Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
AMOS KISENGE APEWA BARABARA
Amos Kisenge amepewa barabara kwa kutambua mchango wake katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Bahati mbaya hapo nilipokuta picha hii haikuelezwa Barabara ya Amos Kisenge iko wapi ingawa bila shaka itakuwa Upareni kwani ndipo kwao alikozaliwa.
Wakati natafiti kitabu cha Abdul Sykes nilielezwa na Sheikh Abdallah Rashid Sembe mkutano wa siri uliofanyika Tanga kati ya Julius Nyerere akiwa na Amos Kisenge na viongozi wa TANU Tanga walipokwenda Tanga mwaka wa 1958.
Nyerere na Kisenge walikwenda Tanga kuonana na viongozi wa TANU Hamisi Kheri, Sheikh Abdallah Rashid Sembe, Mwalimu Kihere na wengineobl kuweka mkakati wa kukabili upinzani wa Kura Tatu ndani ya chama.
Upinzani huu ulikuwa ukiongozwa na Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU na Katibu Mkuu wa TANU Zuberi Mtemvu.
Nyerere kwa kutaka kumkwepa Mtemvu katika mkutano huu wa "Mkakati wa Tanga," alimuomba Mtemvu abakie TANU HQ New Street yeye atawakilishwa na Makamo Katibu Mkuu Amos Kisenge.
Nyerere hakutaka kumchukua Mtemvu kwani agenda ya kikao cha Tanga ilikuwa kuweka mikakati ya kupambana na wanaopinga Kura Tatu.
Mtemvu hakuambiwa agenda kuu ya safari ile.
Hivi ndivyo Amos Kisenge alivyoshiriki katika mkutano ule maarufu na muhimu kwa TANU na akashiriki pia yeye na Nyerere katika dua kubwa iliyofanyika Mnyanjani kijiji kidogo nje ya Tanga kuomba mafanikio.
Amos Kisenge kakumbukwa na taifa hili kwa mchango wake katika kupigania uhuru wa Tanganyika na katunukiwa barabara.