Amos Makalla: NDC karibu Arusha, nawahakikishia usalama

Amos Makalla: NDC karibu Arusha, nawahakikishia usalama

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Makalla, amewakaribisha wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na maafisa mbalimbali kutoka nchi 16 za Afrika na nje ya Afrika walioko kwenye ziara ya mafunzo ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC).

Makalla amewahakikishia usalama na utulivu kwa muda wote wa siku tano watakazokuwa kwenye mafunzo mkoani Arusha.

Kauli hiyo ameitoa leo, Novemba 10, 2025, alipokuwa akiwakaribisha maafisa 72 kutoka nchi mbalimbali, ikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Zimbabwe, Afrika Kusini, Malawi, na Bangladesh.

"Mkoa wa Arusha ni kituo cha utalii kwa Kanda ya Kaskazini. Niwakaribishe sana na mjisikie mpo nyumbani. Arusha inaendelea vyema katika sekta ya utalii na sekta nyingine za kiuchumi, na imeendelea kuwa salama na tulivu kutokana na ushirikiano mkubwa kati ya wananchi na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama," amesema RC Makalla.

Screenshot 2025-11-10 172844.png
 
Back
Top Bottom