Amiri Jeshi mkuu anaegopa wauza unga na wezi wa EPA ataweza kutuongoza vitani?

Acha kujitoa akili,External Payment Account uombwe urudishe ikiwa umechukua halali????? kwa nini urudishe kilicho chako kihalali? FYI uhitaji taarifa za Slaa kujua "scandal" ya EPA

Sasa kama unajuwa hilo kwanini unauliza kama wote wamerudisha? Wanaorudisha ni wale na zile tu ambazo hawajafanya hizo external payments. Kumbuka hilo.
 

Basi nchi nzima hii wanauza unga maana kapata kura kwa kishindo na wapiga kura ndio wanaamuwa wampe nani awaongoze.
 
Basi nchi nzima hii wanauza unga maana kapata kura kwa kishindo na wapiga kura ndio wanaamuwa wampe nani awaongoze.
pole yako kama unaamini alichaguliwa na wananchi ,pole sana dada pole
 

unaweza kuwataja angalau wauza unga wa tano
 
we na slaa lenu moja nani kakwambia tunataka vita sisi tunataka maendeleo hiyo vita fanyeni kwenye chama chenu ambacho mmezoea vita .
 
kukata kuti ulilokalia haiwezekani we jamaa vipiiii :mmph:
 
Tatizo lako hujuwi maana ya EPA ni nini, kwanini wafungwe kama hawana dhambi? unanchekesha.

Mambo ya dhambi ni hukumu za mbinguni we bi kizee, mambo ya EPA ni makosa ya jinai ambayo sheria inataka wapelekwe mahakamani kesi isikilizwe hukumu itolewe. Kilichofanywa na Kikwete ni Kumwambia Manji arudishe hela alizoiba na Jeetu Patel kapelekwa mahakamani kesi haijaitwa kwa miaka mitatu ili kutuzuga. Au unaongelea EPA ipi bi kizee???
 
Weweeeeeeeee banaa! mcheza ngoma na vita wapi na wapi!? Muachage kusingizia watu fani zisizowahusu
 

Hivi Muhamed yupo?

Vipi Mrisho yale majina alisema anayo hivi ameshawataja kweli?
 

Mkuu!
Usichanganye siasa na masuala ya ulinzi wa nchi.
Hayo mambo ya EPA,dawa za kulevya yako kisiasa zaidi,ambapo yote hayo
yamezunguzwa sana.
Logical ni bora watu wetu wakaangamia taratibu kwa tamaa zao za kutumia
dawa za kulevya,kuliko nchi kuvamiwa na watu kuuliwa hovyo hovyo kila mahali.
Ni vema tusiingilie kabisa masuala ya operations za kijeshi au kutumika kuwavunja
nguvu wapiganaji wetu kupitia siasa.
 
Hii kitu ina ukweli ndani yake, wauza unga hawana silaa ila mkuu wa kaya kachemsha kuwataja! na mkumbuke kagame ni moja nchi inayo spend hela nyingi kwenye kununua silaa hasa za kisasa na ni inchi ya pili au tatu katika east africa kuwa na silaa za kisasa na bora na jeshi imara. siyo wanajeshi wetu hawa wanaotorosha pembe za ndovu ........Wanajeshi wetu wanaweza kupigana na wamachinga mtwara
 

mimi naona kesi za ugaidi tu kila kukicha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…