Amini, Usiamini. Nimepona Magonjwa 100+ Kwa Jina la Yesu!

Jibu swali badala ya stori mwanangu. Kwanini hawa matapeli wanaojifanya kuponya na kufanya miujiza hawaombei viwete na wagonjwa mahututi wakapona?
Mbona umeishajijibu swali lako? Matapeli ni matapeli, ni wazi hawawezi kuombea viwete wakapona. Jifunze habari za Yesu uone jinsi alivyoponya viwete, vipofu na kufufua wafu, kisha jifunze jinsi Petro, Paulo walivyotenda miujiza mikubwa kwa Jina la Yesu.
 
Yesu sio Mungu

YOHANA 12:49

Mimi sikunena kwa mamlaka yangu mwenyewe,ila Baba aliyenituma ndiye aliyeniamuru niseme nini na niongee nini

Hivi Mungu anaweza kupewa amri?
Unasoma mstari mmoja tu unaishia hapo
 
Magonjwa yalikuwa yake, kapona yeye, nyie mnataka kujua nini, mwacheni aendelee kutupa story.

Mnaamini Mwarobaini unatibu magonjwa 40, lakini hamtaki yeye kuponywa magonjwa 100 tu na Yesu?
Waambie kwa HERUFI KUBWA labda watakuelewa. Mtu hata akisema kwa Jina la Yesu, amepona ugonjwa mmoja tu(eg kisukari) bado watamuita tapeli
 
Unasoma mstari mmoja tu unaishia hapo
Endeleza wewe ili usomeke,

Nakuongezea na hii,

YOHANA:5:36

Mimi siwezi kufanya kitu kwa uwezo wangu mwenyewe,mimi nina hukumu kama ninavyosikia kutoka kwa Baba,nayo hukumu yangu ni ya haki,nia yangu si kufanya nipendavyo mwenyewe,bali apendavyo aliyenituma.
 
Ahsante sana kwa ushuhuda mzuri, Mungu anaponya sana ni imani yako na kujinyenyekesha. Binafsi nimefurahi kwa ushuhuda mzuri unaoelezea matendo ya Mungu aliyehai. Ubarikiwe sana na Mungu aendelee kujidhihjrisha kwako ili uje utushuhudie ukuu wake. Ahsante sana Mtumishi
 
Kuandika na kuelewa unachoandika ni vitu viwili tofauti. Jiulize kwanza Yesu alizaliwaje? Aliwezaje kutembea juu ya maji, aliwezaje kupaa mbinguni kama sio Mungu?
 
Kabisa, mkuu
Yesu mwenyewe alikua akiomba msaada kwa Mungu,

MK 15:34 SUV
Na saa tisa Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu,
Eloi eloi lama sabakhtani,maana yake Mungu wangu mbona umeniacha?

Hapa alikua anamuomba Mungu yupi? au alikua anajiomba yeye mwenyewe?
 
Amen. Bwana Yesu asifiwe sana
 
Kuandika na kuelewa unachoandika ni vitu viwili tofauti. Jiulize kwanza Yesu alizaliwaje? Aliwezaje kutembea juu ya maji, aliwezaje kupaa mbinguni kama sio Mungu?
Wewe ni mjinga na ujinga wako upo wazi kabisa,acha kukwepa hoja zangu kwa kuleta issue zingine sijui za kupaa au kutembea juu ya maji,
Jibu swali nililokuuliza kwa kuleta maandiko/Aya,
acha kuleta story tu.
 
Yesu mwenyewe alikua akiomba msaada kwa Mungu,

MK 15:34 SUV
Na saa tisa Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu,
Eloi eloi lama sabakhtani,maana yake Mungu wangu mbona umeniacha?

Hapa alikua anamuomba Mungu yupi? au alikua anajiomba yeye mwenyewe?
Jiulize kama sio Mungu aliwezaje kufufuka
 
Wewe ni mjinga na ujinga wako upo wazi kabisa,acha kukwepa hoja zangu kwa kuleta issue zingine sijui za kupaa au kutembea juu ya maji,
Jibu swali nililokuuliza kwa kuleta maandiko/Aya,
acha kuleta story tu.
Wewe ni mwerevu lakini hujui hata Maandiko yanayoeleza wazi kuwa Yesu ni Mungu. Subiri, nikipata nafasi ntaweka uzi maalum wa mada hiyo. Kwa sasa tulia, usituhamishe nje ya lengo la uzi huu.
 
Wewe ni mwerevu lakini hujui hata Maandiko yanayoeleza wazi kuwa Yesu ni Mungu. Subiri, nikipata nafasi ntaweka uzi maalum wa mada hiyo. Kwa sasa tulia, usituhamishe nje ya lengo la uzi huu.
Huna unalolijua wewe,hujui chochote,nimekupa aya hujaweza kunijibu,
wahi Milembe ukatibiwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…