TANZIA Amri Athuman (King Majuto) afariki dunia akiwa hospitali ya Taifa Muhimbili

TANZIA Amri Athuman (King Majuto) afariki dunia akiwa hospitali ya Taifa Muhimbili

Innah lillah wa innah ilahir rajiuun! Mzee Majuyo Uliitendea haki Tasnia.
 
Pumzika kwa amani baba yetu,da wiki hii kwangu imekuwa ya shida pia nimempoteza shemeji yangu mpendwa Regina Ndunguru huko songea,Mungu awapumzishe kwa amani
 
Kuanzia lini Muhimbili, kupitia kwa msemaji wake, inatoa tamko rasmi mgonjwa akifariki?
 
Na Emmanuel J. Shilatu

Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za Msiba wa Msanii nguli na Bingwa wa tasnia ya Sanaa za uigizaji na vichekesho, Amir Athuman almaarufu "King Majuto" kilichotokea usiku wa Agosti 8, 2018 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.

Kifo hiki kimenikumbuka miaka ile ya zamani alipoanza kuwika na msemo wa hamsini, hamsini mia akiwa na muigizaji mwenzake mkongwe Marehemu Mzee Small.

Kwa wasiomjua vyema King Majuto alizaliwa mwaka 1948 jijini Tanga na kusoma shule Msambwini mkoani Tanga. Alianza kuigiza mwaka 1958 akiwa na umri wa miaka 9 akiigiza katika majukwaa.

Mzee Majuto maarufu kama King Majuto ni mtunzi, muigizaji, mwandishi wa mswada. Pia Mzee Majuto ni muigizaji wa kwanza kuandaa kazi zake katika mikanda na kuuza akiwa na Tanzania Film Company ( TFC).

Kwa sasa King Majuto ni mwigizaji mwenye mashabiki wengi kutokana maonyesho mbalimbali, vichekesho vyake aliyoshiriki.

King Majuto ni kipaji halisia cha kuzaliwa cha uchekeshaji kuwahi kutokea hapa nchini. Wenzake walikuwa kina Mzee Jongo, Hamis Kitambi, Fundi Said (Mzee Kipara) na Mama Haambiliki.

Msiba huu ni majonzi makubwa sana kwa familia, Wasanii, Tasnia ya Filamu nchini, Wapenzi wa kazi zake za sanaa na Taifa kwa ujumla.

Daima tutakukumbuka kwa ufundi, ustadi wa uigizaji wako, vituko vyako, tabasamu lako, upendo wako kwa kila Mtu.

Pumzika kwa amani Mfalme na Bingwa wa vichekesho wa kipindi chote hapa nchini Mzee "King Majuto".

Inna lillaahi wainna ilaihi raajiuun.

*Shilatu E.J*
 
TANZIA: Msanii wa vichekesho Mzee King Majuto amefariki dunia usiku wa leo Agosti 8, 2018 katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili alipokuwa anapatiwa matibabu.

Msemaji wa hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha amesema Mzee Majuto alipelekwa hospitalini hapo Julai 31 baada ya hali yake kubadilika.

“Hali yake ilibadilika majira ya saa tisa alasiri ya leo hivyo kuhamishwa kutoka jengo la Sewahaji kwenda ICU. Ilipofika saa 1.30 jioni hii hali yake ilibadilika zaidi na madaktari walijitahidi kuokoa maisha yale bila mafanikio. Ilipofika saa 2 usiku alikata roho,''
View attachment 830443
View attachment 830484
View attachment 830455
Rais Magufuli na Mama Janeth Magufuli waliopokwenda kumjulia hali King Majuto aliyelazwa katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam leo Januari 31, 2018.

Pia soma >
Mzee Majuto: Tanzanian Movie and Comedy Legend
Mzee Majuto atangaza rasmi kuacha kuigiza, sasa kumrudia Mungu wake
Mwakyembe Kuivaa kampuni iliyomdhurumu Mil 25 Mzee Majuto.
Haya ndio maisha halisi anayoishi mzee Majuto
--
Wasifu
Amri Athuman’ King Majuto’ alizaliwa mwaka 1948 jijini Tanga na kusoma shule Msambwini, Tanga, alianza kuigiza 1958 akiwa na umri wa miaka 9 akiigiza katika majukwaa Mzee Majuto maarufu kama King Majuto ni mtunzi, muigizaji,mwandishi wa mswada.


Na ndiye muigizaji wa kwanza kuandaa kazi zake katika mikanda na kuuza akiwa na Tanzania Film Company ( TFC) Kwa sasa King Majuto ni mwigizaji mwenye mashabiki wengi kutokana maonyesho mbalimbali, vichekesho vyake aliyoshiriki nchi mbalimbali.

Habari zaidi, soma=>Mzee Majuto: Tanzanian Movie and Comedy Legend
hakika kila nafsi itaonja mauti,mkumbuke Muumba wako cku za ujana wako kabla hazijaja ciku zilizo mbaya, Parapanda italia parapandaaaa!!!!!!!!!! Roma voice
 
RIP King Majuto tutakukumbuka daima kwa kazi zako zilizotupa furaha na vicheko mioyoni mwetu
 
Back
Top Bottom