Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
Nimeshangazwa na kitendo cha mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam mheshimiwa Amos Makalla kutumia kodi za walalahoi kukodi ndege ya kuwapeleka wamachinga na wadau wengine nchini Rwanda eti kujifunza usafi.
Inamaana Watanzania wenyewe ni wachafu na hawawezi kujifunza usafi mpaka waende kufunzwa na wanyarwanda. Hii si aibu ya mwaka huu mpya wa 2023? Je lile somo lililokuwa linatufunza usafi shuleni halifundishwi tena madarasani?
Ina maana watanzania tumekuwa watu wa kuiga kila kitu kutoka kwa wenzetu hata vile ambavyo tunaweza kuvifanya wenyewe tunashindwa kuvifanya kwa kusubiri kwanza tujifunze kupitia kwa wengine.
Katika hili Makalla amechemsha sana na kuleta aibu kubwa kwa wana Dar es salaam. Hii ni sawa na kumwambia jirani yako amfunze mkeo namna ya kuoga na wakati wewe mumewe unao uwezo huo na dhamana ya kumsimamia mkeo katika hilo.
Mambo ya aibu namna hii ndo yanayosababisha wengi tushindwe kurudi nyumban sasa hivi.