Pre GE2025 Amos Makalla amjibu aliyekuwa DC Longindo, adai kama alienda Maporini labda alienda Kuchimba Dawa, hakutumwa na Serikali

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Huyo aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Longido achukue tahadhari zote. Wanasema ukiwa mchawi halafu ukaweka wazi mambo ambayo wachawi huwa mnafanya kwa watu wasio wachawi, adhabu yako ni kifo.

Mtu yeyote ambaye ni mwovu na anaendelea kukiri kuwa ni mwovu, lazima huyo mtu anaufurahia uovu wake, na ana nia ya kuendelea na uovu wake.

Makala, bila shaka ni mwovu mwente dhamira ya kuulinda na kuuendeleza uovu wake ndiyo maana anaendelea kutoa kauli za kipuuzi kuulinda ushetani ambao CCM huwa inafanya.

Ilaaniwe CCM na maharamia wote wa CCM ambao wameamya kuwa wafuasi wa shetani maisha yao yote. Hongera kwao wanaCCM wanaouchukia uovu unaofanywa na wanaCCM mashetani, ambao hawaufurahii ushetani huo, Mh. Jaji Warioba, Butiku, Shivji, Ndugulile, ni mfano mzuri wa wanaCCM ambao hawafurahii uwepo wa mashetani ndani ya CCM, lakini kwa bahati mbaya mashetani yana mizizi ndani ya CCM kiasi kwamba huwezi kuyang'oa bila ya kuing'oa CCM nzima.
 
Angesema nini zaidi kuficha aibu ya kuvuliwa nguo hadharani?
 
Huwa nashangaa sana watu wanaandika "CPA Makalla atema cheche jukwaani".

Ni wakati umefika sasa hivi vyeo vya Dr, CPA, Eng, Prof vitumike kwenye taalum a husika sio kwa wanasiasa kama hawa.
 
Asitufanyie comedy huyu mtu.. DC alishaweka kila kitu hadharani😂
 
Shida ni kua hao ccm wanatofautiana kimaslahi.
Kuna watu kama huyo DC wameingizwa kwenye michakato ya kufanya rafu ili chama kishike dola lakini wao malengo yao ni hapohapo wilayani kwao..
Hawana habari na nchi wala kimataifa, wao wakifanikisha jambo kwa wilaya yao kwa 100% basi wanaamini ni wakubwa na wakubwa wa nchi wapo upande wao kwa lolote watakalosema maana wamecheza rafu ili kuimarisha chama na wakuu wao wamebariki uhalifu wao.

Lakini ubaya ni kua wakuu wao wana malengo tofauti kidogo na ukubwa tofauti, hawaoni shida kuwatupa lupango, hawaoni shida kuwakana hata kuwapoteza presha ikiwa kubwa.
Hawa wanatumiwa na watatumiwa mpaka mwisho wa maisha yao kama hawatabadirika basi sidhani kama watakua na mwisho mzuri.
 
Wanatuona Sisi mafala.Sawa Amosi
 
Mpaka mawe yatasema
 
Makalla ametoa kauli nyepesi na ya kijinga. Lakini hatukutarajia yeye au chama cha ccm kwa ujumla wake waje na kauli yenye mashiko baada ya kauli za DC Loliondo au kauli ya Nape. Kwa hiyo kauli yake haishangazi kabisa.
Kilichonishgaza toka awali ni vyama vingine makini kabisa kukubali kuingia katika uchaguzi wa 2025 kukiwa na mazingira yale yale ya uchaguzi wa 2020...,tume ya uchaguzi ni ile ile na katika muundo ule ule, na katiba ni ile ile...ambapo neno la rais ambaye ni mwenyekiti wa chama tawala linakuwa amri inayopanda juu ya sheria,..na matangazo yatakayosemwa na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi bila kujali ukweli wake ,ni matakatifu kiasi cha kutohojiwa na mahakama yoyote.

Katika mazingira hayo vyama makini vinatarajia nini? Maendeleo ya nchi yoyote kijamii na kiuchumi yanaanzia na uchaguzi katika uwanja ulio sawa,siyo uwanja ulioinama.
Nini kilifanya vyama makini vikubali kuingia katika mtego ule ule?

Kuna kichekesho kimoja,kuna watu wamempongeza rais kwa kumuondoa DC wa Longido...,yaani kana kwamba kamuondoa kwa vile yale aliyoyafanya huko wakati wa uchaguzi 2020 na yale aliyopanga kuyafanya tena kwa mujibu wa maelezo yake,..eti ni yake binafsi.

Inaonesha wazi kilichofanyika Longido 2020,kilifanyika pia maeneo mengine ya uchaguzi na ndo maana matukio na matokeo yakawa yamefanana.
Na ndo maana tuliona wazi yule askari wa wilaya ya Hai akimuambia Mbowe asidanganye watu kwa vile hatashinda uchaguzi hata iweje.
Na hilo lina maanisha kwamba ma-DC,ma-RC, na polisi wilaya na mikoa,wote walishiriki kufanya aliyoyasema DC wa Longido.
Rais Samia atamuondoa DC wa Longido na kumteua mwingine ambaye atakaa kimya,hatoropoka kama mwenzie aliyeondolewa lakini kwa hali ilivyo atafanya yale yale au tuseme atamalizia pale mwenzie alipoishia...kwa vile alishasema kwamba hata sasa wameshaanza mchakato wa uchaguzi ujao ili wafanye yaleyale.
 
Kumekucha 😂

Kwani DC alizungumzia kuteka? 🐼
Alizungumzia habari ya mapori sasa ni vyema umtafute kupitia jukwaa atuambie kama maporini alikoenda kulikuwa na nini alifuta nini,je alipeleka fomu au akikuwa akisaka yule mnyama mlafi wa madoa doa?Kwani wapo wanaouliza ni lini fomu zinarudi.
 
DC Ng'umbi!
Kama huyo jamaa ni Msukuma najaribu kuchambua uhalisia wa nomino ya jina lake hilo la kilugha!

Nomino hiyo ina maana mbili:
1-Ng'umbi(tumbo-abdomen-stomach).

2-Nghumbi(panzi-grasshopper).

Kama jina lake linamaanisha #1 tumbo, basu limesadifu neno 'mchumia tumbo'.

Na kama jina lake lina maana ya #2 panzi
basi jina lake limesadifu kichwa chake upara, maana panzi hana nywele.

Tujitahidi kuwachagulia watoto wetu majina mema, maana jina linaweza kukamata matendo na mustakabalii wa mtu.
 
Hawa ndo wamepewa dhamana kuijenga nchi!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…