Amini, Usiamini. Nimepona Magonjwa 100+ Kwa Jina la Yesu!

Jibu swali nililokuuliza,alikua anamuomba Mungu yupi?

Wewe ni kilaza hujui lolote ndio maana unakwepa hoja zangu,wahi Milembe ukaanze tiba.
Nimekuambia tulia, uwe na subira. Siwezi kueleza kila kitu kwa siku moja.
 
Hujui lolote wewe,acha kuhamisha magoli,usitafute pakutokea,
Nilijua tu swali langu usingekua na uwezo wa kulijibu,
Umeishia kuruka ruka tu kama Kuku aliyekatwa kichwa kisha akaachiwa ghafla.
 
Hilo swali ndio umeona gumu. Inaonekana wewe umekaririshwa tu mistari na wanaopinga Uungu wa Yesu. Kwa sasa nimekuambia sikujibu. Kujibu hilo swali lazima nianzie mbali. Huu uzi sio mahali pake. Period
 
Wewe una tatizo kichwani sio bure,akili ya kujibu swali langu huna,
Ndio maana uzi wako umesusiwa,una onekana kabisa kua una tatizo kichwani,kuna kitu hakipo sawa.
 
Huu ni ushuhuda wa kweli kabisa. Katika maisha yangu nimekuwa nikiugua magonjwa mengi ya aina mbalimbali. Kifuani, tumboni, miguuni, katika vidole, machoni, masikioni, puani, kichwani, nk, nk. Muda hautoshi kuyaeleza kwa kina. Kwa haraka haraka naweza kusema tangu ujana wangu nimeugua zaidi ya magonjwa 100. Namshukuru Mungu kwakuwa amekuwa akiniponya magonjwa kila yanaponiijia. Ninachokifanya, kila nikiumwa, namuomba Mungu aniponye kwa Jina la Yesu, kisha naweka mkono wangu juu ya sehemu inayoumwa na kuuamuru ugonjwa utoke kwa Jina la Yesu; kisha naamini kwamba imekuwa hivyo. Wakati mwingine inachukua muda kuona matokeo lakini wakati mwingine ugonjwa unatoweka saa hiyo hiyo. Maneno aliyosema Yesu ni kweli kabisa. Katika Mk 16:17-18 anasema: “Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu(Yesu) watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.”

Huu ni uthibitisho kuwa Mungu yupo na anatenda miujiza hata leo kwa watu wanaomuamini. Kwa ushuhuda huu sikuambii usiende hospitali. La, hasha! Ukiwa na pesa, nenda. Nenda hata hospitali za nje ya nchi. Hata mimi kuna wakati huwa naenda hospitali kwa kuwa najua kwamba Mungu anaweza pia kuponya kwa kuwatumia madaktari. Hata hivyo ninapoenda hospitali bado naweka matumaini yangu kwa Mungu kwakuwa najua madaktari nao kuna magonjwa yako juu ya uwezo wao au elimu yao; na wakati mwingine nadhani huwa wanajisahau, badala ya kutia moyo wanakatisha tamaa. Kuna siku nilipungukiwa damu, nikaenda kumuona Daktari. Aliponipima na kuhakikisha damu imepungua, akaniuliza: “Damu umepeleka wapi wewe?” Usipokuwa na matumaini kwa Mungu ukiulizwa swali hilo la kuvunja moyo unaweza ukaugua mara mbili zaidi. Na kwa magonjwa niliyougua, kama kila ugonjwa ningekuwa nakimbilia hospitali, ningehitajika kuwa milionea maana ningepaswa kulipa pesa nyingi za matibabu. Namshukuru Yesu anaponya bila kulipa hata senti. Nawasikitikia wanaosema eti Mungu hayupo. Wanakosa baraka hizi za uzima.

Hata hivyo kuna vigezo na masharti ya kuzingatia ili mtu aone kikamilifu uponyaji wa Mungu kwa Jina la Yesu. Baadhi ya vigezo vimeelezwa katika Andiko hili: Kutoka 15:26. “Mungu akasema, ‘Kama mtaisikiliza kwa bidii sauti yangu mimi BWANA Mungu wenu na kuyafanya yaliyo sawa mbele yangu, kama mtayatii maagizo yangu na kuzishika amri zangu zote, sitaleta juu yenu ugonjwa wowote niliowaletea Wamisri, kwa kuwa Mimi ndimi BWANA, niwaponyaye.’” Uponyaji wa Mungu ni wa bure kwa wote wanaozingatia maneno hayo. Ukisikia Mtumishi anakuambia ulipe pesa kwanza ndio akuombee, jihadhari naye. Yesu alipowapa mamlaka wanafunzi wake ya kukemea pepo na kuweka mikono juu ya wagonjwa ili wapone, aliwaambia amewapa bure, hivyo wanapaswa kutoa huduma hiyo bure(Mathayo 10:8).

Yamkini unaumwa, umetibiwa kila mahali hujapona. Usikate tamaa. Ushuhuda huu ukutie moyo kuwa unaweza kupona kwa uwezo wa Jina la Yesu Kristo. Yote yawezekana kwake aaminiye(Mk 9:23). Amen.

Hahahaha
Kwa hiyo mwamba huyu anakipaji cha kutibu pia kuachana na kuigiza
1736414835517.jpeg
 
Hawa watu wanaodai wamepona kwa dua au kwa jina la Yesu Mara nyingi kinachowasumbua ni magonjwa yanayotokana na hisia na sio magonjwa halisi.

Ilipoingia covid ulimwengu mzima uliitazama zaidi sayansi pamoja na huko dini zilipotoka.

Huko dini zilipoanzia ni mojawapo ya nchi zenye huduma nzuri za kiafya za kisayansi,,,Saud Arabia na Israel.

Hata wanaojiita manabii wote wakiumwa kimbilio lao ni kwenye matibabu ya kisayansi hospitali.
 
Wewe una tatizo kichwani sio bure,akili ya kujibu swali langu huna,
Ndio maana uzi wako umesusiwa,una onekana kabisa kua una tatizo kichwani,kuna kitu hakipo sawa.
Hongera kwa kuwa mzima kichwani
 
A
Hawa watu wanaodai wamepona kwa dua au kwa jina la Yesu Mara nyingi kinachowasumbua ni magonjwa yanayotokana na hisia na sio magonjwa halisi.

Ilipoingia covid ulimwengu mzima uliitazama zaidi sayansi pamoja na huko dini zilipotoka.

Huko dini zilipoanzia ni mojawapo ya nchi zenye huduma nzuri za kiafya za kisayansi,,,Saud Arabia na Israel.

Hata wanaojiita manabii wote wakiumwa kimbilio lao ni kwenye matibabu ya kisayansi hospitali.
Aliyekuzuia kukimbilia Israeli upate huduma nzuri za kiafya ni nani? Mimi nimemkimbilia Yesu nimepona bila kulipa hata senti. Kwenye ushuhuda nimesema kama pesa unazo, nenda Uingereza, nenda Marekani ukapate huduma nzuri. Mimi nisiye na pesa niache nipate huduma ya bure. Period.
 
Huna unalolijua wewe,hujui chochote,nimekupa aya hujaweza kunijibu,
wahi Milembe ukatibiwe.
Wewe unapenda ubishi. Nimekuambia swali lako haliwezi kujibiwa kwa paragraph moja. Linahitaji ufafanuzi na mistari ya kutosha. Kukujibu hapa ni kuchanganya mada ndani ya mada. Nikipata muda nitaeleza kwenye uzi maalum. Uwe na subira!
 
Rubbish.
 
Ulisoma Chuo gani ambapo wanafunzi wanaanza kuuliza maswali kabla ya lecturer kutoa lecture? Subiri kwanza upate lecture halafu kama utakuwa hujaelewa uliza hilo swali lako. Matusi unayotoa yanakuongezea dhambi tu.
 
Back
Top Bottom