Amestaafu na kupewa shilingi milioni mia moja. Anaomba msaada

Yeye anataka laki saba kila mwezi. Hizo hati fungani zitamuingizia hicho kiasi kwa mwezi?
Kwenye benki hawezi kupata laki saba faida kwa mwezi , kwenye hati fungani yes inawezekana - zunguka kwenye mabenki kuna wahudumu watakupa elimu hii na namna ya kuzigawanya hizo hela zako kwa mikupuo.
 
Akawekeze kwenye hisa ndio itamlipa zaidi
 
Yeye anataka laki saba kila mwezi. Hizo hati fungani zitamuingizia hicho kiasi kwa mwezi?
Anipe mim hapa nifanye mafekeche ktk biashara ya viatu vya mtumba kila mwez atapata lak saba na akitaka pesa yake atatoa taarifa nitamkabidh baada ya miez sita tangu atoe taarifa
 
Mpe hongera inaelekea alikua na kamshahara c haba. Mwambie aende nmb wana huduma ya kuweka fixed deposit kwa wastaafu wanatoa interest 7.5% kuanzia milion 10 mpaka 30.

Na 8% kuanzia 31m mpaka 50m na kuanzia 51 m nayo pia kuna rate yake kwa muda wa miaka 2 maxmum. Na kila mwezi unapata faida kutnka kwenye calc ambayo watakufanyia mfano mm kuna mtu ameweka kama zaid ya m 50 na kila mwezi anapata faida ya zaidi tsh. Laki 3.

Ukichangamya na sehdemu ingne aliyowekeza fedha ingme anapata kama laki 2 na pension ya kila mwez anapata kama m 1.2 hzo ni faida tu ila fedha yake ipo pale pale. After 2 years anaweza kuwerenuew tena.

Huo ni mfano halisi nenda nmb watakupa maelezo. Kaz njema.
 
Aende aangalie kila bank fixed deposit interest inasomaje.vinginevyo asifanye biashara yoyote kwa sasa kwa sababu atakufa ndani ya muda mfupi
 
Huyu mama ndio mfano halisi wa wazazi wa kiAfrica yani unataka kufungia 80M as if hauna ndugu na jamaa wanashida husikute ata watoto bado wanaitaji boost kwenye maisha yao. Nimeshindwa kuelewa uelewa wa wazee wetu wa kiAfrica yani huu ubinafsi ndio unaturudisha nyuma sana.

Sent from my 601SO using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…