TANZIA Amos Nnko, Mkurugenzi ofisi ya Msajili wa Hazina, bintiye wafariki ajalini Same

TANZIA Amos Nnko, Mkurugenzi ofisi ya Msajili wa Hazina, bintiye wafariki ajalini Same

Mwenyezi Mungu awape pumziko lenye amani.

Ila Wakuu barabarani tuwe wapole na makini sana hasa wale wa magari yenye ving'ora kwenye dashboard.

Nimeshuhudia mara kadhaa wakifanya overtaking kwenye alama ya pundamilia, na kutanua bila sababu za msingi.

Ajali na kifo havitambui vyeo na uchumi wako.

NB: Ushauri hauna uhusiano na tukio kwenye uzi.
 
Hapo hakuna cha baba,mtoto,gari, cheo na mwisho kutaibuka walemavu kutokana na ajali

Umakini unahitajika kupita kiasi kwa kweli!

Kuna wakati mzee Yusuph Makamba,akiwa mkuu wa mkoa wa Dar,alimwambiaga mtu,akaendeshe gari la baba yake,sio la abiria
 
Hii gari imeumia yenyewe tu au imegonga mti ? Kwa anaejua plz atwambie
 
Ajali zinazotokea msimu wa sikukuu zimeendelea kuacha majonzi kwa Watanzania, baada ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu ofisi ya Msajili wa Hazina, Amos Nnko kufariki dunia.
Nnko amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Same, mkoani Kilimanjaro, jana mchana Jumapili, Desemba 22, 2024. Katika ajali hiyo, pia binti yake wa kwanza, Maureen Nnko amefariki.

Hayo yamethibitishwa na Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu leo Jumatatu Desemba 23, 2024 kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Katika taarifa hiyo, imeelezwa kuwa mke wa marehemu, Agnes Nnko na watoto-- Marilyn, Melvin na pamoja na mwanafamilia mwingine, Sylvana wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya KCMC na Mawenzi.

“Mipango ya mazishi inaendelea kuratibiwa na familia ya marehemu kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina,” imeeleza taarifa hiyo.

Chanzo cha ajali ni Nini! Mbona gari imekatika nusu!
 
Kila siku huwa nasema hapa kusafiri katika barabara za Tanzania ni HATARI na kutembea na KIFO.

Waafrika hasa watanzania bado hawawezi kutumia barabara kwa usalama.

Mijitu inajiendea tu, pakachu pakachu kama mapanya.
 
Kama ni mtu wa majukumu sana usiendeshe gari. Majukumu yanaleta uchovu wa akili na kuhamisha mawazo.
Tafuta vijana hapo mjini wakupeleke, halafu unawatoa na laki moja mbili
Kuna watu wanapenda tu kuendesha gari, huwaambii kitu.

Lakini pia wengine hawana uzoefu wa kuendesha masafa na cha ajabu zaidi wanaendesha mida ya usiku.
 
Back
Top Bottom