Pre GE2025 Amos Makalla amjibu aliyekuwa DC Longindo, adai kama alienda Maporini labda alienda Kuchimba Dawa, hakutumwa na Serikali

Pre GE2025 Amos Makalla amjibu aliyekuwa DC Longindo, adai kama alienda Maporini labda alienda Kuchimba Dawa, hakutumwa na Serikali

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Amos Makalla amesema kwamba ccm haitegemei Kubebwa, haina haja ya kuteka watu na kuwatupa maporini ili kupata ushindi

Na kwamba kauli za aliyekuwa DC wa Longindo anaijua mwenyewe, huenda aliishiwa Hotuba na kuamua kuzungumza porojo zake mwenyewe

Makala amedai kwamba huyo DC kama alienda Maporini basi labda alienda kuchimba dawa.

==
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimejitenga na kauli ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido (DC) mkoani Arusha, Marco Ng’umbi kikisema hakihitaji kubebwa ili kishinde katika chaguzi mbalimbali ukiwemo wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji.

Septemba 1, 2024 kulisambaa kipande cha video mitandaoni inayomwonyesha Ngu'mbi akizungumza mambo kadhaa kuhusu uchaguzi wa mwaka 2020.

Soma: Kuelekea 2025 - DC Longido: Mazingira ya 2020 na yale yaliyofanyika kwenye mapori yalitengenezwa na serikali ili tupite bila kupingwa!

Katika picha hiyo jongefu ya dakika 1.32, Ng’umbi anasikika akiwaeleza watu aliowataja mara kadhaa kuwa ni madiwani kwamba ushindi wao katika uchaguzi huo si ujanja wao, bali ni nguvu ya Serikali.
https://www.jamiiforums.com/safari-...do-ilivyotonesha-kidonda-cha-uchaguzi-4747650
Alikwenda mbali zaidi na kueleza hata waliopita bila kupingwa ni kazi iliyofanywa na Serikali na sio ubora wa wagombea husika.

“Kama kuna mtu ambaye si mwoga ni mimi, wote hapa madiwani mwaka 2020 hayupo diwani aliyepiga kampeni hapa. Sasa yale mazingira ya mwaka 2020 si kwamba yalikuja yenyewe moja kwa moja kwa sababu ninyi mlikuwa wagombea bora sana.”

Pia soma: Kuelekea 2025 - DC wa Longido aliyesema alihusika kutengeneza mazingira ya Madiwani kushinda 2020 atenguliwa

Lakini leo Jumatano Septemba 4, 2024 akizungumza na viongozi wa CCM na Serikali wa Mkoa wa Arusha katika kikao cha ndani, Makalla amesema CCM haiwezi kubebwa na hakitegemei mbeleko katika chaguzi, akisema wanakwenda kinyume na kauli ya Ngu'mbi kuhusu uchaguzi.

"Alisema sijui machakani, mi nasema yule aliishiwa hotuba, akaanza kutafuta maneno yake siye (CCM) hayatuhusu na hizo ni habari zake, yaani ilikuwa mazungumzo badala ya habari.”

"Hotuba ilimuishia aliyozungumza hayahusiani na CCM, ndiyo maana tunawataka viongozi wapangilie hotuba zao kwa kuandika vizuri siyo kutengeneza sinema, eti ulikwenda maporini kufanya nini? amesema na kuhoji Makalla.

Makalla amesema CCM haiwezi kwenda porini bali Ngu'mbi alikwenda peke yake iwe kuchimba dawa au kufanya shughuli nyingine.

"Mimi ndiyo msemaji wa CCM, tunawahakikishia Watanzania, chama hiki kimejiandaa kwa uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani na tutashinda, hatuwezi kwenda porini kuzurura kwa sababu tuna muundo mzuri kuanzia ngazi ya kata na tuna Ilani nzuri, hatuhitaji mbeleko," amesema Makalla.

Mwenezi huyo, ameanza ziara ya kikazi ya siku sita katika mikoa ya Arusha na Manyara akisema ina lengo la kutembelea wilaya ambazo hazikufikiwa katika ziara ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Emmanuel Nchimbi.

Chanzo: Mwananchi
 
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Amos Makalla amesema kwamba ccm haitegemei Kubebwa, haina haja ya kuteka watu na kuwatupa maporini ili kupata ushindi

Na kwamba kauli za aliyekuwa DC wa Longindo anaijua mwenyewe na kwamba huenda aliishiwa Hotuba na kuamua kuzungumza porojo zake mwenyewe

Makala amedai kwamba huyo DC kama alienda Maporini basi labda alienda kuchimba dawa.

View attachment 3087022
Damage control!
Too late.
 
Kama
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Amos Makalla amesema kwamba ccm haitegemei Kubebwa, haina haja ya kuteka watu na kuwatupa maporini ili kupata ushindi

Na kwamba kauli za aliyekuwa DC wa Longindo anaijua mwenyewe, huenda aliishiwa Hotuba na kuamua kuzungumza porojo zake mwenyewe

Makala amedai kwamba huyo DC kama alienda Maporini basi labda alienda kuchimba dawa.

View attachment 3087022
Hayo ndo majibu kwenye jambo zito namna hiyo basi Makalla hana Akili!!

Kwahiyo Rais Samia kamfukuza kazi Kwa kuchimba dawa maporini??
 
Kama Hayo ndo majibu kwenye jambo zito namna hiyo basi Makalla hana Akili!!

Kwahiyo Rais Samia kamfukuza kazi Kwa kuchimba dawa maporini
 
Kumekucha 😂

Kwani DC alizungumzia kuteka? 🐼
Alipaswa kusema labda hakutumwa na CCM

Lakini hakuna hata mwenda wazimu anaetarajia Amos Makala angekiri kuwa huo uliosemwa ndio ukweli, na itakuwa ni wendawazimu kwa Amos Makala kututarajia sisi tumtarajie yeye akisema walichosema Henry na Nape ni ukweli!
 
Kama

Hayo ndo majibu kwenye jambo zito namna hiyo basi Makalla hana Akili!!

Kwahiyo Rais Samia kamfukuza kazi Kwa kuchimba dawa maporini??
Amesema huko porini anajua akichokwenda kufanya....

Ajuaye ni yeye ..ndio maana akatoa mfano huo wa "kuchimba dawa"...
 
Alipaswa kusema labda hakutumwa na CCM

Lakini hakuna hata mwenda wazimu anaetarajia Amos Makala angekiri kuwa huo uliosemwa ndio ukweli, na itakuwa ni wendawazimu kwa Amos Makala kututarajia sisi tumtarajie yeye akisema walichosema Henry na Nape ni ukweli!
Kama ndivyo...

Basi ukweli utapatikana mahakamani kwa kuwa ninyi hamuwaamini wanasiasa....
 
Back
Top Bottom