Amshambulia ofisa wa polisi ubalozi wa marekani na kutaka kupora silaha

Amshambulia ofisa wa polisi ubalozi wa marekani na kutaka kupora silaha

Curtiz

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2021
Posts
1,364
Reaction score
2,583
Wanajamvi kama kichwa kilivo. Nimeitoa huko mtandao wa us embassy hapa Tanzania. Kuna mkulungwa alimshambulia askari polisi anayelinda ubalozi wa US pale msasani na kutaka kupora bunduki. Lakini alishindwa na wakamdhibiti bila madhara yoyote makubwa kuripotiwa.
==
Tarehe: 15 Mei, 2025
Mahali: Ubalozi wa Marekani, Dar es Salaam – 686 Old Bagamoyo Rd, Msasani


Tukio: Tarehe 10 Mei, 2025, mshambuliaji asiye na silaha alimvamia askari wa Jeshi la Polisi la Taifa la Tanzania aliyekuwa amepangiwa lindo mbele ya Ubalozi wa Marekani na kujaribu kuchukua silaha yake. Mshambuliaji alikamatwa haraka na hakuna mfanyakazi wa ubalozi wala mtu yeyote aliyekuwa karibu kujeruhiwa.

Maeneo yanayotembelewa na raia wa Marekani, wageni kutoka nchi nyingine, na watalii yanaendelea kuwa malengo yanayovutia kwa makundi ya kigaidi yanayopanga kufanya mashambulizi. Makundi ya kigaidi yanaweza kushambulia bila onyo au kwa onyo dogo sana. Malengo yanayowezekana ni pamoja na hoteli, balozi, mikahawa, maduka makubwa na masoko, shule, vituo vya polisi, sehemu za ibada, na maeneo mengine yanayotembelewa na wageni na watalii.

==
May 15, 2025

Location: U.S. Embassy Dar es Salaam, 686 Old Bagamoyo Rd, Msasani

Event: On May 10, 2025, an unarmed assailant attacked the Tanzanian National Police Force officer posted in front of the U.S. Embassy and attempted to take control of his weapon. The assailant was quickly apprehended, and no employees or bystanders were harmed.

Locations frequented by U.S. citizens, other foreigners, and tourists continue to be attractive targets to terrorists planning to conduct attacks. Terrorist groups could attack with little or no warning. Potential targets include hotels, embassies, restaurants, malls and markets, schools, police stations, places of worship, and other places frequented by foreigners and tourists.
 

Attachments

  • Screenshot_20250516_115954_Chrome.jpg
    Screenshot_20250516_115954_Chrome.jpg
    399.3 KB · Views: 40
Baada ya kuhojiwa tutaskia alijaribu kutoroka akapigwa risasi kumzuia lakini bahati mbaya akafa.

Hiyo ndo principle
 
HUYO AFANDE APANDISHWE CHEO KWA KUWA NA HURUMA..HUYO MVAMIZI ILITAKIWA MAPEPO YAMTOKE AKIWA AHERA..
 
Kumbe polisi wetu angewachokoza wayues wenyewe😂😂😂

Sema depression is real wakuu
 
Itakua jamaa zetu wale wa kwenye nyuzi za Israel na Palestina.
 
Back
Top Bottom