Amkeni kuna wizi wa Watoto na Utekaji wa Polisi

Ileje

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
9,524
Reaction score
13,682
Watanzania tusipumbazwe na utetezi wa polisi kuhusu utekaji, upo!

Ni hivi wizi wa watoto umekuwepo kutoka zama za kale. Wizi wa watoto hufanywa na wanawake ambao hawajabahatika kupata watoto kwa hiyo huamua kuiba ili angalau waonekane wana watoto. Aidha kuna wanawake wenye watoto wa kike na hawajabahatika kupata watoto wa kiume, nao hawa huiba watoto wa kiume ili wapate mchanganyiko wa watoto wa kiume na kike.

Wizi wa watoto pia hufanywa na washirikina au wachawi kwa ajili ya shughuli zao za uchawi au ushirikina. Wachawi au washirikina pia huwaiba watoto albino na kuwaua watu wazima albino na wenye vipara nk.

Sasa kuna huu utekaji wa watu wazima ambao hufanywa na polisi ambao umeibuka hivi karibuni. Utekaji huu ni mpango mahsusi wa watawala kutumia polisi kuwapoteza au kuwanyamazisha mahasimu wao wa kisiasa au watu wanaopingana na watawala. Mifano ipo mingi na hivi karibuni tumeona Sativa na Kombo walivyofanywa. Wengine ni kama Kabendera, Saanane nk.

Kwa hiyo wananchi tukae tukijua hakuna aliye salama ni suala la muda tu!
 
Mama anasema ni DRAMA
 
Hawa ambao hawakubahatika kupata watoto kwa nini hawaendi vituo vya watoto yatima wachukua watoto wakawaasili? Kwa nini waibe?
 
Hawa ambao hawakubahatika kupata watoto kwa nini hawaendi vituo vya watoto yatima wachukua watoto wakawaasili? Kwa nini waibe?
Wanawaiba ili waonekane wana kizazi! Hujasikia mwanawake anajibebesha mimba feki baada ya miezi kadhaa anasafiri asikofahamika na huko anaiba mtoto na baadaye anarudi kwa mumewe na kumdanganya amejifungua?
 
Wizi wa watoto pia hufanywa na washirikina au wachawi kwa ajili ya shughuli zao za uchawi au ushirikina. Wachawi au washirikina pia huwaiba watoto albino na kuwaua watu wazima albino na wenye vipara nk.
Huenda ni yaleyale ya albino
 
Kama Polisi nao niwatekaji hawawezi kuuzungumzia utekaji na ikaeleweka.
Shetani hawezi kumtoa shetani mwenzie.
Ndiyo sababu ukimwangalia Jumanne Mulilo, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar utaona uso wake unavyojisuta kwa aibu anapotetea uhalifu!
 
Ndiyo sababu ukimwangalia Jumanne Mulilo, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar utaona uso wake unavyojisuta kwa aibu anapotetea uhalifu!
Anavyokaza uso akiongea utadhani anakula nyanya chungu 🥺🥺🥺
 
Watoto wanaibiwa kwa mambo ya ushirikina tu hakuna kingine..wezi wa Watoto wangekua wanapata adhabu kali hizi mambo tungekua tunazisikia tu..
 
Watoto wanaibiwa kwa mambo ya ushirikina tu hakuna kingine..wezi wa Watoto wangekua wanapata adhabu kali hizi mambo tungekua tunazisikia tu..
Tatizo ni kuwa polisi wanatumia wizi wa watoto kuficha udhalimu wao wa kuteka watu!
 
Watu,media wako bize kucheza komasava,kutangaza umbea udaku...dawa za nguvu za kiume makalio makubwa
Ubishi wa mpira

Ova
 
Watu,media wako bize kucheza komasava,kutangaza umbea udaku...dawa za nguvu za kiume makalio makubwa
Ubishi wa mpira

Ova
Sasa hivi wanajadili Kibu Denis kutokuwepo kambini Egypt na Mzengeli kuuzwa Kaizer Chiefs!
 
Wizi wa watoto wadogo mitaani katika jiji
Your browser is not able to display this video.
la Dar-es-salaam
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…