Wakuu bila shaka na nyinyi ni mashahidi tosha kwamba bwana yule au ukipenda muite Jiwe huwa haudhurii kabisa misiba yoyote ile yupo radhi akafungue hata tawi la benki au jambo lolote lile ambalo halina tija kwa wakati huo lakini si kuhudhuria misiba mpaka ikafika mahala watu wakaanza kumuhisi huenda ni mshirikina.
Lakini kwa maajabu kabisa bila kutarajia tumemuona jiwe akihudhuria msiba wa Amri Athumani Majuto kitu ambacho baadhi ya watu wameingiwa na mashaka kwamba huenda kuna kitu kimejificha maana si hali ya kawaida.
Tusubiri baada ya maziko kuna mambo makubwa yataibuka kama kipindi kile cha msiba wa Masaburi yalivyoibuliwa mambo yasiyojulikana hata na wana familia ila jiwe aliyaropoka jambo ambalo halikuwafurahisha wanafamilia.