Hawa siyo watu wa Elimu na kufatilia mambo, ndiyo maana wamekuwa kama wanyama. Hii ni laana, yaani wamekuwa vipofu kabisa wa akili mpaka moyo. Hajui ya kuwa Imamu wa lugha ya Kiarabu hakuwa Muarabu, ambaye ni Sibawayhi.Halafu huyo mpaka leo hajui kama kuna “wamatumbi” wanawafundisha waarabu Dini?
Nimewakumbuka “Wamatumbi” Shaikh Muhammad Amaan al Jami na Shaikh Muhammad Adam al Ethiopi (Allah awarehemu).
Kwetu sisi Waislam elimu haina mwenyewe, elimu ina watu wake (na watu wake ni wale walioichukua).
Katika Wamatumbi wenzetu umemsahau Shaykh Abdulrahman bin Awfi Koni, huyu ni mwanachuoni mkubwa wa Lugha ya Kiarabu, ulienda leo Madina, kwenye lugha ya Kiarabu anarejewa yeye. Ukisoma tarjama ya Shaykh Abdullah bin Abdulrahiim Al Bukhariy Allah amuhifadhi, Shaykh Bukhariy anasema amesoma "Mulhatul I'raab" kwa Shaykh Abdulrahman bin Awfi Koni.
Kama ulivyosema elimu ina watu wake haina mwenyewe.