Amekasirika. Kisa...nimemuuliza "wataondoka lini"


Mkuu wengi wetu hatuna ujasiri huo na ndio maana tunajikuta tunaumia ndani kwa ndani. Kimsingi huu woga na kundekeza yasiyotakiwa kuendekezwa nidko kunakotuzamisha kwenye dimbwi la umaskini!
 

Mimi nadhani wewe ndiyo mwenye matatizo, kuna ulazima gani kumlipia mtua nauli anapokuja kukutembelea?
 
Pole kwa stress, shida ya hawa wenzetu ni kutumia hisia kwa kila jambo, wageni wakiondoka mweke chini umweleze kwa undani kwamba familia inatakiwa kuwa na mipango na ulivyomwuliza ilikuwa ni namna mojawapo wa kujipanga.
 
Nadhani kunatatizo zaidi ya kuulizwa swali! Yawezekana hata yeye mwenyewe hajui tatizo nini! Kaa naye chini muongee vizuri! hizi hadithi za kutegesheana sio nzuri ama kusubiri baadaye sio nzuri! Kwa kuwa yeye ndio mwenye hasira muulize "mke wangu kwanini unadhani siwapendi ndugu zako". Mwache afunguke! akinuna mletee mama yake zawadi ya khanga! upendo unalainisha hasira! halafu wazazi wake wakiondoka huko baadaye kama kuna umuhimu! mtaongea tena!
 
Sasa wewe si ungemueleza lengo lako la kuuliza vile, ili akuelewe!
 

duu hilo wazo ni zaidi ya ufikiriavyo hasa kwa mitz
 
Ndoa yako iangalie kwa jicho la pili kiukweli mkeo ulimuonesha unampenda sana na umeoza kwake hayo ndio malipo yake hebu kuwa na mcmamo si kama anawapenda jamaa zake mpaka kufikia hatua hiyo anatikisa kibiriti
 
Inawezekana ulianza vibaya wakati wa kuuliza, maana unaweza ukakurupuka na kuuliza 'hawa wageni wanaondoka lini' tena kwa sauti ya juu na ukali. Huyo ni mkewe inabidi uongee naye kwa utulivu, utaratibu na upendo ukimkumbusha majukumu yanawakabili likiwepo hilo la kuwapatia nauli wageni wenu, baada ya hapo ukitaka kujua wageni wataondoka lini utafahamishwa bila shaka!
 
Unaendekeza mambo ambayo si matatizo kuyafanya yawe matatizo.

1. Mtu uko kwako (au si kwako?)

2.Umekarimu watu kwa kuwakaribisha , jambo zuri.

3. Apparently unawapa nauli pia , jambo ambalo linapita uzuri na linaweza kuwa baya kwa sababu una wa "enable" depending hawa ni watu wzima au watoto? Wana uwezo wa kufanya kazi au hawana? Kwa nini uwape nauli?

4. Halafu inaonekana hata wewe mwenyewe mambo yako si fresh kihivyo, ukiombwa nauli kwa kushtukizwa unaenda kukopa. Haya mambo ya "keeping up appearances" na "upendo wa mshumaa" si mazuri. Waambie tu kwamba "sina" na kama una nia ya kuwasaidia zaidiwasaidie kujua kwamba hela si maji kwamba utaenda kuchota tu kwenye bomba, hata hayo maji watu wanayapigia hesabu na kuyapangia kazi.

5.Wasaidie zaidi kwa kumueleza hata mkeo kwamba ratiba ni kitu cha kawaida katika maisha.
 
Anatingisha kiberiti aone kama kina njiti za kutosha.
 

Aseeee!!!!!!.
 

Point nzuri sana hii.
 
mwambie mkeo mjini mipango, kuendekeza ndugu mtakufa masikini.

Kwani akinuna unapungua uzito? Mwache anune ataongea tu!
 

Mkuu umeeleza vizuri sana.
Lakini nilishafafanua huko nyuma kuwa kwa familia zetu na utamaduni wa makabila mengi ya kitanzania....ni vigumu sana kusema ukweli hasa katika masuala kama hayo....tunakwepa kuonekana "wabaguzi". Na hapo ndipo maumivu yanapokuja.
 
Mkuu wengi wetu hatuna ujasiri huo na ndio maana tunajikuta tunaumia ndani kwa ndani. Kimsingi huu woga na kundekeza yasiyotakiwa kuendekezwa nidko kunakotuzamisha kwenye dimbwi la umaskini!

Kwa malezi ambayo wengi tumelelewa huku tukijikita katika kile ambacho tunadhani ni upendo ni ngumu sana kwa kweli.

Mfano mdogo tu.
Ukiwa "mkomunisti" labda hutoitoi ofa za bia kwa marafiki na majirani japo wewe unakunywa kila siku, watakuita mchoyo. Kuogopa hilo wengi wanajikuta katika upendo unaozidi uwezo wao.
 
Jinsi ushauri ulivyo mwingi! Nahisi utajichanganya,kwani tamaduni za maisha ya kinyumba ziko tofauti sana tanzania hii, sie kwetu, mara nyingi wageni wa kuja kutembea tu hakuna, labda siku mbili tatu, kama wakija ni wanafunzi likizo, lazima uwe na control na watoto, kama ni wazazi au ndugu watakuwa na issue unayoijua na wataondoka itakapoisha. Nikikushauri kuwa ni lazima ujue, sijui kwenu inaruhusiwa? Usijekususwa, ukaanza shida zingine zisizo na solution
 
Pole sana jaribu kumuelewesha tuu huwa wanaelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…