Amegundua vidonge vya ARV's chumbani kwa mpenzi wake

Amegundua vidonge vya ARV's chumbani kwa mpenzi wake

Nimechanganyikiwa ngoja nitoke, Mungu akipenda nitarudi usiku nikiwa na kitu cha kuchangia.
 
Mleta threat utakua ww ndio muhusika bt unaona noma kuweka waz hapa, anyway we kapime tu ujue kama umeukwaa au vp, na kama ukikuta upo safi huyo dada haina haja hata ya kumsalimia we mpotezee mazima! Last pole sana hayo ndio maisha inabidi ukubali tu matokeo.
 
Khah ! kumbe muhusika mwenyewe ni WEWE ????
Nadhani alimalizia kwa kuandika, 'huzuni yake ni yangu pia.' Lakini hata kama ni yeye muathirika, ushauri utabaki uleule, na jambo zuri zaidi; huu si wakati wa kulaumu au kunyosheana vidole. Hatutamsaidia mlengwa.
 
Kupima hata mahospitali ya binafsi yanapima....................ila kwa kutoa ushauri wengine hawana hata muda......utafikiri anakuambia ukapime malaria................nimemshakumbana nao kama mara mbili...................sipendi kuzitaja hizo hospitali.

Yaani unamwambia docta,mimi ningependa kupima na vvu..............anakuuliza tu "umewahi kupima".......unamjibu hapana......anauliza tena "kwanini unataka kupima" ....unajibu nataka kujua afya yangu.............anakwambi, "ok....nimekuandikia tayari.....watakupima"!.................hivi hapo kakushauri nini?

Mimi nilimaanisha apate ushauri nasaha ambao utamuweka sawa ndio akapime..............mara nyingi AMREF wako makini na wanawashauri nasaha wazuri sana.
Akikurupuka na kwenda private hospital, sitanii....tunaweza kumpoteza iwapo atajikuta ameathirika kwani atakuwa ameongeza stress.
Mkuu umenikumbusha mbali!
Hata mimi niliwahi kwenda kupima ktk hizi hospital za binafsi,yaani hawana ushauri kabisa.Kilichonisaidia ni kuwa nilikuwa najiamini kuwa sina ila nilikwenda tu kama formality kwa ajili ya uthibitisho somewhere.Nilichotaka kusisitiza ni kuwa huyu jamaa ajaribu kumshauri mwenzake waende AMREF au ANGAZA au hospitali za kiserikali atapata ushauri mzuri sana.
Muweke karibu sana katika kipindi hiki kigumu.
 
Mkuu umenikumbusha mbali!Hata mimi niliwahi kwenda kupima ktk hizi hospital za binafsi,yaani hawana ushauri kabisa.Kilichonisaidia ni kuwa nilikuwa najiamini kuwa sina ila nilikwenda tu kama formality kwa ajili ya uthibitisho somewhere.Nilichotaka kusisitiza ni kuwa huyu jamaa ajaribu kumshauri mwenzake waende AMREF au ANGAZA au hospitali za kiserikali atapata ushauri mzuri sana.Muweke karibu sana katika kipindi hiki kigumu.
Huduma za kupima VVU hutolewa bure. Na ushauri nasaha pia. Sasa hospitali tajwa zina staff wachache, na haitakuwa haki kutaka mshauri nasaha ambaye mara nyingi ni nesi, kumwambia atumie angalau dakika 30 kwa ajili ya mtu mmoja anayetaka kupima VVU wakati kuna kazi nyingine kibao za kuhudumia mafuriko ya wagonjwa. Kama huduma hii ingetolewa kwa gharama fulani, yamkini hizi hospitali zingeweza kuajiri watu maalumu kwa huduma hii. Hao ANGAZA and the likes, wanapata misaada mikubwa sana ya upande tu wa kupima HIV, na hivyo wanastahili kutoa huduma nzuri ya ushauri nasaha; labda nenda pale ANGAZA na kidonda halafu ona kama utapata huduma (hata huduma ya kwanza tu)kama utakazopata hospitali zinazolalamikiwa.
 
Mimi naona jamaa kwanza akapime yeye mwenyewe.Akijua hali yake aje na kwa mpenzi wake akapime. Itasaidia jamaa yako kuchua maamuzi sahihi kuliko kubaki anachanganyikiwa.Ukimwi sio mwisho wa maisha.Mimi kuna mtu namjua tangu 1984 na yuko kijijini bado anaishi mpaka leo.Je mtu kama huyo anafanya kazi na anaweza kula chochote atakacho asiogope kupima.....
 
Nadhani alimalizia kwa kuandika, 'huzuni yake ni yangu pia.' Lakini hata kama ni yeye muathirika, ushauri utabaki uleule, na jambo zuri zaidi; huu si wakati wa kulaumu au kunyosheana vidole. Hatutamsaidia mlengwa.
I Guess you are an extra ordinary Genius....we kipaji!u alwayz dance according to the tune.Thanx for speaking my Language
 
Mleta threat utakua ww ndio muhusika bt unaona noma kuweka waz hapa, anyway we kapime tu ujue kama umeukwaa au vp, na kama ukikuta upo safi huyo dada haina haja hata ya kumsalimia we mpotezee mazima! Last pole sana hayo ndio maisha inabidi ukubali tu matokeo.
Siwez kuona aibu,sijalelewa kuona aibu ktk kuliiza Mambo yanayonijenga!inaniuma sbb n rafiki yangu wa kweli...au nikudokeze tu!Jamaa ni zaid ya rafiki!ata baada ya kumalza chuo alitangulia kpata kazi..mi nlchelewa sana!alinsaidia..akanbeba mpaka tukainuka wote!NAYAONJA MAUMIVU YAKE
 
Dah ndugu, poleni sana. Kumbe ndo maana network imekuwa taabu sana hizi siku za karibuni!!...lol
Ozzie kamaliza kila kitu hapo juu, fuata tu ushauri. Na kwa wengine ambao hamjafikwa: MKOME KUCHOVYA CHOVYA NA KULAMBA LAMBA!!! Mnaona hadi tunakosa huduma zenu ambazo ni muhimu kwa jamii... Kwanza Mungu hapendi tabia hiyo, MKOME KABISA.
 
Dah ndugu, poleni sana. Kumbe ndo maana network imekuwa taabu sana hizi siku za karibuni!!...lolOzzie kamaliza kila kitu hapo juu, fuata tu ushauri. Na kwa wengine ambao hamjafikwa: MKOME KUCHOVYA CHOVYA NA KULAMBA LAMBA!!! Mnaona hadi tunakosa huduma zenu ambazo ni muhimu kwa jamii... Kwanza Mungu hapendi tabia hiyo, MKOME KABISA.
We Kiboko!
 
Tafiti zimeonesha kuwa risk ya kupata HIV kwa mwanaume kwa kila tendo la ndoa moja analofanya (nazungumzia insertive vaginal sex) na mwanamke mgonjwa wa VVU ni asilimia 0.03 hadi 0.09
Mkuu Ozzie, umeelimisha VIZURI SANA dhana ya Discodant na kiasi cha hatari ya maambukizi (RELATIVE RISK) kwa tendo bila kinga, naomba kuongezea kuwa hatari kubwa iko kwa kuingiliana kinyume na maumbile ambapo risk/uwezekano wa maambukizi kwa katika kila tendo bila kinga ni karibu mara 18 ya ngono kwa njia ya kawaida (heterosexual act), lakini tendo moja laweza tosha kupelekea 100% maambukizi kutokana na factors ulizozieleza kwa ufasaha hapo mwisho wa maelezo yako,
Hivyo huyo rafiki yake Ngariba anaweza akawa amepata au hajapata VVU, asitaharuki bali amshawishi waende wakapate ushauri nasaha na kupima VVU, mengine yatajipa baada ya hapo, baada ya kupima kama atabainika na VVU,asimlaumu huyo mdada kwani inawezekana yeye alikuwa na VVU hata kabla ya kuanza naye mahusiano kama alikuwa hajui status yake.
 
Mahali palipofikia kuelekea kwenye ndoa sidhani kinga ilitumika. Huyo dada kwa kukaa kimya tu kwa jambo zito kama hili ni wazi anajua chanzo.
Kwa hali ya sasa hivi hata kama mtu anahisi anaweza kuambukizwa ima kwa sindano, kupewa damu n.k kwa mwenye upendo wa dhati lazima amtaarifu mwenzi wake.

Mshauri rafiki yako achukue likizo kwasababu msongo wa mawazo unaweza kumfanya achukue hatua zisizotarajiwa hasa tukizingatia nguzo ndefu anazopanda kila siku. Mshauri asitafute mchawi kwanza bali atulize mawazo. Mwandae atarajie matokeo ya aina yoyote na awe tayari kuyakabili. Aende kupima na kuwe na mpango wa kupata ushauri nasaha kwa wataalamu endapo itatokea vinginevyo.

Hali ikishatulia na kukubalika amuulize mpenzi wake kwani kosa la kufungua mkoba halina ulinganifu na hali iliyopo hata kidogo. Njia bora ni kuelezana ukweli na kuwa tayari kukabiliana na ukweli huo kwa pamoja.

Hili neno tuna aminiana lisikubalike miongoni mwa watu hata kidogo. Mnapoamua kwenda kwa Sheikh au madhabahuni hapo ndipo kuaminiana kuna ingia kwasababu mumekubaliana kwa dhati zenu na likitokea lingine hilo limo ndani ya uaminifu wenu wa ukweli au uongo.
 
Back
Top Bottom