Amebadilika siku chache kabla ya mahari

Amebadilika siku chache kabla ya mahari

Pole sana.Ndoa hupangwa na Mungu.Kama huyo jamaa amebadili uamuzi muache aende, maana yawezekana ungefunga naye ndoa angekuja kubadilika na ungeona rangi zote.Usilazimishe ndoa,Kama Mungu amepanga uoelewe utaolewa tu bado hujachelewa.Usijipe mawazo,fanya ibada na kadiri siku zinavyoenda utamsahau.
 
Salaam kwenu nyote.

Ninaomba ushauri wenu kwenu Kaka zangu na Dada zangu. Mimi ni binti.

Nimekutana na changamoto katika mahusiano yangu. Kisa ni hiki.

Nilikuwa katika mahusiano na kijana mmoja kwa takriban miaka 4. Baadae ikaonekana ni vema tufahamishe mahusiano haya ngazi ya wazazi. Kijana alikuja nyumbani kwa tararibu zote na kupangiwa mahari. Wakati wote huo mimi na kijana tuko vizuri na mawasiliano kwa hakika yalikuwa mazuri mno. Naweza kusema hakukuwa na jambo au tatizo baina yetu na mwenzangu ambalo labda lingekuwa kikwazo.

Hata hivyo, week moja kabla kuelekea siku ya mahari mwenzangu alinifahamisha kwamba wamehairisha kuja nyumbani kwetu sababu familia yake imeona gharama walizopangiwa ni kubwa. Naye alishikilia msimamo kwamba anaungana na familia yake.. Nilijitahidi sana kumweleza kwamba waje na gharama walizojiandaa nazo lakini haikuwezekana tena kwa mwenzangu. Ni kama alishaamua kusitisha jambo hili na mahusiano yote kwa ujumla na kwa hivyo sikuweza kubadili chochote kutokea hapo.

Nimejitahidi mara kadhaa kutaka kujua iwapo kuna sababu nyingine ya sababu hiyo lakin mara zote mwenzangu amekuwa akijikita katika sababu tajwa hapo juu. Hata ninapomuuliza mwenzangu juu ya nini kinachoendelea mpka wakati huu bado hanipi majibu. Kimsingi, inaonekana hakuna mahusiano tena kwa sasa.

Ninaumia kwa namna mambo yalivyoenda na yalivyohitimishwa kwa namna isiyotarajika. ona ni kama ndoto, labda nipo ndotoni lakini ni ukweli ambao watu wanapitia. Nipo katika wakati mgumu mno, ukizingatia kwamba taarifa za jambo hili ziliwaslishwa kwa ndugu, jamaa na marafiki.

Nimekuja kwenu naomba ushauri, nahitajika kufanya nini ili niweze kuchukuliana na changamoto hii? Kuna wakati nashindwa kama binadamu naogopa kumfuru Mungu wangu. Nashindwa kusahau na namkumbuka sana kila wakati.
Kabila gani wewe? Na mahari ilikuwa kiasi gani?
 
Mapenzi yakikuendea vizuri fresh ngoja mambo yavurugike ndio utajua hujui.
Na kwa nini yakuvurugikie...ujue umetaka mwenyewe tu.

Kama huyu dada yeye miaka minne mbusus inaliwa tuu huoni kuwa hamna muoaji hapo?

Wanawake most of the time mnalaume wanaume lakini ni uinga wenu wenyewe ndio unawapelekea huko.

Miaka minne mnachunguzana nini?
 
Pole sana.Ndoa hupangwa na Mungu.Kama huyo jamaa amebadili uamuzi muache aende, maana yawezekana ungefunga naye ndoa angekuja kubadilika na ungeona rangi zote.Usilazimishe ndoa,Kama Mungu amepanga uoelewe utaolewa tu bado hujachelewa.Usijipe mawazo,fanya ibada na kadiri siku zinavyoenda utamsahau.
Acheni utani bwana, yaani mgegeduane kabla ya ndoa kitu kilichokatazwa alafu tena mseme ndoa upangwa na mungu. Kweli are we serious!???
 
Na kwa nini yakuvurugikie...ujue umetaka mwenyewe tuu.
Kama huyu dada yeye miaka minne mbusus inaliwa tuu huoni kuwa hamna muoaji hapo?
Wannawake most of the time mnalaume wanaume lakini ni uinga wenu wenyewe ndio unawapelekea huko. Miaka minne mnachunguzana nini?
Kwa hiyo kama tunarudi nyuma unashauri angemuacha huyo mwanaume au angefanyaje?
 
Mwanamke unatakiwa uniamini bwana...if u quality lady mwanaume unampa miaka miwili, its either we tie the knot or its bye bye.

Ila wengi wenu hamjiamini yaani kwa kuwa society imeweka kuwa mwanaume ndio ana propose basi mnabembeleza weee ata kama mnafangiwa ujinga.

Huyu alitakiwa kumpiga chini after two years basi. Yaani wee unageggedwa tuu miaka minne. Loh..u ladies dont love urselves at all!!!!
 
Haya tutabadilika.
 
Fuatilia kwa makini nadhani utagundua kipi kimeingikia jambo lako, au kuna kitu hukiweka wazi kwa kulinda mapenzi yenu, na baada ya kupanga siku ya nahari na ndugu zako wengi kupata taarifa ya ujio wa wageni - siunajua ikishaingia kwenya familia na marafiki majirani kulijua hilo KATIYENU huwezi kujua labda amemwaga FIGISU, Pole Kila linalotokea chini ya jua lina sababu, muombe Mungu akupe mume mwema na mwenye upendo
nenda kwa mwamposa tu kuna mchawi kwa ndugu zako huko ...amerogwa huyo
 
Salaam kwenu nyote.

Ninaomba ushauri wenu kwenu Kaka zangu na Dada zangu. Mimi ni binti.

Nimekutana na changamoto katika mahusiano yangu. Kisa ni hiki.

Nilikuwa katika mahusiano na kijana mmoja kwa takriban miaka 4. Baadae ikaonekana ni vema tufahamishe mahusiano haya ngazi ya wazazi. Kijana alikuja nyumbani kwa tararibu zote na kupangiwa mahari. Wakati wote huo mimi na kijana tuko vizuri na mawasiliano kwa hakika yalikuwa mazuri mno. Naweza kusema hakukuwa na jambo au tatizo baina yetu na mwenzangu ambalo labda lingekuwa kikwazo.

Hata hivyo, week moja kabla kuelekea siku ya mahari mwenzangu alinifahamisha kwamba wamehairisha kuja nyumbani kwetu sababu familia yake imeona gharama walizopangiwa ni kubwa. Naye alishikilia msimamo kwamba anaungana na familia yake.. Nilijitahidi sana kumweleza kwamba waje na gharama walizojiandaa nazo lakini haikuwezekana tena kwa mwenzangu. Ni kama alishaamua kusitisha jambo hili na mahusiano yote kwa ujumla na kwa hivyo sikuweza kubadili chochote kutokea hapo.

Nimejitahidi mara kadhaa kutaka kujua iwapo kuna sababu nyingine ya sababu hiyo lakin mara zote mwenzangu amekuwa akijikita katika sababu tajwa hapo juu. Hata ninapomuuliza mwenzangu juu ya nini kinachoendelea mpka wakati huu bado hanipi majibu. Kimsingi, inaonekana hakuna mahusiano tena kwa sasa.

Ninaumia kwa namna mambo yalivyoenda na yalivyohitimishwa kwa namna isiyotarajika. ona ni kama ndoto, labda nipo ndotoni lakini ni ukweli ambao watu wanapitia. Nipo katika wakati mgumu mno, ukizingatia kwamba taarifa za jambo hili ziliwaslishwa kwa ndugu, jamaa na marafiki.

Nimekuja kwenu naomba ushauri, nahitajika kufanya nini ili niweze kuchukuliana na changamoto hii? Kuna wakati nashindwa kama binadamu naogopa kumfuru Mungu wangu. Nashindwa kusahau na namkumbuka sana kila wakati.
I know...I feel your situation ..you real love the guy,

Haya maisha yamebeba mambo mengi...hakuna aijuae kesho...

Nacho amini hakuna mtu au kitu kinacho weza kuwazuia watu wakipendana sio dini,Mila, tamaduni

Nilie mpenda nilitegemea yes I do...yey akajibu tue marafik...
Yeye ndie nili mpenda hasa...kisa mm sio Roman Catholic

No 2 yeye alinipenda hasa na nili mwambia na mtu still aliendelea kunipenda vile vile....

Namba 3 yeye ndie wife material ana Kila sifa na vigezo ila moyo una mchukulia powaaa...

Maisha haya nayaheshimu Sanaa... We're still breathing...life goes on..Mungu ni mwema wakati wote...
 
Acheni utani bwana, yaani mgegeduane kabla ya ndoa kitu kilichokatazwa alafu tena mseme ndoa upangwa na mungu. Kweli are we serious!???
Kwahiyo unataka kusema hawa waliokwenye ndoa wote walioana wakiwa bikira? Asikudanganye mtu Kama Mungu hajaruhusu Jambo haliwezi kutendeka, hivyo hiyo ndoa ni mpango wa Mungu isifungwe.
 
Huyo ameamua kwenda, muache aende hata kama inauma na ni vigumu.

Kwahiyo unataka kusema hawa waliokwenye ndoa wote walioana wakiwa bikira? Asikudanganye mtu Kama Mungu hajaruhusu Jambo haliwezi kutendeka, hivyo hiyo ndoa ni mpango wa Mungu isifungwe.
Sasa mbona tunapelekeana jela watu wakiiba au kuua...sii mipango ya mungu tuachie tuu wai e maana mungu ndio kawapangia hivyo
 
Salaam kwenu nyote.

Ninaomba ushauri wenu kwenu Kaka zangu na Dada zangu. Mimi ni binti.

Nimekutana na changamoto katika mahusiano yangu. Kisa ni hiki.

Nilikuwa katika mahusiano na kijana mmoja kwa takriban miaka 4. Baadae ikaonekana ni vema tufahamishe mahusiano haya ngazi ya wazazi. Kijana alikuja nyumbani kwa tararibu zote na kupangiwa mahari. Wakati wote huo mimi na kijana tuko vizuri na mawasiliano kwa hakika yalikuwa mazuri mno. Naweza kusema hakukuwa na jambo au tatizo baina yetu na mwenzangu ambalo labda lingekuwa kikwazo.

Hata hivyo, week moja kabla kuelekea siku ya mahari mwenzangu alinifahamisha kwamba wamehairisha kuja nyumbani kwetu sababu familia yake imeona gharama walizopangiwa ni kubwa. Naye alishikilia msimamo kwamba anaungana na familia yake.. Nilijitahidi sana kumweleza kwamba waje na gharama walizojiandaa nazo lakini haikuwezekana tena kwa mwenzangu. Ni kama alishaamua kusitisha jambo hili na mahusiano yote kwa ujumla na kwa hivyo sikuweza kubadili chochote kutokea hapo.

Nimejitahidi mara kadhaa kutaka kujua iwapo kuna sababu nyingine ya sababu hiyo lakin mara zote mwenzangu amekuwa akijikita katika sababu tajwa hapo juu. Hata ninapomuuliza mwenzangu juu ya nini kinachoendelea mpka wakati huu bado hanipi majibu. Kimsingi, inaonekana hakuna mahusiano tena kwa sasa.

Ninaumia kwa namna mambo yalivyoenda na yalivyohitimishwa kwa namna isiyotarajika. ona ni kama ndoto, labda nipo ndotoni lakini ni ukweli ambao watu wanapitia. Nipo katika wakati mgumu mno, ukizingatia kwamba taarifa za jambo hili ziliwaslishwa kwa ndugu, jamaa na marafiki.

Nimekuja kwenu naomba ushauri, nahitajika kufanya nini ili niweze kuchukuliana na changamoto hii? Kuna wakati nashindwa kama binadamu naogopa kumfuru Mungu wangu. Nashindwa kusahau na namkumbuka sana kila wakati.
Pole sana labda haikupangwa awe mmeo
 
Dunia ni uwanja wa vita
  • Inawezekana, yeye amekuacha kwa ridhaa yake mwenyewe
  • Au ndugu zake wamemshauri aachane na wewe
  • Au ndugu zako wamekufanyia fitina, iwe ya maneno au kiimani
 
Refreshing
Sing haleluyah while closing your eyes
Muombe Mungu sana ndoa hailazimishi pengine Mungu anakuepusha na mengi

Ila maumivu [emoji848]
 
Inawezekana picha ulizopiga za uchi ukiwa chuoni Kuna ndugu aliziona akamuonyesha mtarajiwa wako.
 
Me nakushauri ktk yote USIJARIBU KUJIDHURU au KUDHURU, maisha ndio haya haya, wakat mwingine amini Mungu anakusudi kwa kila jambo linalotokea maishani mwako, liwe baya au zuri... Jikaze ishi maisha yako ya kawaida jipe furaha na amani, ukiwaza sana utakufa kwa presha na ugonjwa moyo...

WANAWAKE ambao hamjaolewa naomba niwaambie jambo, mwanaume akikuambia sasa siku fulani nataka nije kwenu kujitambulisha na kutoa mahali, jitahid sana kuwa mtulivu vuta hata wiki mbili au mwezi upime na uchunguze kama kweli anamaanisha (then mdanganye mwambie ushawajurisha ndug zako)
Baada ya hizo wiki 2 au mwez kupita, wajurishe wazaz/walez wako tu tena waambie wafanye siri, hakikisha ndug wengine wa muhimu unawaambia siku zikiwa zimebak chache hata kama ni siku 3 au 5 kabla ya tukio. Kwasabab wao hawana ulazima wakujurishwa mapema... Marafiki ndio hawafai kabisa ni bora uwaambie siku ya tukio au kutowaambia kabisa...
SIJUI KAMA NAELEWEKA, ni hivi mara nyingi sana hali ya migogoro hujitokeza baada ya wapendanao kuamua kuhalalisha mahusiano yao mbele ya wazaz na jamii, kwa njia ya mahali na kufunga ndoa. Huu ndio wakat shetan hutumia watu wengine kuharibu mahusiano hayo kwa njia ya kupenyeza maneno mabaya, uchawi na hila nyinginezo...
Ukitaka kujua hilo uliza watu walio ktk ndoa ktk watu 10 basi 5 watakuambia changamoto walizokutana nazo hadi kutamani kuacha zoez la mahali au ndoa...
Mimi nakumbuka nilijikuta tu siku za kutoa mahali zinakaribia ila sina morali yakwenda kutoa mahali na nitamani kuhairisha bila sababu ya msingi, Mungu ni mwema nilifanikisha...
Wanawake mtambue nyie mpo ktk risk kubwa sana ya kuharibiwa kisaikolojia kwa matukio kama hayo. Mwanaume ukimwambia umeghairi kupokea mahali yake siku 3 kabla ya tukio, usishangae the same day anatoa mahali kwa mtu mwingine, the moment mwanaume anakutambulisha kwao basi ujue kuna wanawake wengine wawili au watatu amewatambulisha na wote anaona wanafaa kuwa mke...
 
Back
Top Bottom