Infropreneur
JF-Expert Member
- Aug 15, 2022
- 9,830
- 20,686
Huo ukristo wenu bakini nao huko makanisani mwenu, Mkileta hizo dini zenu hapa kwenye public forum tutazikosoa.Im
Ktk Imani ya Ukristo unaitafsri Imani ni kuwa na hakika ya yasiyokuwapo kana kwamba yamekuwepo.
Si lazima Imani ya Ukristo ikupe facts. Msingi wa ukristo ni kuamini. Si ku prove. Ndiyo maana inaitwa Imani. Maana yake it can never be subjected to proofs. Ila kwa wanaoamini wataona utendaji wake.
Hayo ni maneno ya kiimani tuWanaopona bila kumwamini Mungu wanapata uzima wa sasa tu, lakini uzima wa milele wataukosa kwa sababu ya kumkataa Yesu.
Sana,Kumbe na wewe ni kilaza?
Unadai umepona magonjwa 100. Taka walau 10 tu kwa majina na vithibitisho kwamba ulipona.Unaonesha wapi, thibitisha; au unataka na wewe uonekane tu ume-comment
🤣🤣🤣 dohUmepona magonjwa yote , umebakisha moja tu ,Afya ya akili
Hongera sana mkuu kwa kupata matibabu ya bure kwa magonjwa zaidi ya 100.A
Aliyekuzuia kukimbilia Israeli upate huduma nzuri za kiafya ni nani? Mimi nimemkimbilia Yesu nimepona bila kulipa hata senti. Kwenye ushuhuda nimesema kama pesa unazo, nenda Uingereza, nenda Marekani ukapate huduma nzuri. Mimi nisiye na pesa niache nipate huduma ya bure. Period.
Nitapigaje kimya kimya ndugu yangu wakati ninakuonea huruma yatakayokukuta huko mbele. Anyway one day you will remember me na utasema ningejua ningefuata ushauri wa yule jamaa aliyeniambia mambo ya Mungu but it will be too late for you. Maombi yangu Mungu akufunulie siri hii ambayo watu wengi wanaibeza lakini ukweli utasimama tu sikuzote.Huwa mna shida kubwa sana ya akili , sijakuomba uniletee mahubiri , kama hauna jibu ungepiga kimya tu
Unionee huruma kwa lipi? Thibitisha huyo Mungu kama yupo , vitisho vyako wapelekee waumini wenzako kwangu havifanyi kazi yoyote.Nitapigaje kimya kimya ndugu yangu wakati ninakuonea huruma yatakayokukuta huko mbele. Anyway one day you will remember me na utasema ningejua ningefuata ushauri wa yule jamaa aliyeniambia mambo ya Mungu but it will be too late for you. Maombi yangu Mungu akufunulie siri hii ambayo watu wengi wanaibeza lakini ukweli utasimama tu sikuzote.
Hata mimi nimeshagundua, lengo kuu ni kurubuni wajinga.Nimeishasema humu lengo kuu la mada hii sio kujadili majina ya magonjwa...
Tafadhali, usiwaite JF Experts wajinga. Hujasoma hasara 30 za Matusi?Hata mimi nimeshagundua, lengo kuu ni kurubuni wajinga.
Hio maabara ni kisasa. Babu yako alipata dawa maabara ?Jifunze ndugu jinsi dawa zinavyopatikana. Watu wanakaa maabara miaka na miaka wewe unasema ni miracle?
Matusi ni nini?Tafadhali, usiwaite JF Experts wajinga. Hujasoma hasara 30 za Matusi?
Zijue Hasara 30 za Matusi(Kutukana)
Zifuatazo ni hasara za matusi anazopata mtukanaji mwenyewe, na pia hasara anazowasababishia wale anaowatukana: Hasara za Matusi Kiafya: 1. Kutukana kunaongeza viwango vya mfadhaiko wa akili, kiasi cha kusababisha magonjwa ya moyo na kushusha kinga ya mwili. 2. Matusi huamsha hasira na wasiwasi...www.jamiiforums.com
Pole sana nakuombea uzima.. Tena uzima tele.. Kwenye hili naomba niishie hapa japo kiuhalisia kuna mtanziko mkubwaNimeishayataja kwa sehemu, soma replies zangu zote; ila kama wewe ni mzima, mshukuru Mungu usiseme mtu hawezi kuugua magonjwa 100. Codes za magonjwa zipo zaidi ya 55,000 hayo 100 si ni tone tu?
Nikionacho ni kwamba ulikuwa ukiumwa viungo, maumivu ya viungo mara nyingi ni either dalili za ugonjwa fulani, au matokeo a ugonjwa au hali fulani.Huu ni ushuhuda wa kweli kabisa. Katika maisha yangu nimekuwa nikiugua magonjwa mengi ya aina mbalimbali. Kifuani, tumboni, miguuni, katika vidole, machoni, masikioni, puani, kichwani, nk, nk. Muda hautoshi kuyaeleza kwa kina. Kwa haraka haraka naweza kusema tangu ujana wangu nimeugua zaidi ya magonjwa 100. Namshukuru Mungu kwakuwa amekuwa akiniponya magonjwa kila yanaponiijia. Ninachokifanya, kila nikiumwa, namuomba Mungu aniponye kwa Jina la Yesu, kisha naweka mkono wangu juu ya sehemu inayoumwa na kuuamuru ugonjwa utoke kwa Jina la Yesu; kisha naamini kwamba imekuwa hivyo. Wakati mwingine inachukua muda kuona matokeo lakini wakati mwingine ugonjwa unatoweka saa hiyo hiyo. Maneno aliyosema Yesu ni kweli kabisa. Katika Mk 16:17-18 anasema: “Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu(Yesu) watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.”
Huu ni uthibitisho kuwa Mungu yupo na anatenda miujiza hata leo kwa watu wanaomuamini. Kwa ushuhuda huu sikuambii usiende hospitali. La, hasha! Ukiwa na pesa, nenda. Nenda hata hospitali za nje ya nchi. Hata mimi kuna wakati huwa naenda hospitali kwa kuwa najua kwamba Mungu anaweza pia kuponya kwa kuwatumia madaktari. Hata hivyo ninapoenda hospitali bado naweka matumaini yangu kwa Mungu kwakuwa najua madaktari nao kuna magonjwa yako juu ya uwezo wao au elimu yao; na wakati mwingine nadhani huwa wanajisahau, badala ya kutia moyo wanakatisha tamaa. Kuna siku nilipungukiwa damu, nikaenda kumuona Daktari. Aliponipima na kuhakikisha damu imepungua, akaniuliza: “Damu umepeleka wapi wewe?” Usipokuwa na matumaini kwa Mungu ukiulizwa swali hilo la kuvunja moyo unaweza ukaugua mara mbili zaidi. Na kwa magonjwa niliyougua, kama kila ugonjwa ningekuwa nakimbilia hospitali, ningehitajika kuwa milionea maana ningepaswa kulipa pesa nyingi za matibabu. Namshukuru Yesu anaponya bila kulipa hata senti. Nawasikitikia wanaosema eti Mungu hayupo. Wanakosa baraka hizi za uzima.
Hata hivyo kuna vigezo na masharti ya kuzingatia ili mtu aone kikamilifu uponyaji wa Mungu kwa Jina la Yesu. Baadhi ya vigezo vimeelezwa katika Andiko hili: Kutoka 15:26. “Mungu akasema, ‘Kama mtaisikiliza kwa bidii sauti yangu mimi BWANA Mungu wenu na kuyafanya yaliyo sawa mbele yangu, kama mtayatii maagizo yangu na kuzishika amri zangu zote, sitaleta juu yenu ugonjwa wowote niliowaletea Wamisri, kwa kuwa Mimi ndimi BWANA, niwaponyaye.’” Uponyaji wa Mungu ni wa bure kwa wote wanaozingatia maneno hayo. Ukisikia Mtumishi anakuambia ulipe pesa kwanza ndio akuombee, jihadhari naye. Yesu alipowapa mamlaka wanafunzi wake ya kukemea pepo na kuweka mikono juu ya wagonjwa ili wapone, aliwaambia amewapa bure, hivyo wanapaswa kutoa huduma hiyo bure(Mathayo 10:8).
Yamkini unaumwa, umetibiwa kila mahali hujapona. Usikate tamaa. Ushuhuda huu ukutie moyo kuwa unaweza kupona kwa uwezo wa Jina la Yesu Kristo. Yote yawezekana kwake aaminiye(Mk 9:23). Amen.
Labda nikuulize kwa maajabu gani ya yesu mpaka umpe vyeo ambavyo hastailiYesu ni zaidi ya Mitume...
1. Yesu ni Mungu
2. Yesu ni Mfalme wa Wafalme
3. Yesu ni Alfa na Omega
4. Yesu ni Mwokozi wa Ulimwengu
5. Yesu ni Mchungaji Mwema
6. Yesu ni Nuru ya Ulimwengu
7. Yesu ni Njia, Kweli, na Uzima
8. Yesu ni Emanueli (Mungu Pamoja Nasi)
9. Yesu ni Mwana wa Mungu
10. Yesu ni Mtakatifu wa Mungu
11. Yesu ni Bwana wa Mabwana
12. Yesu ni Mwamba wa Wokovu
13. Yesu ni Mshauri wa Ajabu
14. Yesu ni Daktari Mkuu
15. Yesu ni Mkombozi
16. Yesu ni Tumaini la Mataifa
17. Yesu ni Kiongozi wa Uzima
18. Yesu ni Karama ya Mungu
19. Yesu ni Shujaa wa Milele
20. Yesu ni Mwanakondoo wa Mungu
Nani mwingine mwenye majina kama hayo
Kama wewe unajua matusi ni nini tuambie, unaweza kudhani unajua maana ya tusi kumbe hujui, unaishi kwa mazoea tu.Wewe unaishi dunia ipi hujui matusi