Pre GE2025 Amos Makalla amjibu aliyekuwa DC Longindo, adai kama alienda Maporini labda alienda Kuchimba Dawa, hakutumwa na Serikali

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ndo kilicho mleta Arusha?
Watanzania sio nyumbu. Ni kitu kilicho fanyika na walio fanya ndio wanao sema.
Mbona hamtaki ukweli?
Vipi wale alio wataja Mh. Mbowe na namba zao za simu? Na hilo kataeni. Mna jaribu kukimbia kivuli chenu wenyewe. Ila Mungu wa mbinguni ata waacha uchi.
 
Bila shaka kaletwa na hicho
 
Makala bora angenyamaza ,kwa hiyo Mh rais kakosea ?kwamba ukienda kuchimba dawa ni kosa? Rais ana taasis ajakurupuka kumtengua ,kwa hiyo Makala anaona Mh rais kakosea kumtengua? Pedeshee makala akijibu kipedeshee
 
Kwani Makala alikuwa nani kipindi hicho?
 
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla amesema chama hicho hakitegemei kubebwa ili kushinda kwenye chaguzi.

Mbali na hilo, Makalla amesema, kilichosemwa na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido (DC), Marco Ng’umbi ni maoni yake mwenyewe.

Septemba mosi, 2024, katika mitandao ya kijamii kulisambaa picha jongefu ya dakika 1.32, ikimwonesha Ng’umbi akiwaeleza watu aliowataja mara kadhaa kuwa ni madiwani kwamba ushindi wao katika uchaguzi huo si ujanja wao, bali ni nguvu ya Serikali.

Alieleza hata waliopita bila kupingwa ni kazi iliyofanywa na Serikali na sio ubora wa wagombea husika.

Jioni ya siku hiyohiyo, Rais Samia Suluhu Hassan alitangaza kutengua uteuzi wake na Septemba 2, 2024 alimteua Salum Kali kuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido. Kabla ya uteuzi huo, Kali alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigoma.
 
Makala amedai kwamba huyo DC kama alienda Maporini basi labda alienda kuchimba dawa.

Hakika chama dola kongwe kina tudharau sana waTanzania na kutuona hatuna akili ya kubaini mambo hadi katibu mwenezi, propaganda, itikadi na elimu wa CCM aje kututafunia maneno ya yule muovu waliyemtumia 2019, 2020 na ambaye amèshamaliza mchezo wa 2024 na 2025


View: https://m.youtube.com/watch?v=N6oT1Ykg6D0
 
Kitanda hakizai haramu, mbona muna mkana mtoto wenu?! Nani alimuajiri, Mungu anazidi kuwaumbua na bado, yajayo yanafurahisha.....
 
Hizo ndizo kanuni Duniani pote, ukilikoroga unalinywa peke yako na upojichunga unajikuta ndotoni ukiwa pori la mabwe pande
 
Nyerere - ''Mtu mwenye akili akikuambia neno la kijinga kwamba..." mwisho wa nukuu. Kuwa DC wa Loliondo ... na hafai kuchukuliwa hatua za kufunguliwa mashtaka kwa kuleta taharuki inayopelekea kuvuruga mchakato wa kuelekea uchaguzi wa 2024 na ule wa 2025 .... basi mtu huyo Makala Amos ni wa kupuuzwa... kwa kumtetea DC wa Loliondo.

 
Sawa, kwahiyo DC alikuwa anatoroka kituo chake cha kazi pasi mwajiri kujua na kwenda kufanya mambo yake huko porini?
 
Hamwezi kuishinda CHADEMA kwenye sanduku la kura, hili halipo aminia, siku inakuja....
 
Kama ndivyo...

Basi ukweli utapatikana mahakamani kwa kuwa ninyi hamuwaamini wanasiasa....

..ukweli utapatikana ikiundwa Tume ya Uchunguzi kama aliyounda Raisi Kikwete na kuongozwa na Jaji Musa Kipenka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…