TANZIA Amri Athuman (King Majuto) afariki dunia akiwa hospitali ya Taifa Muhimbili

TANZIA Amri Athuman (King Majuto) afariki dunia akiwa hospitali ya Taifa Muhimbili

Sio msambwini ni msambweni, Allah amueke anapostahili
 
Huyu Mzee alikuwa mtu wa kufurahi wakati wote, hata akiumwa alikuwa na tabasamu lake,
R.I.P Majuto the King.
 
Mungu ndio anajua wapi mja wake huelekea anapofikwa na umauti baada ya kuingizwa kaburini kwa imani yangu ndio mana nikasema hivo
Samahani imani yako ni ya dini gani??
 
Wewe mbele yetu sisi nyuma yako ,usisahau kumsalimia Sharo Millionea.

R.I.P. Mzee wetu
 
Hakika ya mauti kweli humfika kila kiumbe, pumzika kwa aman mzee wetu mbele yako nyuma yetu
 
Kaburi ndio Ghetto pekee la Haki, Kila nafsi yenye Uhai ni lazima ionje Mauti. May his Soul Rest In Eternal Peace
 
INNA LILLAH WA INNA ILLAHI RAJIUN.
POLENI WOTE MNAOHUSIKA NA MSIBA HUU.
 
TANZIA: Msanii wa vichekesho Mzee King Majuto amefariki dunia usiku wa leo Agosti 8, 2018 katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili alipokuwa anapatiwa matibabu.

Msemaji wa hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha amesema Mzee Majuto alipelekwa hospitalini hapo Julai 31 baada ya hali yake kubadilika.

“Hali yake ilibadilika majira ya saa tisa alasiri ya leo hivyo kuhamishwa kutoka jengo la Sewahaji kwenda ICU. Ilipofika saa 1.30 jioni hii hali yake ilibadilika zaidi na madaktari walijitahidi kuokoa maisha yale bila mafanikio. Ilipofika saa 2 usiku alikata roho,''
View attachment 830443
View attachment 830484
View attachment 830455
Rais Magufuli na Mama Janeth Magufuli waliopokwenda kumjulia hali King Majuto aliyelazwa katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam leo Januari 31, 2018.

Pia soma >
Mzee Majuto: Tanzanian Movie and Comedy Legend
Mzee Majuto atangaza rasmi kuacha kuigiza, sasa kumrudia Mungu wake
Mwakyembe Kuivaa kampuni iliyomdhurumu Mil 25 Mzee Majuto.
Haya ndio maisha halisi anayoishi mzee Majuto
--
Wasifu
Amri Athuman’ King Majuto’ alizaliwa mwaka 1948 jijini Tanga na kusoma shule Msambwini, Tanga, alianza kuigiza 1958 akiwa na umri wa miaka 9 akiigiza katika majukwaa Mzee Majuto maarufu kama King Majuto ni mtunzi, muigizaji,mwandishi wa mswada.


Na ndiye muigizaji wa kwanza kuandaa kazi zake katika mikanda na kuuza akiwa na Tanzania Film Company ( TFC) Kwa sasa King Majuto ni mwigizaji mwenye mashabiki wengi kutokana maonyesho mbalimbali, vichekesho vyake aliyoshiriki nchi mbalimbali.
RIP King Majuto! Alikuwa genious kwenye kila alichokifanya, he really kept us entertained as we were growing up and i could watch his films more than ten times na nilicheka kila wakati! A big blow indeed but a life well lived!
 
RIP gwiji... umeenda na tasnia yako... Bakurutu baloba..nzela ya bato nyoso [emoji22] [emoji22]
 
Upumzike kwa Amani mzee Majuto - vijana wangu wamesikitika sana walipopata habari hizi!
 
Back
Top Bottom