Melki Wamatukio
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 6,156
- 10,974
Alimtafutia kazi huyu binti wa dada yake. Baada ya miezi mitano tokea kuanza kazi, binti akapata mwamba, akaanza tabia ya kutoroka saa 10 jioni kumpelekea Mwamba Utelezi. Boss ndipo kushtuka, akaamua kumfukuza kazi. Binti ndipo kukimbilia kwa mshkaji ili waishi kama Baba na Mama
Taarifa ndipo kuwafikia ndugu na jamaa, ukoo wa binti ndipo kumuulizia mwenyeji wa binti kama ana taarifa za binti kutokomea kusikojulikana baada ya kufukuzwa kazi. Katika harakati za kutafuta, ndipo kugundua kuwa anaishi na Mwamba maeneo ambayo si mbali na kwa aliyekuwa boss wake
Wajomba akiwemo mmojawao mfupi hivi aliyevalia koti la blue na suruali nyeusi bila kusahau kofia la kikongo ndipo kuja mjini kutoka huko Nanjilinji kwa ajili ya utaratibu wa ndoa, kijana wa watu akabambikwa laki saba. Kwa uzuri gani alionao, Mola anisamehe tu. Kijana wa watu ni msukuma, akaamua kujichanga 300k akawakabidhi na kuahidi kuwa pesa iliyobaki atamalizia mwezi August. Ndugu wakajaa sumu wakasema mtoto wao hajawa bidhaa kusema anaenda kwa mkopo. Kijana kwa majonzi mazito akaamua kuachia dimba😭
Basi bhana, ndugu wakachangishana nauli, wakarudi Nanjilinji. Mwenyeji wa binti ambaye pia ni ndugu yake (Yule mwanamke aliyemtafutia kazi) akabaki na Binti. Kwa kuwa mahali alipokuwa anakaa ni chumba kimoja, hicho hicho anaishi yeye na mumewe, ikabidi amuombee hifadhi kwa rafiki yake ambaye ni jirani yangu ambaye anakaa umbali sawa na kutoka Kimara Baruti kuja Argentina (Dsm) ama Kona ya Bwiru hadi Mkuyuni (Mwz)
Maisha ya binti na jirani huyu kwa mwanzo yalikuwa ni mazuri tu mpaka pale jirani alipopata za chini chini kuwa kipindi cha nyuma huyo rafiki yake mwenye binti alikuwa akimnafikia sana hasa hasa kwenye haya masuala ya mikopo ya kina mama na vikoba. Baada ya kulifahamu hilo hali ya hewa ikabadilika
Alternative iliyobaki ni kumchukua binti, apelekewe yule Msukuma ingawa ndugu hawataki, kila mmoja kamuwekea cha udalali hadi yule Athumani Makoti. Hapa alipo ili apone na njaa anadiliki kukisambaza mtaani japo kwa siri na ninavyomuona ni kama vile kashika ujauzito. Je, msukuma atakapoligundua hili atakubali kulea? Ama awaishiwe mzigo kabla halijasanuka!
Aisee, hii mila ya mahari serikali iingilie kati kwa kweli