TANZIA Amos Nnko, Mkurugenzi ofisi ya Msajili wa Hazina, bintiye wafariki ajalini Same

Tuliwahi kuanguka na basi maeneo hayo hayo tukitokea Morogoro wakafa watu wawili. Pako tambarare kama mezani lakini pana mambo yake. Baada ya ajali mtaona vijana kibao wanakuja nakujifanya kuwapa fedha kumbe ndio wananunua watu hivyo! Dunia hii kubwa.
 
Maisha hayana maana kama wasemavyo wanautamaushi, amesoma, amepata hela, ana familia yake safi, kanunua gari ambalo leo linamuua, kila binadamu ana kitabu cheke anakifungua kwa furaha na ipo siku utakifunga kwa huzuni na kuwaachia wengine wasome.

Kwahiyo tujitahidi vitabu vyetu viwe vizuri kwa wasomaji pindi vifungapo kurasa ya mwisho.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE, AMEN
 
Hicho kipande cha Same, Hedaru , Makanya kote huko natembea na 140 mpk 180 and sometimes nakopa 180+... know your car limitations..

Gari ikiwa imetaga (Ground clearance ni ndogo) upepo hauwezi kukuhamisha, ila likiwa juu (Ground Clearance kubwa) lazima ikutoe, hapa sasa inategemea na weight x speed x direction ya upepo..

Tukirud ktk dhana ya Aerodynamics kuna namna ya kufanya chombo kipae ni kwenda against wind.. sasa kiuhalisia upepo unaokatiza huwa hauna shida, shida inakuja pale unapopishana na gari nyingine inayokuja kasi, inagenerate upepo ambao unakutana nao wewe head to head hivyo inatengeneza lifting mechanism bahati mbaya ikishalift gari kwa kiwango flan unakutana na upepo unaokatisha (Cross wind) ambao utakusogeza either kulia or kushoto hapo sasa ndio unakuta mtu anatoka nje ya barabara au anajaa upande ambao sio wake..

Trick: Kimbia uwezavyo ila ikifikia unapishana na gari nyingine punguza mwendo mpk apite ndio uendelee na flat-foot..
Nimekula sana wali maharage Engineering Cafteria pale.
 
Ni kweli wabongo wengi wanaendesha vibaya sana magari.
Yaani huwaambii kitu 👌👌
Mwendokasi balaa.
Sijui wana matatizo gani?!
Yaani utasema ni Watu hawana cha kupoteza , wana-bet for life 🤔🤔🤔

overtaking za hatari hawajali wala nini.
Always huwa nasema Mwenyezi aendelee kutunusuru na tuepuke mwendokasi ili akitokea wa kutaka kutusababishia Basi kufa na afe mwenyewe au wenyewe.

Hawataki kufuata sheria na hekima za jinsi ya kuendesha gari kiusalama kwa masafa marefu.
Inasikitisha mno lakini mwisho wa siku mchuma janga atakula na wakwao.
Tujitafakali kwa kweli.
Hulka mbaya sana ya kuzoea na kupenda mwendokasi.
Kabisa Mkuu
 
Hicho kipande cha Same, Hedaru , Makanya kote huko natembea na 140 mpk 180 and sometimes nakopa 180+... know your car limitations..

Gari ikiwa imetaga (Ground clearance ni ndogo) upepo hauwezi kukuhamisha, ila likiwa juu (Ground Clearance kubwa) lazima ikutoe, hapa sasa inategemea na weight x speed x direction ya upepo..

Tukirud ktk dhana ya Aerodynamics kuna namna ya kufanya chombo kipae ni kwenda against wind.. sasa kiuhalisia upepo unaokatiza huwa hauna shida, shida inakuja pale unapopishana na gari nyingine inayokuja kasi, inagenerate upepo ambao unakutana nao wewe head to head hivyo inatengeneza lifting mechanism bahati mbaya ikishalift gari kwa kiwango flan unakutana na upepo unaokatisha (Cross wind) ambao utakusogeza either kulia or kushoto hapo sasa ndio unakuta mtu anatoka nje ya barabara au anajaa upande ambao sio wake..

Trick: Kimbia uwezavyo ila ikifikia unapishana na gari nyingine punguza mwendo mpk apite ndio uendelee na flat-foot..
Utundu wa magari ni sayansi na sanaa, watu wengi wanajua ni kulenga bara bara tu kumbe ni zaidi sana ya hapo.
 
Ajali zinazotokea msimu wa sikukuu zimeendelea kuacha majonzi kwa Watanzania, baada ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu ofisi ya Msajili wa Hazina, Amos Nnko kufariki dunia.
Nnko amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Same, mkoani Kilimanjaro, jana mchana Jumapili, Desemba 22, 2024. Katika ajali hiyo, pia binti yake wa kwanza, Maureen Nnko amefariki.

Hayo yamethibitishwa na Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu leo Jumatatu Desemba 23, 2024 kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Katika taarifa hiyo, imeelezwa kuwa mke wa marehemu, Agnes Nnko na watoto-- Marilyn, Melvin na pamoja na mwanafamilia mwingine, Sylvana wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya KCMC na Mawenzi.

View attachment 3183528

“Mipango ya mazishi inaendelea kuratibiwa na familia ya marehemu kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina,” imeeleza taarifa hiyo.

Chama gani tafadhali
 
Kuweka Mayai yote katika KAPU moja si sahihi.. hata safari za ndani ya Mkoa mie naona si sahihi.. ni kheri kusafiri kwa mafungu..

Chanzo cha ajali sijafahamu.. siwez comment chochote.. ingawa kuna baadhi ya watu wanasema kipande kina upepo Mkali, ukiangalia vzr hiyo gari ina kg za kutosha ukiongeza na watu waliokuwemo ndani sijaona upepo wa kuitoa nje ya reli maybe technical issues or human factors..
Huijui ile barabara ........Kuna comment yako moja nimeona umeongea vizur lkn hii umeharibu kwenye hiyo paragraph ya pili
 
Ajali zinazotokea msimu wa sikukuu zimeendelea kuacha majonzi kwa Watanzania, baada ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu ofisi ya Msajili wa Hazina, Amos Nnko kufariki dunia.
Nnko amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Same, mkoani Kilimanjaro, jana mchana Jumapili, Desemba 22, 2024. Katika ajali hiyo, pia binti yake wa kwanza, Maureen Nnko amefariki.

Hayo yamethibitishwa na Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu leo Jumatatu Desemba 23, 2024 kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Katika taarifa hiyo, imeelezwa kuwa mke wa marehemu, Agnes Nnko na watoto-- Marilyn, Melvin na pamoja na mwanafamilia mwingine, Sylvana wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya KCMC na Mawenzi.

View attachment 3183528

“Mipango ya mazishi inaendelea kuratibiwa na familia ya marehemu kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina,” imeeleza taarifa hiyo.

View attachment 3183107R.I.P MTANI!Hii ajali leo nimetaona aya magari nadhani masaa 3 baada ya ajali!nimeyaona yakiwa bado barabarani leo​
 
Kuweka Mayai yote katika KAPU moja si sahihi.. hata safari za ndani ya Mkoa mie naona si sahihi.. ni kheri kusafiri kwa mafungu..

Chanzo cha ajali sijafahamu.. siwez comment chochote.. ingawa kuna baadhi ya watu wanasema kipande kina upepo Mkali, ukiangalia vzr hiyo gari ina kg za kutosha ukiongeza na watu waliokuwemo ndani sijaona upepo wa kuitoa nje ya reli maybe technical issues or human factors..
Unaujua upepo wa same? pale ukiwa unaacha mpaka wa tanga kumeandikwa kilometa ..... zijazo kuna upepo mkali sana, nature ya pale ni semi arid na upande una milima huku kwenye barabara ni mteremko, sasa upepo unaovuma pale ni wa kuhamisha gari kabisa.
 
Inasikitisha sana familia nzima kukutwa na janga kama hili. Poleni sana, Mungu awaweke pema waliotangulia, kuwatibu walio hospitali na kuwapa faraja na subira wanafamilia wote
 
Ajali zinazotokea msimu wa sikukuu zimeendelea kuacha majonzi kwa Watanzania, baada ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu ofisi ya Msajili wa Hazina, Amos Nnko kufariki dunia.

Nnko amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Same, mkoani Kilimanjaro, jana mchana Jumapili, Desemba 22, 2024. Katika ajali hiyo, pia binti yake wa kwanza, Maureen Nnko amefariki.

Hayo yamethibitishwa na Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu leo Jumatatu Desemba 23, 2024 kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Katika taarifa hiyo, imeelezwa kuwa mke wa marehemu, Agnes Nnko na watoto-- Marilyn, Melvin na pamoja na mwanafamilia mwingine, Sylvana wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya KCMC na Mawenzi.

“Mipango ya mazishi inaendelea kuratibiwa na familia ya marehemu kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina,” imeeleza taarifa hiyo.
Hivi kwa nini hii sikukuu inamaliza
Wiki iliyoisha kuna mchungaji wa KKKT alisisitiza sana watu waende makwao wakajumuike na wazazi wao.
Huyo mchungaji ana mission maalum si bure. Mtu ana mji na familia, kwao ni pale alipo. Mahubiri ya kijima.
 
Back
Top Bottom