The Icebreaker
JF-Expert Member
- Feb 11, 2018
- 22,278
- 65,817
Bwana Mungu wangu ni nani?Usimjaribu Bwana Mungu wako
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bwana Mungu wangu ni nani?Usimjaribu Bwana Mungu wako
Kina nani hao waliomdhihaki na kumtusi?Hata Yesu walimdhihaki na kumtusi. Hivyo sishangai kauli yako
Yesu sio MunguYesu ni Mungu
Mbona umeishajijibu swali lako? Matapeli ni matapeli, ni wazi hawawezi kuombea viwete wakapona. Jifunze habari za Yesu uone jinsi alivyoponya viwete, vipofu na kufufua wafu, kisha jifunze jinsi Petro, Paulo walivyotenda miujiza mikubwa kwa Jina la Yesu.Jibu swali badala ya stori mwanangu. Kwanini hawa matapeli wanaojifanya kuponya na kufanya miujiza hawaombei viwete na wagonjwa mahututi wakapona?
Waambie kwa HERUFI KUBWA labda watakuelewa. Mtu hata akisema kwa Jina la Yesu, amepona ugonjwa mmoja tu(eg kisukari) bado watamuita tapeliMagonjwa yalikuwa yake, kapona yeye, nyie mnataka kujua nini, mwacheni aendelee kutupa story.
Mnaamini Mwarobaini unatibu magonjwa 40, lakini hamtaki yeye kuponywa magonjwa 100 tu na Yesu?
Endeleza wewe ili usomeke,Unasoma mstari mmoja tu unaishia hapo
Ahsante sana kwa ushuhuda mzuri, Mungu anaponya sana ni imani yako na kujinyenyekesha. Binafsi nimefurahi kwa ushuhuda mzuri unaoelezea matendo ya Mungu aliyehai. Ubarikiwe sana na Mungu aendelee kujidhihjrisha kwako ili uje utushuhudie ukuu wake. Ahsante sana MtumishiHuu ni ushuhuda wa kweli kabisa. Katika maisha yangu nimekuwa nikiugua magonjwa mengi ya aina mbalimbali. Kifuani, tumboni, miguuni, katika vidole, machoni, masikioni, puani, kichwani, nk, nk. Muda hautoshi kuyaeleza kwa kina. Kwa haraka haraka naweza kusema tangu ujana wangu nimeugua zaidi ya magonjwa 100. Namshukuru Mungu kwakuwa amekuwa akiniponya magonjwa kila yanaponiijia. Ninachokifanya, kila nikiumwa, namuomba Mungu aniponye kwa Jina la Yesu, kisha naweka mkono wangu juu ya sehemu inayoumwa na kuuamuru ugonjwa utoke kwa Jina la Yesu; kisha naamini kwamba imekuwa hivyo. Wakati mwingine inachukua muda kuona matokeo lakini wakati mwingine ugonjwa unatoweka saa hiyo hiyo. Maneno aliyosema Yesu ni kweli kabisa. Katika Mk 16:17-18 anasema: “Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu(Yesu) watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.”
Huu ni uthibitisho kuwa Mungu yupo na anatenda miujiza hata leo kwa watu wanaomuamini. Kwa ushuhuda huu sikuambii usiende hospitali. La, hasha! Ukiwa na pesa, nenda. Nenda hata hospitali za nje ya nchi. Hata mimi kuna wakati huwa naenda hospitali kwa kuwa najua kwamba Mungu anaweza pia kuponya kwa kuwatumia madaktari. Hata hivyo ninapoenda hospitali bado naweka matumaini yangu kwa Mungu kwakuwa najua madaktari nao kuna magonjwa yako juu ya uwezo wao au elimu yao; na wakati mwingine nadhani huwa wanajisahau, badala ya kutia moyo wanakatisha tamaa. Kuna siku nilipungukiwa damu, nikaenda kumuona Daktari. Aliponipima na kuhakikisha damu imepungua, akaniuliza: “Damu umepeleka wapi wewe?” Usipokuwa na matumaini kwa Mungu ukiulizwa swali hilo la kuvunja moyo unaweza ukaugua mara mbili zaidi. Na kwa magonjwa niliyougua, kama kila ugonjwa ningekuwa nakimbilia hospitali, ningehitajika kuwa milionea maana ningepaswa kulipa pesa nyingi za matibabu. Namshukuru Yesu anaponya bila kulipa hata senti. Nawasikitikia wanaosema eti Mungu hayupo. Wanakosa baraka hizi za uzima.
Hata hivyo kuna vigezo na masharti ya kuzingatia ili mtu aone kikamilifu uponyaji wa Mungu kwa Jina la Yesu. Baadhi ya vigezo vimeelezwa katika Andiko hili: Kutoka 15:26. “Mungu akasema, ‘Kama mtaisikiliza kwa bidii sauti yangu mimi BWANA Mungu wenu na kuyafanya yaliyo sawa mbele yangu, kama mtayatii maagizo yangu na kuzishika amri zangu zote, sitaleta juu yenu ugonjwa wowote niliowaletea Wamisri, kwa kuwa Mimi ndimi BWANA, niwaponyaye.’” Uponyaji wa Mungu ni wa bure kwa wote wanaozingatia maneno hayo. Ukisikia Mtumishi anakuambia ulipe pesa kwanza ndio akuombee, jihadhari naye. Yesu alipowapa mamlaka wanafunzi wake ya kukemea pepo na kuweka mikono juu ya wagonjwa ili wapone, aliwaambia amewapa bure, hivyo wanapaswa kutoa huduma hiyo bure(Mathayo 10:8).
Yamkini unaumwa, umetibiwa kila mahali hujapona. Usikate tamaa. Ushuhuda huu ukutie moyo kuwa unaweza kupona kwa uwezo wa Jina la Yesu Kristo. Yote yawezekana kwake aaminiye(Mk 9:23). Amen.
Kuandika na kuelewa unachoandika ni vitu viwili tofauti. Jiulize kwanza Yesu alizaliwaje? Aliwezaje kutembea juu ya maji, aliwezaje kupaa mbinguni kama sio Mungu?Endeleza wewe ili usomeke,
Nakuongezea na hii,
YOHANA:5:36
Mimi siwezi kufanya kitu kwa uwezo wangu mwenyewe,mimi nina hukumu kama ninavyosikia kutoka kwa Baba,nayo hukumu yangu ni ya haki,nia yangu si kufanya nipendavyo mwenyewe,bali apendavyo aliyenituma.
Yesu mwenyewe alikua akiomba msaada kwa Mungu,Kabisa, mkuu
Hebu orodhesha hayo magonjwa 100+ uliyopona, nitajie magonjwa 50 tuHata Yesu walimdhihaki na kumtusi. Hivyo sishangai kauli yako
Amen. Bwana Yesu asifiwe sanaAhsante sana kwa ushuhuda mzuri, Mungu anaponya sana ni imani yako na kujinyenyekesha. Binafsi nimefurahi kwa ushuhuda mzuri unaoelezea matendo ya Mungu aliyehai. Ubarikiwe sana na Mungu aendelee kujidhihjrisha kwako ili uje utushuhudie ukuu wake. Ahsante sana Mtumishi
Wewe ni mjinga na ujinga wako upo wazi kabisa,acha kukwepa hoja zangu kwa kuleta issue zingine sijui za kupaa au kutembea juu ya maji,Kuandika na kuelewa unachoandika ni vitu viwili tofauti. Jiulize kwanza Yesu alizaliwaje? Aliwezaje kutembea juu ya maji, aliwezaje kupaa mbinguni kama sio Mungu?
Jiulize kama sio Mungu aliwezaje kufufukaYesu mwenyewe alikua akiomba msaada kwa Mungu,
MK 15:34 SUV
Na saa tisa Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu,
Eloi eloi lama sabakhtani,maana yake Mungu wangu mbona umeniacha?
Hapa alikua anamuomba Mungu yupi? au alikua anajiomba yeye mwenyewe?
Jibu swali nililokuuliza,alikua anamuomba Mungu yupi?Jiulize kama sio Mungu aliwezaje kufufuka
Wewe ni mwerevu lakini hujui hata Maandiko yanayoeleza wazi kuwa Yesu ni Mungu. Subiri, nikipata nafasi ntaweka uzi maalum wa mada hiyo. Kwa sasa tulia, usituhamishe nje ya lengo la uzi huu.Wewe ni mjinga na ujinga wako upo wazi kabisa,acha kukwepa hoja zangu kwa kuleta issue zingine sijui za kupaa au kutembea juu ya maji,
Jibu swali nililokuuliza kwa kuleta maandiko/Aya,
acha kuleta story tu.
Huna unalolijua wewe,hujui chochote,nimekupa aya hujaweza kunijibu,Wewe ni mwerevu lakini hujui hata Maandiko yanayoeleza wazi kuwa Yesu ni Mungu. Subiri, nikipata nafasi ntaweka uzi maalum wa mada hiyo. Kwa sasa tulia, usituhamishe nje ya lengo la uzi huu.