Amos Kisenge apewa barabara

Amos Kisenge apewa barabara

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
AMOS KISENGE APEWA BARABARA

Amos Kisenge amepewa barabara kwa kutambua mchango wake katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Bahati mbaya hapo nilipokuta picha hii haikuelezwa Barabara ya Amos Kisenge iko wapi ingawa bila shaka itakuwa Upareni kwani ndipo kwao alikozaliwa.

Wakati natafiti kitabu cha Abdul Sykes nilielezwa na Sheikh Abdallah Rashid Sembe mkutano wa siri uliofanyika Tanga kati ya Julius Nyerere akiwa na Amos Kisenge na viongozi wa TANU Tanga walipokwenda Tanga mwaka wa 1958.

Nyerere na Kisenge walikwenda Tanga kuonana na viongozi wa TANU Hamisi Kheri, Sheikh Abdallah Rashid Sembe, Mwalimu Kihere na wengineobl kuweka mkakati wa kukabili upinzani wa Kura Tatu ndani ya chama.

Upinzani huu ulikuwa ukiongozwa na Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU na Katibu Mkuu wa TANU Zuberi Mtemvu.

Nyerere kwa kutaka kumkwepa Mtemvu katika mkutano huu wa "Mkakati wa Tanga," alimuomba Mtemvu abakie TANU HQ New Street yeye atawakilishwa na Makamo Katibu Mkuu Amos Kisenge.

Nyerere hakutaka kumchukua Mtemvu kwani agenda ya kikao cha Tanga ilikuwa kuweka mikakati ya kupambana na wanaopinga Kura Tatu.

Mtemvu hakuambiwa agenda kuu ya safari ile.

Hivi ndivyo Amos Kisenge alivyoshiriki katika mkutano ule maarufu na muhimu kwa TANU na akashiriki pia yeye na Nyerere katika dua kubwa iliyofanyika Mnyanjani kijiji kidogo nje ya Tanga kuomba mafanikio.

Amos Kisenge kakumbukwa na taifa hili kwa mchango wake katika kupigania uhuru wa Tanganyika na katunukiwa barabara.

Screenshot_20230313-142521_Facebook.jpg
 
Nyerere kwa kutaka kumkwepa Mtemvu katika mkutano huu wa "Mkakati wa Tanga," alimuomba Mtemvu abakie TANU HQ New Street yeye atawakilishwa na Makamo Katibu Mkuu Amos Kisenge.
Heshima yako ndugu Mohamed Said ,

Je ni sababu zipi hasa zilizopelekea Mwl. Nyerere kumkwepa Mtemvu? kwenye huo mkutano husika.
 
Heshima yako ndugu Mohamed Said ,

Je ni sababu zipi hasa zilizopelekea Mwl. Nyerere kumkwepa Mtemvu? kwenye huo mkutano husika.
Mwal...
Zuberi Mtemvu na Sheikh Suleiman Takadir walikuwa wapinzani wa Kura Tatu.

Mwalimu alikwenda Tanga kutafuta msaada wa akina Sheikh Rashid Sembe, Hamisi Heri na Mwalimu Kihere waunge mkono kushiriki uchaguzi.

Angekwenda na Mtemvu asingefanikiwa katika azma yake.
 
HAHAHAHAH HAYA MABARABARA WAMEPEWA MPAKA MACHANGU DOA MAARUFU WAKATI HUU WA POST CODE. WAMPE MTAA AU CHUO KIMOJA WAPO CHA MIFUGO/KILIMO HUKO UPARENI.
 
Asalaam wlk mtoa mada, Nami napenda sana kusoma vitabu na majalada hadi newspapers, ningependa mno nikipate kitabu cha history cha Ally Sykes ambaye babu yake, Sykes Mbuwane alikua ni Zulu warrior, je kuna sehemu yeyote ameongelea kuhusu wale 20 Nightingales ambao walikuwa recruited from SA baada ya uhuru, maana tuliokuwa nao wengi walitukimbia,na nimesoma sehemu kuwa operation hii iliombwa na President Nyerere na Ally Sykes aliisimamia,au wewe una informations zozote kuhusiana na operation hii,please share Nami hapa, shukraani
 
Back
Top Bottom