Amebadilika siku chache kabla ya mahari

Amebadilika siku chache kabla ya mahari

Salaam kwenu nyote.

Ninaomba ushauri wenu kwenu Kaka zangu na Dada zangu. Mimi ni binti.

Nimekutana na changamoto katika mahusiano yangu. Kisa ni hiki.

Nilikuwa katika mahusiano na kijana mmoja kwa takriban miaka 4. Baadae ikaonekana ni vema tufahamishe mahusiano haya ngazi ya wazazi. Kijana alikuja nyumbani kwa tararibu zote na kupangiwa mahari. Wakati wote huo mimi na kijana tuko vizuri na mawasiliano kwa hakika yalikuwa mazuri mno. Naweza kusema hakukuwa na jambo au tatizo baina yetu na mwenzangu ambalo labda lingekuwa kikwazo.

Hata hivyo, week moja kabla kuelekea siku ya mahari mwenzangu alinifahamisha kwamba wamehairisha kuja nyumbani kwetu sababu familia yake imeona gharama walizopangiwa ni kubwa. Naye alishikilia msimamo kwamba anaungana na familia yake.. Nilijitahidi sana kumweleza kwamba waje na gharama walizojiandaa nazo lakini haikuwezekana tena kwa mwenzangu. Ni kama alishaamua kusitisha jambo hili na mahusiano yote kwa ujumla na kwa hivyo sikuweza kubadili chochote kutokea hapo.

Nimejitahidi mara kadhaa kutaka kujua iwapo kuna sababu nyingine ya sababu hiyo lakin mara zote mwenzangu amekuwa akijikita katika sababu tajwa hapo juu. Hata ninapomuuliza mwenzangu juu ya nini kinachoendelea mpka wakati huu bado hanipi majibu. Kimsingi, inaonekana hakuna mahusiano tena kwa sasa.

Ninaumia kwa namna mambo yalivyoenda na yalivyohitimishwa kwa namna isiyotarajika. ona ni kama ndoto, labda nipo ndotoni lakini ni ukweli ambao watu wanapitia. Nipo katika wakati mgumu mno, ukizingatia kwamba taarifa za jambo hili ziliwaslishwa kwa ndugu, jamaa na marafiki.

Nimekuja kwenu naomba ushauri, nahitajika kufanya nini ili niweze kuchukuliana na changamoto hii? Kuna wakati nashindwa kama binadamu naogopa kumfuru Mungu wangu. Nashindwa kusahau na namkumbuka sana kila wakati.
Nakushauri tulia endelea na yako. Japokuwa ni mwanamme mwenzangu kwa hilo simtetei. Anaongozwa na akili za ndugu zake. Kwa hiyo upendo hapo haupo tena.

Kwanza mahari huwa haimaliziki. Huta ukiambiwa milioni unaweza toa laki nne ukabeba mke na maisha yakaendelea. Ukalipa kidogo kidogo na wengi hawamalizagi. Kapewa mke kwengine jikate hata mbususu usimpe tena.
 
Jamani pole najua unachopitia, nayahisi maumivu unayopitia
 
Mkuu pole sana, nimejaribu kukivaa kiatu chako , nakusihi uchukulie mambo Kama mipango ya Mungu, sioni haja ya wewe kuumia kwa Jambo ambalo huenda mwenyezi Mungu hakuwahi kukupangia kuwa mwili mmoja na huyo boy wako, lakini pia tambua kuwa likuepukalo lina heri nawe, huenda Mungu kakuepusha makubwa huko mbeleni, lakini Mungu mwenyewe anatuambia kuwa alitujua tangu tuko tumboni mwa mama zetu na mkanda mzima wa Maisha yetu anao yeye, na chote tunachokifanya na kukipitia hapa duniani yeye anajua. Soma yeremia 1:5(a)Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni.

Kikubwa zaidi sahau nausiwaze kuhusu ndugu kuwa watakuonaje baada ya jamaa kuishia mitini, wewe songa mbele na Maisha yako, sio kila mahusiano ya kimapenzi tunayoanzisha lazima yazae ndoa. Tulia utapata aliye sahihi kwako, huyo hakuwa mtu sahihi kwako kulingana na nguvu za kiroho.

Hebu jiulize kidogo, je unatatizo, Kama jibu ni ndiyo , jiulize tena je, unao uwezo wa kulitatua, Kama jibu Ni ndiyo Basi relax na hauna haja ya kuumiza moyo wako, lakini pia Kama jibu ni hapana pia relax maana hunao uwezo wa kulitatuta tatizo hilo.

Mwisho mimi naona kuwa ulipaswa kumdodosa boy wako kabla hajapeleka posa, ungemuuliza je kwake yeye ni kiasi gani Cha mahali anaweza lipia , baada ya hapo ungewasiliana na wazazi wako na kuwaambia kuwa huyu boy wangu uwezo wake wa kutoa mahali ni kiasi kadhaa hivyo wasizidishe, hii changamoto isingejitokeza, Mimi kabula ya kwenda unyakyusani girl wangu aliniuliza uwezo wangu wa mahali baada ya hapo akawajulisha ndugu zake , hivyo nilipopeleka posa sikusumbuka sana,ilikuwa Kama kumsukuma mlevi kwenye mtelemko, lakini pia ulipaswa kuzingatia tamaduni na makabila yenu, yaani upate mwanamme wa pwani harafu wewe(binti) msukuma , balaa lake wakati wa kuelewana mahali ni kubwa sana, maana pwani ukiwa na sh 200,000/= unapata mke.So Ni ngumu kumuambia jamaa wa pwani atoe mahali ya ngombe ishirini.

Pole sana kwako mtoa mada.
 
Fuatilia kwa makini nadhani utagundua kipi kimeingikia jambo lako, au kuna kitu hukiweka wazi kwa kulinda mapenzi yenu, na baada ya kupanga siku ya nahari na ndugu zako wengi kupata taarifa ya ujio wa wageni - siunajua ikishaingia kwenya familia na marafiki majirani kulijua hilo KATIYENU huwezi kujua labda amemwaga FIGISU, Pole Kila linalotokea chini ya jua lina sababu, muombe Mungu akupe mume mwema na mwenye upendo
Ahsante pia. Nilikuwa muwazi kwake kwa kiwango kikubwa. Hili limenipa funzo kubwa sana. Sikumtegemea kwa jinsi alivyo.
 
Fuatilia kwa makini nadhani utagundua kipi kimeingikia jambo lako, au kuna kitu hukiweka wazi kwa kulinda mapenzi yenu, na baada ya kupanga siku ya nahari na ndugu zako wengi kupata taarifa ya ujio wa wageni - siunajua ikishaingia kwenya familia na marafiki majirani kulijua hilo KATIYENU huwezi kujua labda amemwaga FIGISU, Pole Kila linalotokea chini ya jua lina sababu, muombe Mungu akupe mume mwema na mwenye upendo
Amiin.
 
Kwakawaida mtu ukikaanae kwamuda mrefu kuna kujisahau ( kujiachia) au Dada yangu ulijisahau kuwa kunasiku itafika Mahari itahusika - kutokana na ule muachio ulio jiachia bahati mbaya nae jamaa akapitia MULEMULE
 
Mkuu pole sana, nimejaribu kukivaa kiatu chako , nakusihi uchukulie mambo Kama mipango ya Mungu, sioni haja ya wewe kuumia kwa Jambo ambalo huenda mwenyezi Mungu hakuwahi kukupangia kuwa mwili mmoja na huyo boy wako, lakini pia tambua kuwa likuepukalo lina heri nawe, huenda Mungu kakuepusha makubwa huko mbeleni, lakini Mungu mwenyewe anatuambia kuwa alitujua tangu tuko tumboni mwa mama zetu na mkanda mzima wa Maisha yetu anao yeye, na chote tunachokifanya na kukipitia hapa duniani yeye anajua. Soma yeremia 1:5(a)Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni.

Kikubwa zaidi sahau nabusiwaze kuhusu ndugu kuwa watakuonaje baada ya jamaa kuishia mitini, wewe songa mbele na Maisha yako, sio kila mahusiano ya kimapenzi tunayoanzisha lazima yazae ndoa. Tulia utapata aliye sahihi kwako, huyo hakuwa mtu sahihi kwako kulingana na nguvu za kiroho.

Hebu jiulize kidogo, je unatatizo, Kama jibu ni ndiyo , jiulize tena je, unao uwezo wa kulitatua, Kama jibu Ni ndiyo Basi relax na hauna haja ya kuumiza moyo wako, lakini pia Kama jibu ni hapana pia relax maana hunao uwezo wa kulitatuta tatizo hilo.

Mwisho miki5 naona kuwa ulipaswa kumdodosa boy wako kabla hajapeleka posa, ungemuuliza je kwake yeye ni kiasi gani Cha mahali anaweza lipia , baada ya hapo ungewasiliana na wazazi wako na kuwaambia kuwa huyu boy wangu uwezo wake wa kutoa mahali ni kiasi kadhaa hivyo wasizidishe, hii changamoto isingejitokeza, Mimi kabula ya kwenda unyakyusani girl wangu aliniuliza uwezo wangu wa mahali baada ya hapo akawajulisha ndugu zake , hivyo nilipopeleka posa sikusumbuka sana,ilikuwa Kama kumsukuma mlevi kwenye mtelemko, lakini pia ulipaswa kuzingatia tamaduni na makabila yenu, yaani upate mwanamme wa pwani harafu wewe(binti) msukuma , balaa lake wakati wa kuelewana mahali ni kubwa sana, maana pwani ukiwa na sh 200,000/= unapata mke.So Ni ngumu kumuambia jamaa wa pwani atoe mahali ya ngombe ishirini.

Pole sana kwako mtoa mada.
Ahsante sana. Kabla ya yote alibainisha kiwango alichokuwa nacho. Hata gharama za mwisho zililenga hapohapo baada ya kuieleza familia yangu. Lakini tayari alishafanya maamuzi. Nilijitahidi kumuomba aje na kiwango chochote alichonacho lakini ikawa ngumu tena kwake. Mambo ya Mungu ni mengi ni njia zake hazichunguziki.
 
Nakushauri tulia endelea na yako. Japokuwa ni mwanamme mwenzangu kwa hilo simtetei. Anaongozwa na akili za ndugu zake. Kwa hiyo upendo hapo haupo tena.

Kwanza mahari huwa haimaliziki. Huta ukiambiwa milioni unaweza toa laki nne ukabeba mke na maisha yakaendelea. Ukalipa kidogo kidogo na wengi hawamalizagi. Kapewa mke kwengine jikate hata mbususu usimpe tena.
Alirudi na kusema tuendelee kuwa wapenzi. Nilipohitaji majibu kuhusu mustakabali na hatma ya haya yote hakuweza kutoa majibu. Nikaona nia yake ni kunipotezea muda na kunichezea. Hivyo, nikasitisha mawasiliano nae.
 
Sasa haya ndio maamuzi ya ki super woman. Hesabu hasara tulizana. Tafuta pesa mammy wanaume ni washenzi tuu.🤣🤣🤣🤣
 
Kwakawaida mtu ukikaanae kwamuda mrefu kuna kujisahau ( kujiachia) au Dada yangu ulijisahau kuwa kunasiku itafika Mahari itahusika - kutokana na ule muachio ulio jiachia bahati mbaya nae jamaa akapitia MULEMULE
Inawezekana yeye akawa na nafasi xaidi ya kusemea hili.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] pole yataisha
Usifurahie ee adui yangu. Niangukapo nitasimama tena..!
 
Back
Top Bottom