Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, ambaye pia ni Mfadhili wa zamani wa Bendi ya FM ACADEMIA, Pedeshee Amos Makalla mkazi wa Mvomero, Morogoro, ametamka hadharani kwamba tangu enzi na enzi CCM haijawahi kuiba kura, Kama haitoshi amemshutumu Tundu Lissu kwamba aache kutisha na kupotosha Wananchi
Habari kamili hii hapa
---
Your browser is not able to display this video.
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla amesema chama hicho hakijawahi kuwaza wala kufikiria kuiba kura wakati wa uchaguzi.
Makalla amemuonya Makamu Mwenyekiti wa Chadema-Bara, Tundu Lissu kuacha kuwatisha Watanzania kwa lugha za kichochezi.
Mwenezi huyo amesema hayo leo Jumanne, Juni 4, 2024 katika mkutano wa hadhara uliofanyika Bomang'ombe, Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro.
Makalla yupo katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Dk Emmanuel Nchimbi ya kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi na kuangazia maandalizi ya uchaguzi ujao wa serikali za mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025.
Ukiwa kama Mtanzania unayeona Chaguzi za Nchi hii pamoja na ule 2015 na ile ofisi ya Masaki iliyokuwa chini ya Mzee Kinana, na ule wa 2020 ambao ulisimamiwa na Dkt Mahera na Dar es Salaam ikiwa na RPC aliyeitwa Lazaro Mambosasa, TOA MAONI YAKO
CCM haijawahi kuiba kura kwa sababu hata yale mabegi yaliyokamatwa na karatasi zenye kura za Gwajima kule Ubongo, hazikuwa kura walizoiba CCM bali aliiba shetani akampa mgombea wa CCM.
Alaaniwe mtu yule anayetetea na kuulinda uovu. Lakini asemehewe na atakaswe yule azijutiaye dhambi zake hata kama ni nyekundu kama damu