Amini usiamini vita waliyoianzisha Hamas huko gaza imefungua ukurasa mpya wa ufahamu na utapelekea kutimia kwa tabiri muhimu za biblia

Amini usiamini vita waliyoianzisha Hamas huko gaza imefungua ukurasa mpya wa ufahamu na utapelekea kutimia kwa tabiri muhimu za biblia

joex

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2011
Posts
1,598
Reaction score
1,294
Nakusihi utumie muda wako kujielimisha kupitia mahojiano haya kwenye video hapa chini ambayo Zuby (gwiji aliyepata kumhoji Elon Mask) anamhoji Loay Alshareef, msaudia aliyezaliwa na kukulia Saudia ila kwa sasa amefanya makazi yake Abbudhabi, UAE.

Highlights za mahojiano
Zuby akiwa mtoto wa expatrate alikulia Jeddah na kusoma huko, lakini hajui kiarabu, kwa sababu sera za Elimu Saudia zinatenga shule kwa watoto wa expatriates na huko strictly hamna kufundishwa kiarabu: USIRI WA WAARABU ILI TUSIJUE KILICHOANDIKWA KWENYE QURAN

Loay toka mtoto alifunzwa dini na kupata kusoma vitabu vyote kikamilifu ikijumuisha Sunna za Mohammad vitabu sita muhimi ikiwa ni pamoja na Sahihi bukhari

Alshareef asema kuwa Quran inasema ugomvi wa Waislamu na Jews ni wa milele. Pia asema kuwa Quran inafundisha kuwa Waislamu hawatakiwi kuwa na urafiki na Wayahudi na Wakristo

Alshareef anamshukuru Mungu kwani alipata bahati ya kuenda France ktk exchange program ambapo akaka na Familia ya Wayahudi. Ktk familia hiyo alikuja kujifunza kuwa Torah haifundishi chuki dhidi ya jamii yeyote nyingine ya DINI, hata Waislamu. Aidha, alijionea mwenyewe upendo walionao Jews hao kwake. Fursa hiyo ilimfanya ajifunze zaidi kuhusu historia ya taifa la Israel na kuja kujua kuwa kume taifa hilo limekuwepo tangu miaka 3000 BCE na Daudi akiwa ndiye mfalme wao aliyeasisi hekalu la Jerusalem

Alshareef asema kuwa Hamasi kuianzisha hii vita ni njama za Maislamists ya kuvuruga mkataba wa amani kati ya Israel na mataifa ya kiarabu yanayotaka amani Abrahamic Accord.

Alshareef anasema kuwa mataifa ya kiarabu ya Saudia UAE, Bahrain na mengine kama Morocco na Egypt waneona mapungufu ktk Quran kwa maana ya context ya wakati huo mtume Mohammed akiisha ambayo haifai kutumika ktk karne ya 21. Hivyo wako mbioni kufanyia REFORM baadhi ya mafundisho hayo ya kiislamu ili waishi kwa AMANI na COUSINS wao wayahudi. Ametoa mfano kule UAE ambako serikali imeruhusu wayahudi na wakristo kuishi, kufanya kazi na kuwa na majengo yao ya Ibada. Aidha, anasema MBS wa Saudi arabia anaendelea na reforms kama hizo.

Alshareef anasema Hamasi na Muslim brotherhood watashindwa hii vita; na anasema viongozi wa nchi za kiarabu hawataki Gaza itakayobaki baada ya vita itawaliwe na HAMASI.

Alshareef anasema kuwa Hamasi ktk charter yao ya 1988 wanasema moja kwa moja hati ktk tafsiri ya kiingereza kuwa lengo ni kuua kila myahudi. Lakini walipokuja kuifanyia Review mwaka 2017 kipengere hicho wakakiondoa kwenye tafsiri ya kiingereza ila bado kipo ktk tafsiri ya Kiarabu

Anaendelea kusema kuwa waarabu wameanza kuona umaana wa ile statue ya Amani iliopo ktk majengo ya UN ambayo kwa maneno yake Alshareef anasema yanatoka kwa Nabii Isaiah ambao wao Waislamu wanamheshimu pia. Isaiah 2:4 respecting many peoples. They will beat their swords into plowshares And their spears into pruning shears. Nation will not lift up sword against nation, Nor will they learn war anymore.

Screenshot_20240831-190128_Chrome.jpg
Kutokana na maoni haya ya Alshareef naweza sema tena kuwa vita aliyoianzisha Hamasi, imeendelea kuwafungua macho waislamu wengi kujua kuwa mafundisho ya kitabu cha Quran yanatakiwa kufanyiwa reform ili waishi kwa Amani na Jews na Jamii nyingine za Dini ktk karne hii ya 21
Vita hii, na ukweli kuwa watu wengi sasa wamechoka vita na wanachotaka ni kufocus kwenye maendeleo, mm naona unabii wa BIBLIA wa 1 Thessalonians 5:3 Mataifa kuanzimia kuleta Amani.

Ktk hili la kuleta Amani ambapo baada ya hapo Maislamists kwa vichwa vyao vigumu watapinga, Viongozi watawapiga Marufuku. Lakini ukiangalia mwenendo wa Serikali za Magharibi ambazo huwa wanawaogopa Maislamists, wao wataona ni bora kupiga marufuku Dini zote kutia ndani na za kikiristo ili wasionekane wanapendelea upande mmoja.

Hivyo basi ili Serikali za Dunia zipige marufuku dini zote (Ufunuo 18:4) kule nchi za Magharibi itabidi Serikali zilizopo madarakani ziwe zile zenye MRENGO WA KUSHOTO ( DEMOCRATS & LABOUR) kwa UINGEREZA NA MAREKANI. UPANDE WA MASHARIKI YA KATI, Serikali ya Kitheocracy ya Kiislamu ya Iran inabidi isiwe madarakani(najua this is a tough staff for some of you to comprehend)

Naomba fuatilia kwa makini majojiano hayo


View: https://youtu.be/lLCjSfr57V0?si=CzbeA1_6QMYy_ikx
 
Back
Top Bottom