The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla, amesema kuwa uchaguzi utafanyika hata bila ushiriki wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwani vyama vingine vingi vimeshajipanga kushiriki.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara mkoani Iringa Machi 28, 2025 , Makalla amesema kuwa CCM inaingia kwenye uchaguzi kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku akishangazwa na msimamo wa CHADEMA wa kususia uchaguzi bila katiba mpya, Makalla ameeleza kuwa tayari wanavunja Katiba iliyopo kwa kukataa kushiriki uchaguzi.
"CCM ni chama kikubwa, kinapenda demokrasia na kinaheshimu Katiba ya nchi. Wameamua wao kususia uchaguzi, hatuwalazimishi, lakini vyama vingine vitashiriki na uchaguzi utafanyika bila wao," alisema Makalla.
Ameeleza kuwa ndani ya CHADEMA kuna mvutano mkubwa kati ya viongozi na wanachama, ambapo wengi wao wanapigania nafasi za udiwani na viti maalum. Hata hivyo, uongozi wa chama hicho ulitoa tangazo la kufanyika kwa kikao tarehe 3 Aprili, 2025 kabla ya kuahirisha mkutano, jambo ambalo Makalla anadai lililenga tu kutikisa CCM ili waitwe kwenye mazungumzo.
"Baada ya kuona tumewapotezea, sasa wamesema watatoa msimamo wa chama kuhusu watia nia. Wamefungwa ndani ya chama chao, lakini vyama viko vingi. Wanaotaka kugombea waende kwenye vyama vingine," aliongeza.
Makalla pia amesema kuwa ndani ya CHADEMA hakuna nafasi ya mgombea urais kwani hakuna anayewaza kushindana na Rais Samia Suluhu Hassan ambapo amewataka vijana na wanawake wa CHADEMA wenye nia ya kugombea kuhamia vyama vingine ili kutimiza ndoto zao za kisiasa.
Kuhusu uandikishaji wa wapiga kura, Makalla amesema kuwa viongozi wa CHADEMA waliwakataza wanachama wao kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, hatua ambayo itawapelekea kukosa ushindi katika uchaguzi mkuu.
"Msije kutupigia kelele mkishindwa kwa sababu hamkujiandikisha. Sisi (CCM) tumehamasisha watu na wamejiandikisha, hivyo tunategemea ushindi wa kishindo," alisema Makalla na kuongeza
"Leo mkianza kusema mmefanya maamuzi ya kushiriki uchaguzi, mkishindwa msilalamike. Watu wenu mliwaambia wasijiandikishe