Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 9,524
- 13,682
Watanzania tusipumbazwe na utetezi wa polisi kuhusu utekaji, upo!
Ni hivi wizi wa watoto umekuwepo kutoka zama za kale. Wizi wa watoto hufanywa na wanawake ambao hawajabahatika kupata watoto kwa hiyo huamua kuiba ili angalau waonekane wana watoto. Aidha kuna wanawake wenye watoto wa kike na hawajabahatika kupata watoto wa kiume, nao hawa huiba watoto wa kiume ili wapate mchanganyiko wa watoto wa kiume na kike.
Wizi wa watoto pia hufanywa na washirikina au wachawi kwa ajili ya shughuli zao za uchawi au ushirikina. Wachawi au washirikina pia huwaiba watoto albino na kuwaua watu wazima albino na wenye vipara nk.
Sasa kuna huu utekaji wa watu wazima ambao hufanywa na polisi ambao umeibuka hivi karibuni. Utekaji huu ni mpango mahsusi wa watawala kutumia polisi kuwapoteza au kuwanyamazisha mahasimu wao wa kisiasa au watu wanaopingana na watawala. Mifano ipo mingi na hivi karibuni tumeona Sativa na Kombo walivyofanywa. Wengine ni kama Kabendera, Saanane nk.
Kwa hiyo wananchi tukae tukijua hakuna aliye salama ni suala la muda tu!