Amiri Jeshi mkuu anaegopa wauza unga na wezi wa EPA ataweza kutuongoza vitani?

Amiri Jeshi mkuu anaegopa wauza unga na wezi wa EPA ataweza kutuongoza vitani?

Acha kujitoa akili,External Payment Account uombwe urudishe ikiwa umechukua halali????? kwa nini urudishe kilicho chako kihalali? FYI uhitaji taarifa za Slaa kujua "scandal" ya EPA

Sasa kama unajuwa hilo kwanini unauliza kama wote wamerudisha? Wanaorudisha ni wale na zile tu ambazo hawajafanya hizo external payments. Kumbuka hilo.
 
hapa ndio umeongea nini mkuu? ukweli ni kwamba hao wauza unga ndio waliomuweka madarakani na wengi amewapa madaraka ubunge etc .usitufanye wajinga wanaokamatwa kwenye unga sio madealer ni mateja tu ambapo ni sawa nakukata matawi umeacha mti na mizizi yake

Basi nchi nzima hii wanauza unga maana kapata kura kwa kishindo na wapiga kura ndio wanaamuwa wampe nani awaongoze.
 
Basi nchi nzima hii wanauza unga maana kapata kura kwa kishindo na wapiga kura ndio wanaamuwa wampe nani awaongoze.
pole yako kama unaamini alichaguliwa na wananchi ,pole sana dada pole
 
Hamjaziona kesi za epa na watu kufungwa?

Hamuoni watu wa unga wanavyokamatwa kila siku?

Chuki zenu ni za kibinafsi na roho zanu zilivyombaya kila mnapoona mafanikio ya Kikwete nyie ndio mnazidi uhasidi. Mtaungulika sana, Kikwete ndio Rais na Mohamed Gharib Bilal ndio makamu wake.

unaweza kuwataja angalau wauza unga wa tano
 
we na slaa lenu moja nani kakwambia tunataka vita sisi tunataka maendeleo hiyo vita fanyeni kwenye chama chenu ambacho mmezoea vita .
 
kukata kuti ulilokalia haiwezekani we jamaa vipiiii :mmph:
 
Tatizo lako hujuwi maana ya EPA ni nini, kwanini wafungwe kama hawana dhambi? unanchekesha.

Mambo ya dhambi ni hukumu za mbinguni we bi kizee, mambo ya EPA ni makosa ya jinai ambayo sheria inataka wapelekwe mahakamani kesi isikilizwe hukumu itolewe. Kilichofanywa na Kikwete ni Kumwambia Manji arudishe hela alizoiba na Jeetu Patel kapelekwa mahakamani kesi haijaitwa kwa miaka mitatu ili kutuzuga. Au unaongelea EPA ipi bi kizee???
 
Weweeeeeeeee banaa! mcheza ngoma na vita wapi na wapi!? Muachage kusingizia watu fani zisizowahusu
 
Hamjaziona kesi za epa na watu kufungwa?

Hamuoni watu wa unga wanavyokamatwa kila siku?

Chuki zenu ni za kibinafsi na roho zanu zilivyombaya kila mnapoona mafanikio ya Kikwete nyie ndio mnazidi uhasidi. Mtaungulika sana, Kikwete ndio Rais na Mohamed Gharib Bilal ndio makamu wake.

Hivi Muhamed yupo?

Vipi Mrisho yale majina alisema anayo hivi ameshawataja kweli?
 
Hivi tujiulize,Raisi asieweza hata kuwakamata na kuhakikisha wauza madawa ya kulevya na wezi wa EPA ndani ya nchi ataweza kweli kuongoza majeshi yetu katika vita dhidi ya taifa lingine?

Wabongo tusithubutu kuingia vitani chini ya Raisi wa sasa.Tutaambulia aibu na kipigo,Amiri jeshi mkuu wa sasa sidhani kama anaweza hata kuhamasisha majeshi yetu na siamini hata wanajeshi wetu wana imani na nae.

Mgogoro baina yetu na Malawi na sasa Rwanda ni bora tu ukaishia kuwa ni wa vita ya maneno tu.

Nina mashaka kama kweli Amiri Jeshi Mkuu wa sasa anaweza hata kuhutubia wanajeshi na kuwapa ujasiri.Ukishaonekana ni dhaifu ndani ya nchi yako hata wanajeshi wanapoteza imani na wewe na kujiona hawana kiongozi anaewafaa.

Tafakari ukiwa "realistic" na sio kishabiki uone utapata jibu gani.

Mkuu!
Usichanganye siasa na masuala ya ulinzi wa nchi.
Hayo mambo ya EPA,dawa za kulevya yako kisiasa zaidi,ambapo yote hayo
yamezunguzwa sana.
Logical ni bora watu wetu wakaangamia taratibu kwa tamaa zao za kutumia
dawa za kulevya,kuliko nchi kuvamiwa na watu kuuliwa hovyo hovyo kila mahali.
Ni vema tusiingilie kabisa masuala ya operations za kijeshi au kutumika kuwavunja
nguvu wapiganaji wetu kupitia siasa.
 
Hii kitu ina ukweli ndani yake, wauza unga hawana silaa ila mkuu wa kaya kachemsha kuwataja! na mkumbuke kagame ni moja nchi inayo spend hela nyingi kwenye kununua silaa hasa za kisasa na ni inchi ya pili au tatu katika east africa kuwa na silaa za kisasa na bora na jeshi imara. siyo wanajeshi wetu hawa wanaotorosha pembe za ndovu ........Wanajeshi wetu wanaweza kupigana na wamachinga mtwara
 
Hamjaziona kesi za epa na watu kufungwa?

Hamuoni watu wa unga wanavyokamatwa kila siku?

Chuki zenu ni za kibinafsi na roho zanu zilivyombaya kila mnapoona mafanikio ya Kikwete nyie ndio mnazidi uhasidi. Mtaungulika sana, Kikwete ndio Rais na Mohamed Gharib Bilal ndio makamu wake.

mimi naona kesi za ugaidi tu kila kukicha
 
Back
Top Bottom