Amepima akakuta ana damu nyingi. Njia ipi ni rahisi ku-level damu?

Amepima akakuta ana damu nyingi. Njia ipi ni rahisi ku-level damu?

Mimi nina 19. Nimeambiwa nisitoe itakuwa inaongezeka sana. Nipunguze mboga za majani na vyanzo vyote sababishi kuongezeka damu. Ila napata kizunguzungu sana na kichhwa kuuma

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Ninalo hilo tatizo msaada nifanyeje

Habari!

Jambo hili si suala la namba tu, bali linahitaji uhusishwaji wa vitu muhimu kabla ya kufikia hutimisho:

1: Reference range ya mashine husika (kiasi cha wastani wa kawaida kwa mpimwaji kulingana na mashine iliyohusika).

2: Jinsia ya mhusika

3: Umri (hasa kwa watoto)

4: Umbali toka usawa wa bahari( mtu anaeishi sehemu ya milima kama Iringa, Kilimanjaro, Lushoto nk. si sawa na anaeishi Dar-es-salaam).

Baada ya kuzingatia hayo, ni kazi ya daktari bingwa wa magonjwa ya damu kutafuta chanzo na kupata jawabu halisi la tatizo.

Kuna hali ambazo kuongezeka kwa kiasi cha damu jibu si kutoa damu bali tiba yake mwafaka.

Hivyo, ni vyema kuwahusisha wataalamu husika katika hili kama ni kweli na upate utatuzi timilivu.
 
Wakuu msaada kwa ilo ni njia ipi rahis ya kupunguza wingi wa damu ukiacha ile ya kuchangia damu.

Jinsia yake ni Ke,
Mimi nina 18.1, daktari akanishauri nisitoe maana nakuwa kama naipalilia na itabidi kila mwezi nikatoe, Ila inanisumbua balaa, kuna wakati nikiinama naona giza
Damu inaongezekaje, inazidi vipi?

Inazidi kulingana na kipimo, ila kulingana na mwili wako (subconsciously) hiyo ndio damu sahihi kwako!

Mwili sio jinga tu eti izidishe kiwango cha damu, hata siku moja. Kwake hicho ndicho akili yako consciously imeamua ndiyo hali halisi.
Ipo hivii;
Tangu na tangu, jamii zilipojiandaa na vita au mapambano zilitegemea kupoteza damu.

Miili ikajiboresha na kuwa inajiandaa kwa kuongeza wingi wa damu ikisikia tu kwamba kuna mapambano yanafuatia au yanaendelea.

Ni kama tu mwili unavyochemka kabla ya ngono hata kama bado hamjaanza kunjunjana.

So wenye tatizo la damu kuwa nyingi, jitueni mizigo mnayohisi mmebeba, malizeni mapambano mnayohisi mnapaswa kuyapigana. Hii ndio nadharia inayofanya kazi kwa upande wangu. Aipate pia Xmonster pamoja na mtani21
 
Back
Top Bottom