BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Jeshi la Polisi mkoani Tabora linamshikilia Ali Idd Mkonongo, mkazi wa Kijiji cha Inala kwa tuhuma za kumuua mke wake aliyefahamika kwa jina la Mariam Yusuph kwa kumpiga na kitu kizito kichwani wakati akiwa amelala majira ya saa sita usiku, kisha kuuchukua mwili na kuutumbukiza kisimani kwa lengo la kuficha ushahidi.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Richard Abwao, mwanaume huyo alitekeleza mauaji hayo baada ya kutoka kupigiwa ramli kwa mganga wa kienyeji na kuelezwa kwamba atamuona mchawi wake ndotoni. Baada ya kumuota mkewe, Ali amiamua kufanya mauaji hayo akitekeleza kile alichokiota ndotoni.
Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya kukamilisha taratibu za uchunguzi dhidi ya mauaji hayo.