Amri Kiemba: Mechi kati ya Simba na Wydad ni Ngumu

Amri Kiemba: Mechi kati ya Simba na Wydad ni Ngumu

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
AMRI KIEMBA|+

🗣“Kwa mazingira na namna ambavyo hizi timu zilivyo [Simba na Wydad Casablanca] na kwa heshima ya mpira wa miguu Simba inaweza kushinda kwa Mkapa.”

🗣“Kwa takwimu sasa ndio unakuja kugundua ugumu wa mechi, ugumu unaletwa na timu ambazo zinacheza. Wydad ni bingwa mtetezi lakini ameanza kwa nguvu kuutetea ubingwa.”

🗣“Kuna timu inachukua ubingwa halafu msimu unaofata anakuwa hoi! Wydad anatetea kama ndio anautafuta ubingwa, hicho ntio kitu ambacho kinaweza kuleta tofauti.”

🗣“Ukiangalia bingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika RS Berkane, msimu huu ipo hoi na imetolewa hatua za mapema.”

🗣“Wydad ni timu ngumu kwa Simba lakini kwa historia ya Simba uwanja wa Mkapa inaonekana ni mechi ngumu pia kwa Wydad kuzuia kile ambacho Simba imekuwa ikikifanya uwanja wa Benjamin Mkapa.”

🗣“Inawezekana kumbukumbu za Raja bado zipo kwa watu wengi, inawezekana kilichoikuta Simba mbele ya Raja tayari kimekuwa somo ambalo wakati wanakutananao hawakuwanalo.”

🗣“Nyakati ambazo Simba ilifanikiwa kushinda mbele ya Al Ahly, AS Vita na hata kutoka sare na TP Mazembe, walikuwa wanaziheshimu hizo timu na historia zao lakini kwa Raja, Simba walikuwa wazi sana kama wanacheza mechi ya Ligi Kuu!”

🗣“Sioni Simba wakifanya hivyo tena dhidi ya Wydad kufunguka bila kujua wanawazuiaje.”

🗣“Kwa hiyo Simba kushinda uwanja wa Benjamin Mkapa inawezekana lakini matokeo ya jumla yatategemea zaidi mechi ya pili.”
 
Wydad Casablanca huwezi kuwafunga kwa kutegemea uchawi, na ukitegemea viwango vya wachezaji ndio unakufa zaidi.

Simba wajiandae kwa kusajiri wachezaji wenye viwango msimu ujao.

Kwa msimu huu shughuri ndio imeishia hapo.
 
Jamaa muoga sana. Anaogopa kupigwa mawe. Anaongelea kwenye ncha haeleweki ana msimamo gani.
Kweli kabisa. Eti “Kwa hiyo Simba kushinda uwanja wa Benjamin Mkapa inawezekana lakini matokeo ya jumla yatategemea zaidi mechi ya pili.” Sasa nani asiyejua hilo?
 
Mbona leo mvua inaonekana kukata, kwenye mida ya saa 7 kwenda mbele jua litakuwepo zuri tu.
Hao wydad watashindwa kuendana na hali ya pitch, simba wanaweza kushinda mechi hii.
 
Back
Top Bottom