TANZIA Amos Nnko, Mkurugenzi ofisi ya Msajili wa Hazina, bintiye wafariki ajalini Same

TANZIA Amos Nnko, Mkurugenzi ofisi ya Msajili wa Hazina, bintiye wafariki ajalini Same

Kila siku huwa nasema hapa kusafiri katika barabara za Tanzania ni HATARI na kutembea na KIFO.

Waafrika hasa watanzania bado hawawezi kutumia barabara kwa usalama.

Mijitu inajiendea tu, pakachu pakachu kama mapanya.
Katika Barabara hatari Tanganyika ni kutoka Dar, chalinze,morogoro, kitonga,iringa,mafinga,Makombako, mbeya kwenda Tunduma.

Ninasali ili siku Moja Saa100 apitishwe hiyo Barabara.

Mzee Kinana,alipitia huko mwaka Jana, akachanganyikiwa,akatoa ahadi hewa ya ujenzi wa Barbara nne, akaishia kujiuzulu
 
Kuna watu wanapenda tu kuendesha gari, huwaambii kitu.

Lakini pia wengine hawana uzoefu wa kuendesha masafa na cha ajabu zaidi wanaendesha mida ya usiku.
Yeah.... Udereva ni proffession, ni kazi, tofauti na kuendesha kawaida.

Ukisikia usingizi paki, au kama sio professional jikwekee vituo njiani, kaa hata saa moja, anza tena safari
 
Sawa wanasema kifo hakiepukiki lakini huyu kigogo alikua na machaguo yafuatayo :
1. Kukodi dereva (angempeleka mpaka kijijini )
2.Shule zmefunga muda kidogo angetanguliza watoto
3.Kupanda ndege gari imkute KIA

NB:kwa majukumu na uchovu wa Mkurugenzi kuendesha gari zaid ya KM 600 ni ubinafsi sana kwa family yake!
 
Kuweka Mayai yote katika KAPU moja si sahihi.. hata safari za ndani ya Mkoa mie naona si sahihi.. ni kheri kusafiri kwa mafungu..

Chanzo cha ajali sijafahamu.. siwez comment chochote.. ingawa kuna baadhi ya watu wanasema kipande kina upepo Mkali, ukiangalia vzr hiyo gari ina kg za kutosha ukiongeza na watu waliokuwemo ndani sijaona upepo wa kuitoa nje ya reli maybe technical issues or human factors..
 
Siyo Dereva tu, Bali dereva makini maana hata Marehemu alikuwa Dereva pia, pengine alikuwa makini akasababishiwa ajali na extrenal factors, haya mambo ni magumu na yanatafakarisha sana
Ni sawa kabisa ila niliiona hii twitter ndio maana nikaja na hoja ya kuwa na dereva
Mashuhuda Wanasema Dereva wa Prado ni kama alilala akaifata TATA..
.
Mkuu wa wilaya ya Same anasema madereva waongeze umakini hasa kipindi hiki cha sikukuu..
.
Anaendelea kusema madereva huwa wanajisahau wakiwa barabarani..
.
NI kama anataka kumpiga Mkurugenzi mawe.
 
Hizi highways za mikoani kama Dar- Dom, Dar-Ars, Dar- Mbeya zingekuwa double line zingesaidia sana kupunguza ajali.

Ukienda Europe au nchi zinazoendelea barabara za highways ni double au zaidi ya double yani unakuta line 3 za barabara zinaenda ars na line 3 zinarudi

Ajali nyingi zinasababishwa na wembamba wa barabara unashindwa kukwepa ile ya ghafla ghafla unaishia kula uso kwa uso au kubiringita
 
Ajali zinazotokea msimu wa sikukuu zimeendelea kuacha majonzi kwa Watanzania, baada ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu ofisi ya Msajili wa Hazina, Amos Nnko kufariki dunia.
Nnko amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Same, mkoani Kilimanjaro, jana mchana Jumapili, Desemba 22, 2024. Katika ajali hiyo, pia binti yake wa kwanza, Maureen Nnko amefariki.

Hayo yamethibitishwa na Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu leo Jumatatu Desemba 23, 2024 kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Katika taarifa hiyo, imeelezwa kuwa mke wa marehemu, Agnes Nnko na watoto-- Marilyn, Melvin na pamoja na mwanafamilia mwingine, Sylvana wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya KCMC na Mawenzi.

“Mipango ya mazishi inaendelea kuratibiwa na familia ya marehemu kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina,” imeeleza taarifa hiyo.

RiP
Ingawa ajali haina kinga, ila ni hatari familia nzima kusafiri ndani ya gari moja.
 
Back
Top Bottom