Ndio. Yaweke hapa na uonyeshe mahali pameandikwa muue.
Kama haijaandikwa hivyo usilete maandiko.
Zingatia Aya zote Ila jibu lipo Aya ya 29, iliyokolezwa
Mambo ya Walawi 18:22
Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo.
Mambo ya Walawi 18:23
Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni uchafuko.
Mambo ya Walawi 18:24
Msijitie unajisi katika mambo hayo hata mojawapo; kwa maana hizo taifa nitakazozitoa mbele zenu zimekuwa najisi kwa mambo hayo yote;
Mambo ya Walawi 18:25
na hiyo nchi imekuwa najisi; kwa ajili ya hayo naipatiliza uovu wake juu yake, na hiyo nchi yatapika wenyeji wake na kuwatoa.
Mambo ya Walawi 18:26
Kwa hiyo mtazishika amri zangu na hukumu zangu, wala msifanye machukizo hayo mojawapo; yeye aliye mzalia, wala mgeni aketiye kati yenu;
Mambo ya Walawi 18:27
(kwa kuwa hao watu wa nchi wameyafanya machukizo haya yote, hao waliotangulia mbele zenu, na hiyo nchi imekuwa najisi
😉
Mambo ya Walawi 18:28
ili kwamba hiyo nchi isiwatapike na ninyi pia, hapo mtakapoitia unajisi, kama ilivyoitapika hiyo taifa iliyotangulia mbele yenu.
Mambo ya Walawi 18:29
Kwani mtu awaye yote atakayefanya machukizo hayo mojawapo, nafsi hizo zitakazoyafanya zitakatiliwa mbali na watu wao.
Mambo ya Walawi 18:30
Kwa ajili ya hayo yashikeni mausia yangu, ili kwamba msifanye kabisa desturi hizi zichukizazo mojawapo, zilizotangulia kufanywa mbele zenu, wala msijitie unajisi katika mambo hayo; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.