Amebadilika siku chache kabla ya mahari

Nakushauri tulia endelea na yako. Japokuwa ni mwanamme mwenzangu kwa hilo simtetei. Anaongozwa na akili za ndugu zake. Kwa hiyo upendo hapo haupo tena.

Kwanza mahari huwa haimaliziki. Huta ukiambiwa milioni unaweza toa laki nne ukabeba mke na maisha yakaendelea. Ukalipa kidogo kidogo na wengi hawamalizagi. Kapewa mke kwengine jikate hata mbususu usimpe tena.
 
Jamani pole najua unachopitia, nayahisi maumivu unayopitia
 
Mkuu pole sana, nimejaribu kukivaa kiatu chako , nakusihi uchukulie mambo Kama mipango ya Mungu, sioni haja ya wewe kuumia kwa Jambo ambalo huenda mwenyezi Mungu hakuwahi kukupangia kuwa mwili mmoja na huyo boy wako, lakini pia tambua kuwa likuepukalo lina heri nawe, huenda Mungu kakuepusha makubwa huko mbeleni, lakini Mungu mwenyewe anatuambia kuwa alitujua tangu tuko tumboni mwa mama zetu na mkanda mzima wa Maisha yetu anao yeye, na chote tunachokifanya na kukipitia hapa duniani yeye anajua. Soma yeremia 1:5(a)Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni.

Kikubwa zaidi sahau nausiwaze kuhusu ndugu kuwa watakuonaje baada ya jamaa kuishia mitini, wewe songa mbele na Maisha yako, sio kila mahusiano ya kimapenzi tunayoanzisha lazima yazae ndoa. Tulia utapata aliye sahihi kwako, huyo hakuwa mtu sahihi kwako kulingana na nguvu za kiroho.

Hebu jiulize kidogo, je unatatizo, Kama jibu ni ndiyo , jiulize tena je, unao uwezo wa kulitatua, Kama jibu Ni ndiyo Basi relax na hauna haja ya kuumiza moyo wako, lakini pia Kama jibu ni hapana pia relax maana hunao uwezo wa kulitatuta tatizo hilo.

Mwisho mimi naona kuwa ulipaswa kumdodosa boy wako kabla hajapeleka posa, ungemuuliza je kwake yeye ni kiasi gani Cha mahali anaweza lipia , baada ya hapo ungewasiliana na wazazi wako na kuwaambia kuwa huyu boy wangu uwezo wake wa kutoa mahali ni kiasi kadhaa hivyo wasizidishe, hii changamoto isingejitokeza, Mimi kabula ya kwenda unyakyusani girl wangu aliniuliza uwezo wangu wa mahali baada ya hapo akawajulisha ndugu zake , hivyo nilipopeleka posa sikusumbuka sana,ilikuwa Kama kumsukuma mlevi kwenye mtelemko, lakini pia ulipaswa kuzingatia tamaduni na makabila yenu, yaani upate mwanamme wa pwani harafu wewe(binti) msukuma , balaa lake wakati wa kuelewana mahali ni kubwa sana, maana pwani ukiwa na sh 200,000/= unapata mke.So Ni ngumu kumuambia jamaa wa pwani atoe mahali ya ngombe ishirini.


Pole sana kwako mtoa mada.
 
Ahsante pia. Nilikuwa muwazi kwake kwa kiwango kikubwa. Hili limenipa funzo kubwa sana. Sikumtegemea kwa jinsi alivyo.
 
Amiin.
 
Kwakawaida mtu ukikaanae kwamuda mrefu kuna kujisahau ( kujiachia) au Dada yangu ulijisahau kuwa kunasiku itafika Mahari itahusika - kutokana na ule muachio ulio jiachia bahati mbaya nae jamaa akapitia MULEMULE
 
Ahsante sana. Kabla ya yote alibainisha kiwango alichokuwa nacho. Hata gharama za mwisho zililenga hapohapo baada ya kuieleza familia yangu. Lakini tayari alishafanya maamuzi. Nilijitahidi kumuomba aje na kiwango chochote alichonacho lakini ikawa ngumu tena kwake. Mambo ya Mungu ni mengi ni njia zake hazichunguziki.
 
Alirudi na kusema tuendelee kuwa wapenzi. Nilipohitaji majibu kuhusu mustakabali na hatma ya haya yote hakuweza kutoa majibu. Nikaona nia yake ni kunipotezea muda na kunichezea. Hivyo, nikasitisha mawasiliano nae.
 
Alirudi na kusema tuendelee kuwa wapenzi. Nilipohitaji majibu kuhusu mustakabali na hatma ya haya yote hakuweza kutoa majibu. Nikaona nia yake ni kunipotezea muda na kunichezea. Hivyo, nikasitisha mawasiliano nae.
Sasa haya ndio maamuzi ya ki super woman. Hesabu hasara tulizana. Tafuta pesa mammy wanaume ni washenzi tuu.🤣🤣🤣🤣
 
Kwakawaida mtu ukikaanae kwamuda mrefu kuna kujisahau ( kujiachia) au Dada yangu ulijisahau kuwa kunasiku itafika Mahari itahusika - kutokana na ule muachio ulio jiachia bahati mbaya nae jamaa akapitia MULEMULE
Inawezekana yeye akawa na nafasi xaidi ya kusemea hili.
 
Usifurahie ee adui yangu. Niangukapo nitasimama tena..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…