa wanasiasa na sera zao,hii imekua kwa miaka mingi sana!
Cha ajabu unatumia fedha kibao ili uendelee kuwa mtumwa zaidi kwao!!

Niliiona elimu niyoipotezea Miaka 17 Haina maana nikiwa udsm miaka 3!

Sikuona umuhimu wake zaidi ya ku strive upate cheti tu!!
 
Safari ya elimu nchini ina maumivu sana.Unapambana kutokea malezi magumu unafika elimu ya juu ambayo umeamua kuwa fani yako itakuwa ni hii halafu mtu anakusumbua tu bila sababu.Mwalimu mmoja aliuliza "hapa darasani mpo wangapi,akaambiwa course ina watu 120 akasema atafyeka vichwa kama 50 kwanza semister ya kwanza kwa hiyo tujiandae waulizeni wenzenu." KUFELISHA IMEKUWA SIFA NCHINI.Mwambie mwamba arudi na aombe kubadilishiwa msimamizi.
 
Duh pole sana, hakuna njia nyingine? Mil 10 nyingi aisee
 
Elim ya bongo ina maumivu yake,nakumbuka Michael Kadege PhD yake ilipatikana kwa njia ya mahakama baada ya Supervisor kushindwa kuthbitisha kasoro ya Thesis ya jamaa,na hapo alisha mzungusha mara kdhaa.
Wapare kesi kwao ni jambo la kawaida
 
Lecturer huyo tunamvukia maji tunaenda kumuomba Mungu anavunjiwa nazi 7 asipo wehuka akili niite Mbwa !!!

Mi hawa ndio nawapendaga hawa, Nazipendaga hizi league kinoma noma.

Mna muendekeza tu huyo.
 
Hivi ni yeye kamwaga manyanga au kashindwa shule?

Mwalimu wake anayemtahini katamka waziwazi kuwa hakuna kitu umefanya na huwezi ku graduate, hii sio maana yake kuwa dissertation yake haina kitu tangible?

By the way kutumia 10m sio ndio ishara moja kwa moja unafaulu
 
Back
Top Bottom