LGE2024 Amos Makalla ajiandikisha kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mikocheni

LGE2024 Amos Makalla ajiandikisha kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mikocheni

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Katibu wa NEC-Itikadi Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Amos Makalla, leo Oktoba 16 ameshiriki zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la wakaazi kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Zoezi hilo limefanyika katika Ofisi ya Serikali za Mitaa TPDC, Kata ya Mikocheni, Wilaya ya Kinondoni, Mkoa wa Dar es Salaam.

1729073639018.png

Akizungumza na wakazi wa mtaa wa TPDC Mikocheni mara baada ya kujiandikisha, Makalla alisisitiza umuhimu wa kushiriki katika zoezi hili la kijiandikisha, akibainisha kuwa ni haki ya msingi kwa kila raia. Alieleza furaha yake kwa kutimiza jukumu hilo muhimu la uraia na kuonyesha kuridhishwa na utaratibu mzuri uliowekwa kwa ajili ya zoezi hilo.

“Ni jambo muhimu sana kujitokeza na kujiandikisha, kwani ndilo linaloweka msingi wa maendeleo ya wananchi wetu,” alisema Makalla. Aidha, aliwasihi Watanzania wote, bila kujali tofauti za kiitikadi, kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika zoezi hilo muhimu.

Makalla pia aliongeza kuwa CCM inaridhika na jinsi zoezi la uandikishaji linavyoendelea kote nchini, na alieleza matumaini kwamba wananchi wataitikia wito huo kwa wingi.

Soma, Pia:

+ Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni muhimu, tukajiandikishe
+ Special Thread: Hali ya Vituo vya Kujiandikisha kupiga Kura Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 kwa Picha na Video
 
Back
Top Bottom