TANZIA Amos Nnko, Mkurugenzi ofisi ya Msajili wa Hazina, bintiye wafariki ajalini Same

TANZIA Amos Nnko, Mkurugenzi ofisi ya Msajili wa Hazina, bintiye wafariki ajalini Same

Kama ni mtu wa majukumu sana usiendeshe gari. Majukumu yanaleta uchovu wa akili na kuhamisha mawazo.
Tafuta vijana hapo mjini wakupeleke, halafu unawatoa na laki moja mbili
Sahihi na hii ni sababu kubwa, hizi safari ndefu kama huna uzoefu ni hatari...Poleni wafiwa, poleni familia.
 
Kile kipande upepo ni mkali na hatujui sehemu za upepoili utoke salama uendeshe vioo vikiwa cimefungwa au wazi? Na speed ngapi ili gari ipite salama.
Upepo wa pale sio kinzani ni upepo unaokata brbr. Unakuhamisha chap
 
Kama ni mtu wa majukumu sana usiendeshe gari. Majukumu yanaleta uchovu wa akili na kuhamisha mawazo.
Tafuta vijana hapo mjini wakupeleke, halafu unawatoa na laki moja mbili
Usisahau: kila kifo lazima kiwe na sababu, ili kitokee!
 
View attachment 3183106
Ajali zinazotokea msimu wa sikukuu zimeendelea kuacha majonzi kwa Watanzania, baada ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu ofisi ya Msajili wa Hazina, Amos Nnko kufariki dunia.

Nnko amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Same, mkoani Kilimanjaro, jana mchana Jumapili, Desemba 22, 2024. Katika ajali hiyo, pia binti yake wa kwanza, Maureen Nnko amefariki.

Hayo yamethibitishwa na Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu leo Jumatatu Desemba 23, 2024 kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Katika taarifa hiyo, imeelezwa kuwa mke wa marehemu, Agnes Nnko na watoto-- Marilyn, Melvin na pamoja na mwanafamilia mwingine, Sylvana wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya KCMC na Mawenzi.

“Mipango ya mazishi inaendelea kuratibiwa na familia ya marehemu kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina,” imeeleza taarifa hiyo.
View attachment 3183107
Watoto Wana umri Gani? Nimeuliza tu
 
Pumzika kwa Amani Mr Nko, umekuwa Mzee wetu wa usharika KKKT Mbezi Beach kwa muda mrefu sana, Mungu akulipe sawasawa na matendo yako hapa duniani. Mungu awajalie majeruhi nafuu ya mapema
 
Imefika wakati sasa Hilo eneo linalosemekana kuwa na upepo mkali hapo Same dereva anapokaribia Hilo eneo pawekwe barrier kwa ajili ya kuwakumbusha mdereva ambao Siyo wazoefu na jiografia ya Hilo eneo hatari, au vinginevyo pawekwe matuta kadhaa kunusura maisha ya watu
 
Sifa ya kwanza kama unasafiri na familia, hakikisha umelala zaidi ya saa 8, hakikisha spidi hauzidi 100, hakikisha safari unaigawa kwa phases angalau kila baada ya km 70-100 una break dk 15.

Kama unasafiri mwenyewe una drive na uko pwkw yako jilipue hata 360km/hr
 
Back
Top Bottom