TANZIA Amos Nnko, Mkurugenzi ofisi ya Msajili wa Hazina, bintiye wafariki ajalini Same

Ajali zinazotokea msimu wa sikukuu zimeendelea kuacha majonzi kwa Watanzania, baada ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu ofisi ya Msajili wa Hazina, Amos Nnko kufariki dunia.
Nnko amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Same, mkoani Kilimanjaro, jana mchana Jumapili, Desemba 22, 2024. Katika ajali hiyo, pia binti yake wa kwanza, Maureen Nnko amefariki.

Hayo yamethibitishwa na Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu leo Jumatatu Desemba 23, 2024 kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Katika taarifa hiyo, imeelezwa kuwa mke wa marehemu, Agnes Nnko na watoto-- Marilyn, Melvin na pamoja na mwanafamilia mwingine, Sylvana wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya KCMC na Mawenzi.

“Mipango ya mazishi inaendelea kuratibiwa na familia ya marehemu kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina,” imeeleza taarifa hiyo.

R.I.P inaumiza sana, ila hiyo barabara ya Same kuna kitu sio bure( kiroho zaidi)

Kuna familia huwa hazisafiri kwenye usafiri wa pamoja, tujifunze kwenye hili.

Tusafiri kwa mafungu ya wawili wawili au hata mmoja mmoja
 
hii nadharia ina ukakasi japo ndo reality lakini viumbe hai siku zote tupo katika nature ya kujilinda,

leo hii ukipata meli tunatarajia kue na life jackets ili likitokea lolote watu waweze kujitetea huku wakisuburi msaada hatuwezi sema hakuna umuhimu wa life jackets kisa kifo hakikimbiliki.

hali kadhalika huko porini simba anakula wanyama wengine ila swala akimuona simba lazima ajihami kujitetea asiliwe.

hivyo hata barabarani siku zote duniani kote wanaweka mikakati ya kupunguza ajali zinazoweza kuepukika, watu wafe kwa njia zingine ambazo zipo nje ya uwezo
Hii nadharia kuna sehemu haiingii akilini kwa kweli kuna mazingira yanasababisha vifo ambavyo sio mpango wa Mungu.
 
Ajali zinazotokea msimu wa sikukuu zimeendelea kuacha majonzi kwa Watanzania, baada ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu ofisi ya Msajili wa Hazina, Amos Nnko kufariki dunia.
Nnko amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Same, mkoani Kilimanjaro, jana mchana Jumapili, Desemba 22, 2024. Katika ajali hiyo, pia binti yake wa kwanza, Maureen Nnko amefariki.

Hayo yamethibitishwa na Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu leo Jumatatu Desemba 23, 2024 kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Katika taarifa hiyo, imeelezwa kuwa mke wa marehemu, Agnes Nnko na watoto-- Marilyn, Melvin na pamoja na mwanafamilia mwingine, Sylvana wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya KCMC na Mawenzi.

“Mipango ya mazishi inaendelea kuratibiwa na familia ya marehemu kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina,” imeeleza taarifa hiyo.

High speed kills
 
Hii nadharia kuna sehemu haiingii akilini kwa kweli kuna mazingira yanasababisha vifo ambavyo sio mpango wa Mungu.
nakuunga mkono, mfano ukisoma historia ya ujenzi wa panama canal, wafanyakazi kuna kipindi walikua wanakufa bila kujua tatizo ni nini, wakadhani wadudu aina ya sisimizi kwahiyo wakawa wanaweka kama vyombo vyenye maji kwenye miguu ya kitanda ili sisimizi au wadudu wengine wanaotambaa wasiweze panda kitandani kuwapa ugonjwa maana ndo walidhani wanaleta ugonjwa,
matokeo yake vifo vikaongezeka rate kwa kasi, mpaka wanakuja kustuka kua ni mbu ndo wanaleta ugonjwa "malaria" walisha pata vifo vingi maana yale maji yaliongeza mazalia ya mbu. so waanza jikinga na mbu na vifo vya ugonjwa ule vikapungua.

sema hapa sasa kila mtu na imani yake.

ila mimi naungana na wewe , maana kukitokea mafuriko alafu unalazimisha kuvuka mto na unaona watu wanavutwa a maji na kuzama alafu na wewe ukaingia hii hapa mchawi ni wewe
 
Taadhar n muhimu barabaran kwa safari ndefu Inatakiwa mabos mnatafuta madereva makin
 
Ajali zinazotokea msimu wa sikukuu zimeendelea kuacha majonzi kwa Watanzania, baada ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu ofisi ya Msajili wa Hazina, Amos Nnko kufariki dunia.
Nnko amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Same, mkoani Kilimanjaro, jana mchana Jumapili, Desemba 22, 2024. Katika ajali hiyo, pia binti yake wa kwanza, Maureen Nnko amefariki.

Hayo yamethibitishwa na Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu leo Jumatatu Desemba 23, 2024 kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Katika taarifa hiyo, imeelezwa kuwa mke wa marehemu, Agnes Nnko na watoto-- Marilyn, Melvin na pamoja na mwanafamilia mwingine, Sylvana wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya KCMC na Mawenzi.

“Mipango ya mazishi inaendelea kuratibiwa na familia ya marehemu kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina,” imeeleza taarifa hiyo.

wahanga wa ajali mama na watoto Mungu awape afya njema kwa mara nyingine
 
Kutoka nyumbani kwake kwenda Kilimanjaro airport ni about 30 kms.
Hili hakuliwaza, akachukua familia yote na Prado?
 
Pole Sana.

Ila mnapobarikiwa kupata high position na fedha muwe na utamaduni wa kuisaidia jamii na sio kuwa selfish.

Sio lazima mrudi kwenu kutambika na kufanya ibada za kishirikina .
 
Hii familia ilikuwa imefika mbali kimaisha,sasa wamerudi nyuma ,zaidi ya sifuri!
Kisa mafuta ya gari ya kupewa Bure!
Sasa kimbembe ukute mama ni mama WA nyumbani kama Mimi!
 
Back
Top Bottom