Amekasirika mume wake anataka kuoa mke mwingine

Khaaaa hii ndo sababu hatuchangii pato la familia! Yaani fedha tulizochuma wawili tulipokubaliana ndoa y mke mmoja halafu mara tamaa imuwake mwanaume eti anaoa mke mwingine na anamnunulia nyumba!
Hapo tutauana!
 
Kwani bi mkubwa ana shughuli yoyote ya kumuingizia kipato? Au na yeye alikua anadaka magoli tu bila yeye kufunga pia?
 
wacha aoe tuu.....ndoa ni maisha....na maisha ni kujipanga ili uyafurahie, so ukiona furaha uliyonayo haikidhi au stress kibao,,, unadabo direction....hata kama ni mkristo aoe tuu.....ni maisha yake....
 
Mkristo anaoa mke wa pili??

ni mkristo jina mkuu mara ya mwisho kwenda kanisani ni 2005
Huyo aliesema wakristo wasio mke zaidi ya mmoja Sio Mungu, Mungu wakweli anajuwa wanawake ni wngi zaidi ya wanaume atawekaje sheria ya aina hiyo.Hizo ndio baadhi za kazi za binadamu ndani ya Bible. Wakrsto wengi wameshapuuza hilo haliendani na ukamilifu wa Mungu.
 
Hata Shetani aweza kutunga kitabu akakiita kitabu kitukufu! Na kuweka sheria zake ili kutoa fursa za uzinzi!
Mungu wa kweli aliumba Adam na mwanamke mmoja ambaye ni Eve!
 
Nimelipenda hili jibu....ubarikiwe.
 
Khaaaa hii ndo sababu hatuchangii pato la familia! Yaani fedha tulizochuma wawili tulipokubaliana ndoa y mke mmoja halafu mara tamaa imuwake mwanaume eti anaoa mke mwingine na anamnunulia nyumba!
Hapo tutauana!

Nyumba alishanunua, yaani mimi hili jambo limenikera sana, na hata sisi wanawake sijui tukoje yaani unakubali kabisa kwenda kuharibu amani ya mwenzio, kama angekuwa wa kuolewa si angaolewa na vijana wabichi wenye nguvu zao, yaani wanaume nao wanatia aibu sana nguvu za kiume zenyewe mbili bado wanafanya vitu vya ajabu. mtu mmestruggle juani pamoja kivulini anaketi na mwingine khaaa!!! sina ham nao hawa watu.
 
Huyo aliesema wakristo wasio mke zaidi ya mmoja Sio Mungu, Mungu wakweli anajuwa wanawake ni wngi zaidi ya wanaume atawekaje sheria ya aina hiyo.Hizo ndio baadhi za kazi za binadamu ndani ya Bible. Wakrsto wengi wameshapuuza hilo haliendani na ukamilifu wa Mungu.

Imani ya kikristo popote ulimwenguni inatambua mke mmoja, suala la ndoa ni makubaliano tu. kunandoa za kipagani, kiislam, kikristo, kiserikali n.k kwa hiyo ni uhuru wa mtu kuamua ila ukristo ni mke mmoja,
Hata kama wanawake ni wangi kuliko wanaume isiwe fursa ya watu kufanya uzinzi. kilichopo mioyoni mwa watu ni uzinzi tu hizi nyingine ni sababu za kujifichia uzinzi. Hivi vitu lazima viendane na ulimwengu tuliopo, dunia hii magonjwa kibao bado watu hawaogopi tu. Wanaume wenyewe kila siku mnahangaika kwa madaktari mmebakiwa na nguvu mbili za kiume leo mtu anaenda kuoa wake wawili, huyo mmoja wa ndani kwa mwezi mara moja sasa wawili si ndio kutafuta kusaidiwa mwisho wake kupata magonjwa.
 
Vizuri kabisa, mke hapaswi kukasirika kamwe, anapaswa kumpongeza mumewe....
 
Hakuna mkristo anayeruhusiwa kuoa mke zaidi ya mmoja...mila na desturi zingine inabidi ziangaliwe mara mbili mbili jaman...mwshowe huyo mkewe afe kwa presha bure
Bongo hii wakristu ni wachache sana. Hawafiki 2% ya population. Waliobaki ni wakristu majina. Kwa maana hawafuati na kuishi kwa misingi na mafundisho ya kikristo
 
Huyo aliesema wakristo wasio mke zaidi ya mmoja Sio Mungu, Mungu wakweli anajuwa wanawake ni wngi zaidi ya wanaume atawekaje sheria ya aina hiyo.Hizo ndio baadhi za kazi za binadamu ndani ya Bible. Wakrsto wengi wameshapuuza hilo haliendani na ukamilifu wa Mungu.

Biblia iliandikwa kwa ajili ya wagalatia.Hivi umewahi kuona waraka wa mtakatifu Paulo kwa Wakurya? Au wasukuma? Au wanyakyusa?
 
Nyumba alishanunua, yaani mimi hili jambo limenikera sana, na hata sisi wanawake sijui tukoje yaani unakubali kabisa kwenda kuharibu amani ya mwenzio, kama angekuwa wa kuolewa si angaolewa na vijana wabichi wenye nguvu zao, yaani wanaume nao wanatia aibu sana nguvu za kiume zenyewe mbili bado wanafanya vitu vya ajabu. mtu mmestruggle juani pamoja kivulini anaketi na mwingine khaaa!!! sina ham nao hawa watu.

Kama ndio mimi muhanga wa kuolewa mke wa pili??? weee pangechimbika bila jembe wala koleo...!!! :banghead:
 
Bongo hii wakristu ni wachache sana. Hawafiki 2% ya population. Waliobaki ni wakristu majina. Kwa maana hawafuati na kuishi kwa misingi na mafundisho ya kikristo

Kwahiyo imind wewe unaafiki kabisa jamaa asogeze mzigo wa pili?? sikutegemea kabisa 🙁
 
Huyo aliesema wakristo wasio mke zaidi ya mmoja Sio Mungu, Mungu wakweli anajuwa wanawake ni wngi zaidi ya wanaume atawekaje sheria ya aina hiyo.Hizo ndio baadhi za kazi za binadamu ndani ya Bible. Wakrsto wengi wameshapuuza hilo haliendani na ukamilifu wa Mungu.

Si kweli wanawake wanaonekana wengi kwa kuwa tu wanahesabiwa wote mpk wazee sasa hii group ya 60yrs and above wengi ni wajane so msiwatishe wanawake kuwa ni wrngi unless kama mnataka kuoa nyanya zenu wa 80yrs lakini vijana mnatosheana vizuri tu
 
Iwe dini au mila...
kama kuoa wake wengi aoe asubuhi.
Tunaanza tuanze wake wote hatua kwa hatua.
Sio leo tunakaa chumba kimoja uone mie ndio wife material
Tumejibana na kujinyima tukapata kisehemu unisifie. Kesho ukiongeza cha ziada uone sikutoshi eti "uchumi unaruhusu" mfyuuu.
kama sijakukata hicho kiume.
Huo uchumi mbona haukuruhusu kwangu ila ulinioa? Ungetuoa wote na njaa yako.
 
Back
Top Bottom