PreGE2025 Amos Makalla: Rais Samia ametuhakikishia Tanzania ni salama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
843
Reaction score
1,024
•Nchi yetu ni salama, mipaka yetu ni salama chini ya uongozi wa Dr Samia

Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla amesema kuwa hali ya usalama Tanzania ipo shwari chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye Amiri Jeshi Mkuu.

Makalla ameeleza hayo leo akiwasalimu wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Nanyamba mkoani Mtwara akiwa njiani kuelekea Wilaya ya Tandahimba, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku 10 mkoa wa Lindi na Mtwara.

Makalla ameeleza kuwa katika mipaka ya Tanzania ni salama na amepita Nanyamba kuelekea Tandahimba ameona hali ya nchi ni salama na ili maendeleo yapatikane lazima kuwe na amani na utulivu na katika hilo Rais Samia ameifanya kazi hiyo vizuri sana.

“Dk Samia Suluhu Hassan ndiye amiri jeshi wetu Mkuu na yeye bado ametuhakikishia Tanzania ni salama na mimi nashuhudia napita katika mipaka yetu hii tunatoka Nanyamba tunaenda Tandahimba, Newala mpaka Masasi Tanzania ni salama wananchi wetu wanapenda amani na utulivu,” amesema Makalla.

Ameongeza kwa kuwataka wananchi waendelee kushirikiana na serikali na wayalinde mapinduzi na maendeleo yaliyofanyika kwa wivu mkubwa hususani mapinduzi yaliyofanyika katika zao la korosho yalindwe.

20250415_153956.jpg

20250415_153954.jpg

20250415_153949.jpg
 
View attachment 3305191

View attachment 3305192

View attachment 3305194
Salama gani wakati wananchi wanatekwa na kuuwawa,cdf alisema watu wa nhi jirani wamejipenyeza serikalini?
 
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM CPA. Amos Makalla, amewahakikishia na kuwatoa hofu wakazi wa Mikoa ya Kusini kuwa mipaka ya Tanzania ni salama chini ya Amiri jeshi Mkuu Dkt. Samia Suluhu Hassan hivyo waendelee kuchapa kazi na kujiletea maendeleo pasi na shaka.

CPA. Amos Makalla ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na mamima ya wakazi wa Halmashauri za Nanyamba pamoja na Tandahimba, mkoani Mtwara, kwenye siku ya pili ya ziara yake mkoani Mtwara, baada kumaliza ziara ya Mkoa wa Lindi.
 
Kwa Sasa Tanzania hakuna amani maana watu wanatekwa Kila siku.Kwa Sasa Nchi ilikofikia Kwa uvunjifu wa amani ni Bora zaidi kwenda kuishi Gaza kuliko Tanzania
 
Kuna watu kweli ni wagonjwa wa akili. Watu qanatekwa, wanauawa, wanapotezwa,wanabambikiziwa keai, halafu jitu linasema hiyo ni amani!!

Kuna matatizo makubwa CCM!! Wagonjwa wa akli waliotakiwa kusaidiwa matibabu Milembe, inawapa uongozi wa chama!!
 
Back
Top Bottom