abdulatif himid
JF-Expert Member
- Dec 23, 2011
- 326
- 814
Imebaki miezi tu kufika uchaguzi Mkuu,Ajenda kubwa ya CDM ni Katiba Mpya!
CCM ipo kazini,Nchi inajengwa na Wananchi wanaona!
Leo hii,tunajenga Morogoro na Biashara tunafanya DSM!
Tunasafiri Dar mpaka Dom unaenda na kurudi bila uchovu wowote.
Na project inaendelea kuunganisha Nchi nzima na Nchi za Jirani na Treni ya Umeme!
Daraja la Kigongo Busisi limekamilika bado uzinduzi tu.
Bwawa la Umeme limefikia zaidi ya Asilimia 90%.
Maji na umeme vijijini usambazaji wake unakwenda kwa Kasi.
Miundombinu ya Barabara inazidi kuboreshwa.
Watu wanafanya Biashara zao kwa Amani na wanapata faida!
Kariakoo inajengwa kwa Kasi,Kila mtaa kunaota maghorofa mapya!
Hii ni KAZI kubwa ya Chama Cha Mapinduzi!
CDM kama kweli mnataka Ushindi,fanyeni Utafiti na mjue Wananchi huku chini wanataka kitu Gani.
CCM imeongoza Nchi hii kwa Miaka zaidi ya 60,ikianza kama Tanu!
KAZI waliyoifanya kwa Miaka yote hiyo haiwezi kubezwa kwa maneno matupu!
Kama MABADILIKO,wote tunayataka lakini kwa Ajenda zipi?
Kenya Kila siku wanabadilisha vyama,Je Kuna nini kipya?
Zambia wanabadilisha vyama,Je Kuna nini kipya?
Nigeria wanabadilisha vyama,Je Kuna nini kipya?
Malawi wanabadilisha vyama,Je Kuna nini kipya?
Sisi Tanzania tukibadilisha Chama,Tukawaondoa CCM tuwaweke CDM watafanya jipya Gani?
Kama ni Katiba Mpya hata CCM wanaweza wakaileta tu!
Chadema ije na Ajenda mahsusi ya Uchaguzi,Wananchi wa Kawaida ambao wanajitegemea kwa jasho lao hawaishi kwa ajili ya Katiba!
Tunataka kusikia,Huduma za matibabu zitakuwa Bure chini ya Utawala wenu,Elimu Bure iwe Bure kweli,Mishahara ya Watumishi wa Umma itaongezwa kwa Asilimia ngapi!
Sera yenu kimataifa itakuwaje na Jinsi Gani mtakavyokusanya Kodi Ili kufanikisha yote hayo!
Kuibeza CCM ni sawa na kujitekenya na kucheka mwenyewe.
CCM imefanya kazi ya kutukuka na kupigiwa mfano sana.
Nchi yetu ni Kubwa na Ina watu wengi,wenye makabila tofauti lakini pamoja na hayo maendeleo tunayaona na Amani,Utulivu,Umoja na mshikamano upo miongoni mwa watu.
Kwangu Mimi CCM ikishinda,ni Inastahili kushinda na si Vinginevyo.