Amos Makalla amewataka CHADEMA wamalize migogoro ndani ya chama chao na wasiwahadae Watanzania kwa kuwasingizia TAMISEMI, na kuwalaumu Chama cha Mapinduzi (CCM) bali wajilaumu wao wenyewe, wasifiche mgogoro na mpasuko mkubwa uliowafanya wakose maandalizi yakutosha.
Aidha, ameongeza kuwa "Chochote watakacho sema leo ni kuficha ukweli juu ya matatizo waliyonayo juu ya maandalizi mabovu, hakuna jambo lingine. Tutegemee hadaha, upotoshaji na uongo na utengenezaji wa propaganda ili kuwatuliza wanachama wao lakini wakificha matatizo yao. Ila ninachojua kuanzia tarehe 1, mgogoro utaendelea kuwa mkubwa katika nafasi wanazoenda kugombea ndani ya chama chao"
Pia, Soma: