Me nakushauri ktk yote USIJARIBU KUJIDHURU au KUDHURU, maisha ndio haya haya, wakat mwingine amini Mungu anakusudi kwa kila jambo linalotokea maishani mwako, liwe baya au zuri... Jikaze ishi maisha yako ya kawaida jipe furaha na amani, ukiwaza sana utakufa kwa presha na ugonjwa moyo...
WANAWAKE ambao hamjaolewa naomba niwaambie jambo, mwanaume akikuambia sasa siku fulani nataka nije kwenu kujitambulisha na kutoa mahali, jitahid sana kuwa mtulivu vuta hata wiki mbili au mwezi upime na uchunguze kama kweli anamaanisha (then mdanganye mwambie ushawajurisha ndug zako)
Baada ya hizo wiki 2 au mwez kupita, wajurishe wazaz/walez wako tu tena waambie wafanye siri, hakikisha ndug wengine wa muhimu unawaambia siku zikiwa zimebak chache hata kama ni siku 3 au 5 kabla ya tukio. Kwasabab wao hawana ulazima wakujurishwa mapema... Marafiki ndio hawafai kabisa ni bora uwaambie siku ya tukio au kutowaambia kabisa...
SIJUI KAMA NAELEWEKA, ni hivi mara nyingi sana hali ya migogoro hujitokeza baada ya wapendanao kuamua kuhalalisha mahusiano yao mbele ya wazaz na jamii, kwa njia ya mahali na kufunga ndoa. Huu ndio wakat shetan hutumia watu wengine kuharibu mahusiano hayo kwa njia ya kupenyeza maneno mabaya, uchawi na hila nyinginezo...
Ukitaka kujua hilo uliza watu walio ktk ndoa ktk watu 10 basi 5 watakuambia changamoto walizokutana nazo hadi kutamani kuacha zoez la mahali au ndoa...
Mimi nakumbuka nilijikuta tu siku za kutoa mahali zinakaribia ila sina morali yakwenda kutoa mahali na nitamani kuhairisha bila sababu ya msingi, Mungu ni mwema nilifanikisha...
Wanawake mtambue nyie mpo ktk risk kubwa sana ya kuharibiwa kisaikolojia kwa matukio kama hayo. Mwanaume ukimwambia umeghairi kupokea mahali yake siku 3 kabla ya tukio, usishangae the same day anatoa mahali kwa mtu mwingine, the moment mwanaume anakutambulisha kwao basi ujue kuna wanawake wengine wawili au watatu amewatambulisha na wote anaona wanafaa kuwa mke...