Superbug
JF-Expert Member
- Jan 31, 2018
- 13,864
- 35,079
Umeongea vyema Sana na huu ndio ukweli mtupu kuielezea serikali hii na ndio maana inaungwa mkono na watu wa aina tatuKwa sababu ni serikali iliyojengwa kwenye misingi ya uongo na uzushi, serikali inayopika takwimu ili ionekane inafanya kazi hivyo wanazuia watu msiwachallenge kwenye uongo. Wanataka wakisema umasikini umepunga 92% asitokee mtu wa ku-challenge au kuhoji umasikini umepunguaje, ukihoji unaitwa sio mzalendo, utapewa kesi ya uraia. Yaani hii serikali ya wanyonge kua mzalendo maana yake ni kua taahira, mtu mpumbavu asietumia akili kuhoji, ukihoji tu kosa.
Ni serikali ambayo inataka ikisema imejenga viwanda 4,000(vingi kuliko vya ujerumani, ujerumani wana viwanda 2,500) kwa miaka 4 kila mtu akubali, maana yake kiwanda kimoja kimejengwa kwa wastani wa siku 3.
Ni serikali ambayo ikisema ilipoingia madarakani faru waikua 5 ila leo wako 145(ukihoji ina maana siku hizi faru wanataga mayai), unaishia kupata kesi, inasema tembo walikua 500 leo wako karibu 50,000 unashangaa tembo siku hizi anazaa kama samaki?
Serikali ikisema uchumi unakua 17%, asitokee mtu wa kuhoji, ukihoji unaishia jela.
Wenye upeo mdogo (Hawa ni wale wazee wa vijijini wengi wao mpk Leo wanavaa makofia na maflana ya CCM yaliyochoka ambao wanaaminishwa kirahisi vyama vingi vitaleta Vita ujinga wa enzi zile wanao mpk Leo.
Wanufaika na mfumo dhalimu (Hawa ni makada na wooote wenye maslahi ya wazi au ya Siri na ccm na serikali yake hapa pia wapo wanaofanya siasa Kama ajira
Wachumia tumbo (Hawa wanajua ujinga uliopo ila wameamua kuwa wanafiki makusudi Hawa pia Ni wataka vyeo na teuzi hili Ni kundi hatari Sana kwasababu Lina include vijana wa vyuo vikuu ambao wanajitangaza kwenye social media wakiamini kwamba ipo siku wataonekana na kupata teuzi za kisiasa.