the guardian 17
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 395
- 570
Wazee wivu wa hivi kwa dada zenu mnatoa wapi?
=====
Jeshi la Polisi limemkamata Festo Francis Makambula (34) Mkulima na Mkazi wa Kijiji cha Mululu Wilaya ya kipolisi Ruhembe mkoani Morogoro kwa tuhuma ya kumuua Rashid Bandei Kiupi (49) mlinzi wa kampuni ya Stigmatin.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama amesema tukio hilo limebainika Februari 18, 2025 eneo la Mlulu-Kisanga ambapo mtuhumiwa alimvamia Rashid ambaye ni mpenzi wa Dada yake wakati akielekea kazini majira ya asubuhi na kumshambulia kisha kumchoma kisu kifuani na kupelekea kifo chake.
Uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha tukio hilo ni ugomvi unaohusiana na mahusiano ya kimapenzi ambapo mtuhumiwa hakukubaliana na Rashid (marehemu) kumuoa dada yake.